Dk Slaa: Kwanini sikumsalimia JK

Wasalimiane ili iweje? Salamu zao zinatatua nini Kati ya haya
1. Umeme Juu 40%
2. Inflation Juu 19%-30%
3. Tz ni nchi ya ya Tatu kwa kuongoza kwa umaskini duniani
4. Tz nchi ya 3 kwa kuzisha Madini na ya 3 kwa umaskini duniani
4. Tz nchi ya mwisho kwa miundo mbinu ya Barabara kwa nchi za East Africa
5. Maisha ya mtanzania wa kawaida ni utata mtupu.....
6....
7....
8....

Unaweza ongeza orodha hiii...

Haya ndio mambo ya msingi ya kuzungumza na Sio kusalimiana kwenye misiba.... Period
 
Huu ni udaku, kabla ya kutoa toleo lao la jana la "Mwananchi-udaku" walipaswa kumtafuta Dr Slaa ili kupata upande wa pili wa story. Wajinga hawa wanamtafuta saa 24 baadaye ili "wauze" toleo jingine la gazeti lao la "udaku". Hovyo kabisa!
 
Mode, hamishia habari hii kule Chit chat na baadae Hoja Mchanganyiko. Habari hii haistahili Jukwaa la Siasa!. Hizi double standards zitatufikisha pabaya!.

Sio kwasababu inamaana moja na yakwako ndo iende Chitchat angalia aina ya uandishi mbona umekaa kidaku kama gazeTi lenu la mwananchi???????
 
kwanini dr. Slaa tu, inamaana pale msibani walikuwa wawili tu Slaa na Rais pekee? mbona hawakuandikwa na hao wengine au alisalimiana nao wote isipokuwa yeye tu!?.
 
Jamani jamani jamani!!!!! SHAME ON YOU JF MEMBERS!!!
Mmekosa mambo ya kujadili jukwaani!!? Yaani sasa Jf imekuwa sehemu ya udaku? Mmekalia kuangalia nani atamsalimia mwingine? Duh!! GT ya Jf inafifia taratibu!!
Lawama zinakuja kwa wana Jf kwasababu kuna topic zaidi ya 5 zote ni udaku tu na zina page zaidi ya 7!! Hii ni aibu kwa Gt kujadili udaku!!!
Li nchi linaenda kombo hatujadili, tumekalia umbea tu!!
MODS NAOMBA U- MGAMBO NIANZE KUCHARAZA WATU VIRUNGU HUMU NDANI!!
 
Mazishi ya KITAIFA yalifanyika Karimjee. JMK akatimkia Morogoro. Tusubiri Jumamosi kwa msiba wa Sumari hapohapo Karimjee.
 
hivi ni lazima kusalimiana?? mbona sioni sehemu ikisema JK hakumsalimia Slaa??

Upuuzi wa Mtanzania wa leo, inflation juu, sie tuko bize kuangalia nani kamsalimia nani

Mkuu naungana na wewe kabisa,ili suala maelezo yake yamejitosheleza lakini bado kuna watu wanauliza maswali yenye majibu tayari!dah Mungu atuokoe waTanzania na hv vichwa vyetu!ukileta uzi juu ya mfumuko wa bei,gharama za maisha,mporomoko wa uchumi hapa wachangiaji watakua wachache sana,vitu vinavyoathiri maisha yetu moja kwa moja havina maana kwetu,ila vya kijinga ndio washadadiaji wakuu,nani katuloga au kutulaani Watanzania?
 
teh teh teh kumbe anamtambua kama JK rais
SOURCE MWANANCHI GAZETI
KATIBU Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa amesema kuwa, hakuweza kusalimiana na Rais Jakaya Kikwete kutokana na Jiografia ya eneo la makaburini lilivyopangwa na watu wa usalama wa taifa pamoja na kamati ya mazishi kutomruhusu kufanya hivyo.

Hata hivyo Dk Slaa alisisitiza kuwa, kwa upande wake, kwenye msiba siyo sehemu ya kwenda kwa ajili ya kusalimiana na watu ama kurekebisha mambo yaliyoharibika bali ni sehemu ya kumwombea marehemu.

"Siyo hulka ya Dk Slaa kutumia misiba kama sehemu ya kusalimiana, wala kutengeza mambo yaliyoharibika, mimi huwa naenda kwenye msiba kwa lengo moja tu la kumwombea marehemu, huwa simtazami hata mtu aliyekaa pembeni yangu," alisema Dk Slaa alipozungumza kwa njia ya simu jana.

Alifafanua kuwa, katika eneo la makaburi kulikuwa na mabanda matano ambayo yalipangwa kwa ajili ya Askofu, Rais, Viongozi wa vyama vya siasa, mwili wa marehemu na familia na banda jingine lilikuwa la watu wengine waliohudhuria mazishi hayo. "Sasa kutoka alipokuwa amekaa Rais mpaka kwenye banda nilipokuwa mimi, kulikuwa na umbali wa karibu mita 20, sasa mlitaka nikimbie kumsalimia Rais nivunje protokali kisha nikamatwe na usalama wa taifa," alisema Dk Slaa. Alisema alikuwa mtu wa kwanza kufika makaburini kwa lengo la kuangalia jinsi kaburi la mbunge wa chama chake lilivyochimbwa kisha akaonyeshwa sehemu ya kukaa na watu wa usalama wa taifa.

