Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

Kamala ni msanii na mzushi hana lolote ndiyo maana hata wahaya wenzake wamenyima kura.
Yeye ndiye mbumbumbu maana anapingana hata na BOSI wake na Mwenyekiti wa Chama chake-JK.

Soma hii habari hapa chini ambayo JK mwenyewe alikuwa anaomba wenye viwanda WAPUNGUZE BEI.
Asifikiri watu hatujui Uchumi kiasi hicho. Bei ya Saruji(Cement) inaweza kupungua kabisa hata kama haiwezi kuiwa 5,000/= kwa mfuko.
Kanuni za Bei kwa kutumia ile inaitwa DEMAND versus SUPPLY curve kuwa DEMAND au uhitaji wa bidhaa unapokuwa mkubwa na wakti huo huo bidhaa inayozalishwa ni kidogo BEI LAZIMA IWE JUU.

Kwa hiyo basi kama ukifanya kinyume chake yaani BIDHAA izalishwe kwa wingi(kuwe na surplus) kwenye soko automatically BEI itapungua.
Kadri bidhaa inavyokuwa nyingi sokoni bei inashuka na kadri bidhaa inavyopungua bei lazima ipande. Hapa tunazungumzia Saruji.

Kwa hiyo kama Dr. Slaa wa CHADEMA akiingia pale Ikulu akahakikisha saruji inazalishwa kwa wingi nina hakika bei itatelemka. Kwanza watu wanatakiwa kujiuliza malighafi ya saruji ni nini na inatoka wapi. Saruji haihitaji malighafi toka nje ya nchi kwa maana ya gharama za uagizaji kwa fedha za kigeni.

Nakumbuka vizuri sana kuwa SARUJI ya Kenya ni rahisi kuliko ya Tanzania. Uliza watu wengi wanaokaa mipakani wanajenge saruji toka Kenya inayoitwa Bamburi. Mfukio ni Kshs.650-700 sawa na kama Tzhs.7000-8500. Saruji ya Tanga Cement au Wazo iko kwenye Tshs 12,000/-15,000/=na ikifikishwa huko bara a Kanda ya Ziwa inafikia Tsh.18,000-20,000/=.

Kamala hasemi kweli hapa yeye ndiye mwongo mkubwa. TUNASEMA HIVI CCM WAMESHINDWA KUZUIA MFUMKO WA BEI KUTOKANA NA KUPOROMOKA KWA THAMANI YA SHILINGI YETU. NANI ALAUMIWE. Slaa au JK na serikali yake??

HATUDANGANYIKI. KAMALA ASEME JINGINE KAMA NI HILI YEYE NDIYE MBUMBUMBU MZUNGU WA RELI. Pambaf!



