Dk Slaa Mbumbumbu - Kamala

Wa Ndima

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
1,526
323
Leo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Diodorus Kamala, alisema Dk Slaa katika uchumi ni mbumbumbu na inaonekana anazungumza asichokijua na kudanganya wananchi.

Dk Kamala alisema ahadi hiyo ni ya uongo kwani Sh 5,000 ni gharama ya usafirishaji wa mfuko kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa njia ya reli na tani moja ya saruji ya mifuko 20 ni Sh 100,000 hivyo gharama kwa mfuko kuwa Sh 5,000 sawa na bei anayowaahidi Watanzania. Alisema gharama za uzalishaji si chini ya Sh 7,000 kwa mfuko na kabla ya kuongeza gharama nyingine, mfuko wa saruji unapofika Mwanza gharama inakuwa zaidi ya Sh 12,000, hivyo kwa bei yake kuwa kubwa.

Dk Kamala alisema hoja hiyo ni ndoto ambayo hata viongozi wa nchi tajiri duniani hawatarajii kuiota mbali na kuitekeleza na huko ni kudanganya wananchi. Akizungumzia hoja ya makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwamba yanaumiza Watanzania, alisema Dk. Slaa anapotosha kwani msingi mkuu wa makubaliano hayo ni ushirikiano huo kujengwa hatua kwa hatua kulingana na ridhaa ya wananchi. “Serikali imekuwa ikizingatia msingi huu kikamilifu kwa kushirikisha wananchi, likiwamo Bunge ambalo Dk Slaa amekuwamo kwa miaka mingi, mfumo huu unaziwezesha nchi wanachama kupata fursa ya kujipanga vema katika utekelezaji na kuitumia ngazi moja kuwa msingi wa kupanda ngazi inayofuata ya utangamano,“ alisema Kamala.

Kuhusu mfumo wa kodi katika jumuiya, alisema si kweli kwamba aliuanzisha yeye, kwa kuwa yalianza kabla hajawa waziri na haiwezekani ushuru ufutwe bila kujadiliana na kukubaliana nchi wanachama, hivyo akasema Dk.Slaa hawezi kufuta ushuru huo kwani ni lazima ajadiliane na viongozi wa EAC.

Kuhusu viwango vya VAT alisema Dk. Slaa ameonesha hajui kuwa kodi hiyo si ya Afrika Mashariki na kiasi cha VAT anacholipa mlaji kinategemea bei ya bidhaa katika soko, huku akitolea mfano wa maji ya kunywa ya ujazo wa nusu lita, ambayo Tanzania yanauzwa Sh 500 na Kenya Sh 800 ingawa Mkenya analipa VAT ya asilimia 16 na Mtanzania asilimia 18; Mkenya analipa kiasi kikubwa kuliko Mtanzania.

Alisema kabla Dk. Slaa kusema Tanzania imeliwa, kwa kuwa na kiwango cha juu cha VAT Afrika Mashariki, alitakiwa kuelewa kwamba VAT si kodi ya Afrika Mashariki na katika uchumi, huwezi kulinganisha viwango vya VAT kabla ya kuangalia mfumuko wa bei kwenye nchi unazotaka kulinganisha, na kabla haujakokotoa, lazima uangalie viwango vya thamani ya kubadilisha fedha na gharama ya maisha.

Alimtaka Dk. Slaa kuwaomba radhi Watanzania kwa kuwadhalilisha akiwaita mbumbumbu, kielimu na katika kufanya biashara, huku akitaka kura zao, jambo ambalo si kweli, kwani miaka mingi Tanzania imekuwa kitovu cha elimu katika kanda hii huku viongozi wake wengi wakisoma Tanzania.

Sasa kama CCM Imeshindwa si ikae pembeni?
 
Kama Kiwete akiulizwa kwa nini watanzania masikini na hajui kwa nini ndio utegemee nini toka Chama cha Majambazi???
 
Kama yeye hawezi wengine wanaweza hata darasani unaweza shindwa swali mwenzako akalifanya kwa dk moja.
 
Yule kijana Msemakweli yuko wapi amkamate huyu Dr.Kamala na vyeti
vyake ambavyo chuo cha Udokta hakitambuliki?
 