Alisema kuwa, hata katika wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Regia Mtema, katika ukumbi wa Karejee, kulikuwa na utaratibu kama huo ambapo ilitengwa sehemu ya kukaa Makamu wa Rais, Spika wa Bunge, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani na Makamu wake na yeye Dk Slaa akawekewa sehemu yake kama Katibu wa Chama alichokuwa akikitumika marehemu.

"Mimi sipendi kuweka siasa kwenye mambo kama ya msiba, Dk Slaa siyo kichaa siyo kichaa aanze kukimbia kumsalimia Rais. Katika sehemu kama ile Rais huwa anakuja baada ya watu wote wakiwa wameshakaa, yeye ndiye hupita na kuanza kusalimia watu na hamjaona hata sehemu moja aliponyoosha mkono kunisalimia nikamkwepa," alisema Dk Slaa:

"Msiba siyo mahali pa kutengeza urafiki, au kutengeza mambo yaliyo haribika, pale ni ibada tu na kumuombea marehemu siyo sehemu ya kufanya siasa" alisisitiza Dk Slaa. Jana baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa, Dk Slaa alishindwa kusalimiana na Rais Jakaya Kikwete katika mazishi ya Regia Mtema yaliyofanyika kijijini kwao Ipangalala Morogoro juzi.Regia alifariki dunia Januari 14 kwa ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Ruvu mkoani Pwani.
MY TAKE
: Mwananchi ni gazeti la udaku kwani jana kabla ya kuandika habari ya Dr. Slaa kumuepa kikwete ilishindwa kumuuliza Dr mwenyewe ili athibitishe madai hayo? Tuache kuandika habari za bila utafiti, huu nao si uchochezi? usilazimishe kuandika habari za uchochezi ili tu gazeti lako liuzwe
 
Mhariri wa Mwananchi aitwae Dennis Msaki ni swahiba mkubwa wa Zitto Kabwe so udaku kama huu si ajabu kuandikwa na Mwananchi
 
Kinachonifurahisha ni kuwa kila anayeikurupukia hii habari ya "kusalimiana" anaishia kujichanganya na kujikanganya!
Alianza Pasco wa Jf hapa bodini na kuunganisha dot ambazo mwishoni zilitokea Chit-chat,
leo Mwananchi wanatapatapa....
 
Mode, hamishia habari hii kule Chit chat na baadae Hoja Mchanganyiko. Habari hii haistahili Jukwaa la Siasa!. Hizi double standards zitatufikisha pabaya!.

Kaka bado unayo tu?
Ah tusifike huko bana, ngoja kwanza na hii isogezesogeze page kama ile yako afu tutaitupia panapobidi.
 
Magazeti wakiishiwa mambo ya kuandika ndipo huzua upupu na kuupulizia perfume ili angalau mikono yao iende vinywani mwao. Kusalimia msibani ni habari kweli? Sikumbuki kama hata mimi nikienda msibani nasalimia kila mtu. Hata aliyeandika habari hiyo hafanyi hivyo. Ametumwa kuandika ili kuchafua mtu, sababu wamekosa kitu cha kumchomekea Slaa kwa sasa na bado wanakitafuta.
 
Hii protokali ya hapa nayo ni kizungumkuti, iweje ZK, naibu katibu mkuu akae kwenye zulia halafu WS, Katibu Mkuu akae nje ya zulia, besides kushoto ya ZK kulikua na kiti ambacho kilionekana kuwa wazi ikimaanisha kabisa kwamba kilikua kimetengewa Mh WS.........!!!??? anachotuaminisha WS ni kwamba usalama walichakachua haki yake???

ile ilikuwa ni shughuri ya bunge, ZK ni naibu kiongozi wa kambi ya upinzani, Dr Slaa si mbunge, ingekuwa inaratibiwa na chama, sawa, wangekuwa na utararibu tofauti na huo
 
Zitto ni mbunge na aliyefariki ni mbunge hivyo alipangwa kukaa banda la bunge na spika,naibu na mbowe ambao wote ni wabunge pia.....Dr sio mbunge...fuatilia maelezo ya Dr vizuri....hicho kiti kitupu pembeni ya Zitto kiko wapi?

attachment.php

Kiti wazi hakipo pembeni ya ZK, naona kiko pembeni ya Ndugai - MAGAMBA KAMA KAWAIDA YAO WAO NI KULALA KILA SEHEMU - Shame on them!
 
Jana nilileta thread hapa JF nikilalamikia story yao ya jana kuwa ilikuwa ni ya udaku mtupu! Kwa mara nyingine narudia tena kuwa CREDIBILITY YA GAZETI LA MWANANCHI IMESHUKA KWA KIWANGOI CHA JUU SANA!
 
Salamu ya Jk kwa Dr Slaa haisaidii tanzania kwa lolote. JK aliiba kura kashinda kwa dhambi na dhuluma hakuna haja ya kumsalimia dhulumati. Unafiki ndio unaotumaliza Watanzania, tuwachukie wezi na wahujumu kwa vitendo ili tuendelee waache njia zao mbaya. Hata maandiko yameandika wenye dhambi kwao ni jehanamu Mungu hawapendi.

Kwa nini umsalimie mnafiki ambaye anatamani ufe? anakuombea mauti anatamani ufungwe anatamani uwe na kesi za uzushi kila asubuhi???? ni unafiki tu ndio utakufanya ukenua .

Salamu haitufanyi tuwe na amani wala tupate ujira bora. Salamu haikoi madini yetu. Salamu haiwezi kutuwashia umeme, Salamu haiwezi kutuletea katiba mpya bora. Tunahitaji ukweli na matendo ya haki.
 
Back
Top Bottom