DK SLAA ASEMA "Pinda, kwa siku moja akiwa kule bungeni hupata posho ya Sh200,000 ambayo inazidi mshahara wa mwezi mmoja wa mwalimu, hata polisi anayelinda usalama wenu,
Dk Slaa aliyekuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka jana alisema, inasikitisha kuona Mbunge wa Katavi anakuwa mbinafsi kwa kujiwekea umeme wa jua kwenye nyumba yake pekee katika Kijiji cha Usevya badala ya kuupeleka kwa wananchi wote.
source mwananchi.
lakini huyuhuyu dk slaa anayesema pinda hupata posho ya sh 200,000 kwa siku mbona yeye hajapinga chama chake kumlipa marupurupu na mshahara anaolipwa mbunge ambao yy mwenyewe alisema ni milioni 7. kwa ufupi dk ni muongeaji mzuri na mhamasishaji mzuri wa wananchi lkn katika vitendo ni ZIRO kabisa, yy kila siku hulia kuwa posho wanazolipwa wabunge ni kubwa leo posho anayolipwa waziri mkuu ni kubwa sasa mbona yy haonyeshi mfano kwa kukataa marupurupu ambayo chadema wameamua kumlipa, aseme tu msinilipe hizi hela ni bora tuwasomeshee yatima ktk majibo yetu, tena kwa hivyo itakuwa kakisaidia sana chadema.
Tofautisha basi,mshahara na marupurupu.M7 za Dr slaa ni mshahara,200,000 ya pinda ni marupurupu,kwa siku.Piga hesabu zako pinda anapata Marupurupu sh ngapi kwa mwezi? + mshahara.Marupurupu tu ya pinda yanazidi mshahara wa DR Slaa.Sasa kwanini point ya DR isiwe na mashiko.