Sure, kama wao wameshindwa wakae kando na sio kulazimisha kuwa eti HAIWEZEKANI. Huo ndio umbumbumbu
 
Yeye ndio mbumbu asiyejua kuwa ili kumaliza malaria ni lazima uondoe hadi mazalia yake! Ndio maana Dr. Slaa anazungumzia kuboresha usafiri wa Reli ili ghalama za usafirishaji zishuke pia. Watatapatapa sana safari hii
 
Rais Mtarajiwa Dr Slaa angekuwa mbumbumbu basi Kikwete asingeukacha mdahalo na kuingia mitini. Utaogopa vipi kufanya mdahalo na mbumbumbu? Raisi wa nchi anapoingia mitini kufanya mdahalo na mbumbumbu ni nani ambaye ni mbumbubu kuliko mwenziye? Huhitaji kwenda shule kujibu hili swali :peace:
 
Si mbumbumbu kwenye uchumi tu, hata katika maisha yake binafsi amejionyesha ni mbumbumbu... Utatembeaje na mke wa mtu bila kujua?
 
Si mbumbumbu kwenye uchumi tu, hata katika maisha yake binafsi amejionyesha ni mbumbumbu... Utatembeaje na mke wa mtu bila kujua?


Bahati yako naogopa ban vinginevyo ungekoma kutembelea JF

JK ndiye mbumbumbu namba moja maana anasema hajui hajui kwa nini Tanzania ni maskini

Kuhusu huyo mke ataishi naye milele mpasuke na roho zenu mbaya za kifisadi
 
Si mbumbumbu kwenye uchumi tu, hata katika maisha yake binafsi amejionyesha ni mbumbumbu... Utatembeaje na mke wa mtu bila kujua?[/QUOTE]

We ndo bado kweli! Kwani wake za watu wanaandikwa usoni 'mke wa mtu' kiasi ambacho ukikutana naye tu basi utaweza kusoma kama kishawekwa ndani? Kama mke wa mtu anakudanganya kwamba hana mume utajua kweli? Kivipi?:peace:
 
Kuhusu mfumo wa kodi katika jumuiya, alisema si kweli kwamba aliuanzisha yeye, kwa kuwa yalianza kabla hajawa waziri na haiwezekani ushuru ufutwe bila kujadiliana na kukubaliana nchi wanachama, hivyo akasema Dk.Slaa hawezi kufuta ushuru huo kwani ni lazima ajadiliane na viongozi wa EAC.

Hapo ndipo Dr. kamala ameonyesha upeo wake ulivyo finyu.................kumbe anaelewa ya kuwa ili kubadilisha sheria za EAC ni majadiliano sasa Dr. Slaa akishatawazwa kuwa Raisi atakwenda huko Arusha na kumwaga sera ambazo akina Kibaki, Museveni na wengineo watamwelewa vyema na kugeuza utumwa ambao CCM ilishiriki kuwafungia watanzania washindwe kuwa na makazi bora kutokana na ushuru wa bei za vifaa vya ujenzi.....
 
Yeye angekuwa na akili si angeaminiwa na wananchi wake kule jimboni? Mbona walimpiga chini pamoja na kuhonga? Atakuwa anawinda kuteuliwa!
 
Si mbumbumbu kwenye uchumi tu, hata katika maisha yake binafsi amejionyesha ni mbumbumbu... Utatembeaje na mke wa mtu bila kujua?
Nisamehe, unaweza kuniita mbumbumbu kwa sababu nilitembea na mai waifu wako bila kujua.
 
Jamani nawashauri msipoteze muda wenu kumjadili Kamala ...... huyo jamaa ni mbumbumbu mno; hata watu wa jimbo la Nkenge wanalifahamu hilo ndiyo maana walimtosa kurudi mjengoni.
 
Si mbumbumbu kwenye uchumi tu, hata katika maisha yake binafsi amejionyesha ni mbumbumbu... Utatembeaje na mke wa mtu bila kujua?

Muulize Mahimbo hilo swali!

Kamala ndio amemshikia Tambwe nini kitengo kwa muda? Anajitahidi kuthibitisha taarifa za msema kweli. Kile kitabu kitabu kilipopelekwa jimboni kwake inawezekana jamaa aliuza hata nyumba ili avinunue vyote. Pole sana ndugu Kamala. labda ni bora ukaanzia chini ili uelewe uchumi. Namuomba Dokta akuteue wala hata afisa mipango wa mtaani kwetu labda from that experience unaweza kujifunza tena uchumi kwa kuwa ulishindwa darasani mpaka ukachakachua.

Naahidi kukupa contacts za walimu wa tuisheni ya uchumi wakusaidie kubrush up.
 
Mh... labda kweli:tape:

Lakini ngoja kwanza... hivi kamala ndiye yule aliyetujaza EAF na mambo ya VAT siye??

Na gharama za simennti ya china vipi?
 
Back
Top Bottom