JK awaasa wenye viwanda kupunguza bei ya saruji


By Lulu George

29th May 2010


JK(30).jpg

Rais Jakaya Kikwete



Rais Jakaya Kikwete, amewataka wafanyabiashara wenye viwanda vya saruji, kuzalisha bidhaa zenye ubora na kupunguza bei, ili kuongeza idadi ya watumiaji.
Alitoa rai hiyo jana, baada ya kuzindua kinu na mtambo wa kufungashia bidhaa hiyo katika kiwanda cha saruji cha Simba, kilichopo mkoani hapa.
Uzinduzi wa mitambo hiyo ni hatua mojawapo ya kukabiliana na uhaba wa saruji unaolikabili Taifa.
Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania inaongeza kasi ya uzalishaji wa saruji inayofikia tani milioni tatu kwa mwaka, na mahitaji ni tani milioni mbili huku matumizi kwa mtu mmoja ni kilo 50.
Kiasi hicho kinatokana na viwanda vya saruji vya Simba,Wazo Hill na Mbeya, ambapo pia imebainika kuwepo ziada ya tani milioni moja ya saruji kwa mwaka.
"Naomba niwatake wenye viwanda vya saruji hapa nchini, kwamba upanuzi wa uzalishaji huu uende sambamba na upunguzaji wa bei kwa sababu, bado watu wanajenga nyumba za miti na matofali ya kuchoma," alisema.
Rais Kikweta alisema anafanya ushawishi kwa wawekezaji wanaokusudia kujenga viwanda vipya vya saruji katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Tanga, Dar es Salaam na Pwani.
Pia, aliwataka wenye viwanda hivyo kutumia malighafi kutoka ndani ya nchi.
Naye Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko Dk. Mary Nagu, alisema kiwanda hicho kiliwekeza kiasi cha Dola milioni 146 za Marekani na kwa sasa kinazalisha tani milioni 1.250 za saruji kwa mwaka.
Wakati huo huo, Rais Kikwete, ameweka jiwe la msingi katika eneo la Mikocheni jijini Tanga, ikiwa na hatua moja ya kuanza rasmi ujenzi wa barabara ya Tanga hadi Horohoro yenye urefu wa kilometa 65 kwa kiwango cha lami.
Barabara hiyo ambayo inatarajiwa kugharimu kiasi cha Shilingi bilioni 70 hadi itakapokamilika, itasaidia kuboresha mawasiliano na kuongeza ushirikiano wa kibiashara kati ya Kenya na Tanzania.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Kikwete aliwataka watanzania kuchangamkia fursa za kibiashara zitakazojitokeza mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo, alisema ujenzi huo unaosimamiwa na mkandarasi, kampuni ya Sinohydro Cooperation kutoka China, unatarajiwa kukamilika ifikapo Aprili, 2012.
Naye Waziri wa Miundombinu, Dk.Shukuru Kawambwa, alisema barabara hiyo itakapokamilika, itawahudumia watu takriban milioni 6.5 kutoka mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Pwani.
Pia alisema itakuwa kiungo kwa bandari ya Mombasa nchini Kenya na Tanzania.




SOURCE: NIPASHE


0 Comments | Be the first to comment
 
Kweli huyu kamala ni kihiyo aliyefoji vyeti. Anapozungumzia simenti kwa mkoa mmoja tu wa mwanza anamaanisha hata wanunuzi wa mikoa ambayo viwanda vipo wataenda kuinunulia mwanza? Angejaribu kutoa mchanganuo wa bei jinsi zinavyowezatofautiana toka kituo kimoja hadi kingine tungeweza angalau kuona unafuu wa uzuzu wake.
 
Kuweni macho na ahadi zisizotekelezeka

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Diodorus Kamala

Ahadi zinazotolewa na baadhi ya wagombea uongozi nchini katika kampeni zinazoendelea za uchaguzi mkuu zikitekelezwa, huenda zikawaweka Watanzania pabaya, imebainika.

Taarifa ya kitaalamu imebaini, kwamba kuna wagombea urais ambao wamekuwa wakiwaahidi Watanzania kuondoa kodi katika saruji watakapochaguliwa kuingia Ikulu.

Taarifa ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, iliyotolewa jana na Waziri mwenye dhamana, Dk Diodorus Kamala, ilisema ahadi hiyo inapotosha wananchi na kuwapa matumaini ambayo hayatekelezeki.

Alisema chini ya kifungu 2(4)(c) cha Itifaki ya Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki, nchi wanachama zilikubaliana kuweka na kutekeleza wigo wa pamoja wa ushuru wa forodha kwa bidhaa zitokazo nje ya Jumuiya.

Aliongeza kuwa wigo huo ulianza kutekelezwa Januari mosi, 2005 na viwango vilivyokubalika ni asilimia 0 kwa malighafi, pembejeo za kilimo, dawa na mitambo; asilimia 10 kwa bidhaa zilizosindikwa kiasi; na asilimia 25 kwa bidhaa zilizokamilika katika uzalishaji. Kamala alisema, bidhaa nyeti ushuru wake ni zaidi ya asilimia 25.

“Hivyo nchi binafsi mwanachama haina mamlaka ya kurekebisha viwango vya kodi ya forodha … mfumo wa uamuzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hauruhusu nchi moja mwanachama, kufuta ushuru wa forodha wa bidhaa ya aina yoyote ile, ikiwamo saruji.”

Alisema, kuwaahidi wananchi jambo ambalo halijakubaliwa na viongozi wa nchi zingine wanachama ni kuwadanganya. “Kwa kawaida muungana na mkweli, hatoi ahadi ya jambo ambalo uamuzi au utekelezaji wake unategemea ridhaa ya mamlaka nyingine iliyo juu yake.”

Alihoji: “Je, ombi la kufuta ushuru likikataliwa na nchi zingine wanachama itakuwaje? Je, mhusika atawarudia wapiga kura na kuwaambia kuwa alitoa ahadi hewa au isiyo na mantiki?”

Alisema, saruji ni miongoni mwa bidhaa zilizowekwa katika kundi la bidhaa nyeti, ambazo wazalishaji wa nchi zinakotoka, hupewa ruzuku ambapo wazalishaji wa EAC hawapewi ruzuku hiyo, lakini wanaweza kuzalisha kwa ufanisi.

Hatua hiyo alisema kuwa inachangia katika maendeleo ya viwanda, ajira, mapato ya Serikali na kuokoa fedha za kigeni, ambapo pia kuweko kwa ruzuku kwa wazalishaji wa nje huku wa ndani wakikosa, kunaweka mazingira ya ushindani usio sawa katika soko la Jumuiya dhidi ya wazalishaji wa Afrika Mashariki.

Alisisitiza, kwamba kwa upande wa saruji, kuanzia Januari mosi 2005 ushuru wake ni asilimia 55 na nchi wanachama zilikubaliana ushuru huo ushuke kila mwaka hadi asilimia 35 kuanzia Januari mwaka huu na ubaki katika kiwango hicho.

Alitaja bidhaa zingine katika kundi hili na kiwango cha ushuru kwenye mabano, kuwa ni sukari (100%), mahindi (50%), ngano (35%), mchele (75%), maziwa (60%), tumbaku (35%), sigara (35%), khanga, kikoi, kitenge (50%), mashuka (50%), magunia ya jute (50%), viberiti na betri za redio (35%).

“Kwa hiyo kufutwa ushuru si tu kutasababisha viwanda kufa, lakini mapato ya serikali na ajira vitapungua sambamba na uanachama wa Tanzania katika Jumuiya kuwa shakani.

“Sina hakika kama misamaha ya kodi inaendana na ahadi dhaifu za elimu na afya bure kwa Watanzania zinazotolewa na wapinzani.

Huwezi kutoa elimu bure na afya bure na wakati huo huo, usamehe ushuru wa forodha,” alisema Kamala.

Alisisitiza pia kuwa, hatua ya kupunguza ushuru wa forodha kwenye saruji ilichukuliwa kitambo, lakini kufutwa kukashindikana kutokana na hali halisi iliyobainishwa awali.

“Mwaka 2005 ushuru ulikuwa asilimia 55 ukapunguzwa hadi asilimia 25 ya sasa … hatua hii ilichukuliwa kutokana na maandalizi ya Kombe la Dunia, Afrika Kusini na Olimpiki, China.

Alisema, wakati huu ambao ushuru kwa muda umeshushwa hadi asilimia 25 huku ikifikiriwa kama utarejea asilimia 35, tayari wazalishaji saruji wameanza kulalamika kuwa wenzao wa nje hususan Misri, wanapata ruzuku na hivyo kuiuza kwa bei ndogo katika Jumuiya.

“Kwa maana hiyo kufutwa kabisa kwa ushuru, kutasababisha viwanda kufa na dhana ya kuwapa wananchi saruji ya bei nafuu kufa pia … bei ya bidhaa yoyote duniani, hutegemea upatikanaji wake na mahitaji ya soko.

“Pindi viwanda vya saruji vya Afrika Mashariki vikifa, wazalishaji kutoka nje ya Jumuiya, watashawishika kupandisha bei, kwa kuwa sasa watakuwa wamejengewa ukiritimba katika soko kwa kukosa mpinzani wa ndani,” alisema Waziri.

Katika kampeni zake nchini, mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa, amekuwa akiwaahidi wananchi kuwa akiingia Ikulu atapunguza bei ya saruji hadi Sh 5,000 kwa mfuko wa kilo 50, ili wananchi wajijengee nyumba bora za kisasa.
 
naona serikai yote ni feki. Maana wengi wao wanaitwa madoctor. Mfano dr jk, kamala, nchimbi, chegeni, makongoro, makamba, nk,taja mwenyewe. Kwa style hii nchi itaenda kweli, lazima ikwame tuu.
 
naona serikai yote ni feki. Maana wengi wao wanaitwa madoctor. Mfano dr jk, kamala, nchimbi, chegeni, makongoro, makamba, nk,taja mwenyewe. Kwa style hii nchi itaenda kweli, lazima ikwame tuu.
haaaa hata makamba!?????????
 
Rais Mtarajiwa Dr Slaa angekuwa mbumbumbu basi Kikwete asingeukacha mdahalo na kuingia mitini. Utaogopa vipi kufanya mdahalo na mbumbumbu? Raisi wa nchi anapoingia mitini kufanya mdahalo na mbumbumbu ni nani ambaye ni mbumbubu kuliko mwenziye? Huhitaji kwenda shule kujibu hili swali :peace:

Kweli kabisa
 
Nitamuheshimu yule aliyekaa kimya mbele ya mbumbumbu kuliko yule aliyejishughulisha kujibishana nae....!
 
Hivi tulitegemea nini sisi watanzania kwa kuongozwa na viongozi wenye mawazo mfu kama ya huyu Dr Kamala? Naililia Tanzania ya Nyerere na Sokoine.
 
angelikuwa na akili asingepigwa chini kwenye kura za maoni hana jipya anatafuta huruma kwa jk ambayo hatoipata kwani mbayuwayu hatoruka,subiri 31 oktoba,atapata majibu
 
Yeye si ndo alikaa kwenye hivyo vikao vya kupitisha makubaliano hayo hakuona kama yataumiza wa TZ, ukweli wengi bado wanakaa kwenye matembe! mi nafikiri ndo mana hata CCM wenyewe waliona hafai!
 
yeye si ndo alikaa kwenye hivyo vikao vya kupitisha makubaliano hayo hakuona kama yataumiza wa tz, ukweli wengi bado wanakaa kwenye matembe! Mi nafikiri ndo mana hata ccm wenyewe waliona hafai!
jamani haya watu akili wanazo basi, kunahaja ya kupima iq
 
Kweli Waziri Kamala ameonyesha ni ngumbalu katika masuala ya uchumi. Kinachoshindikana ni nini! Kwani hizo vocha zinazotolewa na serikali kwa
kwa ununuzi wa mbolea lengo lake ni nini? Sikuwawezesha wakulima kununua mbolea hiyo kwa bei iliyochini ya soko. ni kitu gani kitamzuia Dr. wa
wakweli kutumia utaratibu kama huo pinde akiukwaa urais. Na hili suala la gharama za usafirishaji, huko nyuma tulikuwa na kitu kilichojulikana kama "pan-teritorial pricing" kwa bidhaa muhimu kama vya ujenzi. Chini ya mfumo huo uliundwa utaratibu ambapo walaji walio karibu na chanzo cha bidhaa husika, walikuwa wanafidia gharama za kusafirisha bidhaa hiyo hadi mikoa ya pembezoni. Mpango huo uliwezesha kuwepo kwa bei moja katika nchi nzima kwa bidhaa muimu kama mafuta ya petroli, vifaa vya ujenzi n.k. Ni kushamili kwa ufisadi kulikosababisha utaratibu kusitishwa. Kwa mfano transporter wa mafuta alikuwa akipakia mafuta kutoka dsm kuyapeleka Mbeya, lakini anayateremsha dsm huku anadai malipo ya kusafirisha mafuta hayo hadi Mbeya. Kwa udhalimu wa aina hiyo, kiasi kikubwa cha mafuta yaliyokuwa yakitumika dsm na mikoa jilani yalilipiwa gharama ile ile ya usafiri kama kwamba yamesafirishwa hadi mikoa ya pembezoni. Kushindwa kwa serikali kudhibiti hali hiyo, pamoja na hali ya serikali kutojali watu wake,ndiyo ilisababisha utaratibu huo kutupiliwa mbali. Hii haimanishi, utaratibu huo hauwezi kurejwshwa.
 
Huyu ni mvivu wa kufikiri..mambo ya Tanzania yaamuliwe na EAC members....wananchi wa jimbo lake walikuwa werevu sana sana kumpiga chini!
 
Kamala nakuombea kwa Mungu yakupate mabaya, ikiwezekana uangukiwe mnazi upate ngeo kubwa.

Kuna mamlaka gani iliyo juu ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutekeleza mambo yanayowafaa watanzania???? Huu unaousema kuwa haiwezekani ni upuuzi ambao kama mawaziri wote walioteuliwa wana mitizamo kama yako hatuwataki hata kidogo.
 
Back
Top Bottom