Elections 2010 Dk. Slaa asigombee Urais 2010

Fareed

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
328
135
Kumekuwa na mjadala mpana kuhusu Dk. Wilbrod Slaa, Mbunge wa Karatu na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kugombea Urais mwaka huu ili apambane na Kikwete wa CCM.

Kwa maoni yangu, Slaa akigombea Urais inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa sana nguvu ya upinzani hapa Tanzania. Hii ni kwa sababu kuwa akigombea Urais ni dhahiri kuwa atashindwa na JK kwa sababu kadhaa, ikiwemo fitna za siasa, nguvu kubwa za kifedha ilicho nacho chama tawala, na ukweli kuwa bado Watanzania wengi wako kwenye giza nene na wanaendelea kukipigia kura CCM licha ya kushindwa kuleta maendeleo hapa nchini kwa miaka 40 sasa. It is a foregone conclusion that JK atakuwa re-elected kuwa Rais hivyo ni bora tujiandae kisaikolojia kuendelea na huu mzigo wetu for the next 5 years.

Slaa akigombea Urais ina maana kuwa he will relinquish (ataliachia) jimbo lake la Ubunge la Karatu na hivyo kutoswa nje ya mainstream politics unless Chadema impe Ubunge wa kiti maalumu au asubiri pengine kama by-election itatokea mahali. Siasa za Tanzania zipo ndani ya Bunge kwani macho ya wananchi wote yapo huko. Tukimtoa Slaa Bungeni kwenda kupambana in a losing battle maana yake kuwa tuna uwa nguvu ya upinzani Tanzania. Slaa ndiye mhimili mkuu wa upinzani hapa Tanzania na bado taifa linamhitaji awashe moto Bungeni dhidi ya ufisadi.

Bado tunamhitaji Slaa aikabe koo serikali kuhusu rushwa ya rada, Richmond, EPA, Tangold, Meremeta, DeepGreen, Mwananchi Gold, Kiwira, TICTS, TRL na ufisadi mwingine lukuki. Kwa maoni yangu, Slaa abaki bungeni ili kujiimarisha kugombea Urais 2015 ambapo ndiyo kuna nafasi realistic ya upinzani kushinda.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amegundua kuwa alifanya kosa kutoka Bungeni kwani umaarufu wake umeshuka kutokana na kuwa nje ya uwanja wa mapambano. Pengine hii ndiyo maana hana mzuka wa kugombea Urais mwaka huu na anaelekea kutaka kugombea Ubunge.

It's time to face the hard truth, Slaa akigombea Urais atapunguza tu margin of victory ya JK. Mbaya zaidi atakuwa amepoteza kiti chake cha Ubunge na kuenguliwa kwenye national politics wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi mama wa 2015 (the mother of all general elections). Think about it...

OMBI KWA WANA JF:
Wilbrod Slaa abaki Bungeni. The nation desperately needs him. Imagine Bunge la Tanzania bila Slaa. It will be a political nightmare!
 
Naona tusimpe JK green light kuwa lazima ashinde uchaguzi wa October. Kwa madudu anayofanya watz wengi wameelewa upungufu wake na akipata mpinzani strong anaweza kuanguka. Ushindi wa Kikwete upo mikononi mwa wapiga kura na wakiamua hatarudi.

Kama Dr. Slaa anataka kugombea mwacheni na tusijaribu kuwakatisha watu tamaa kwamba lazima JK atashinda. Watanzania wamebadilika sio wajinga kiasi hicho.
 
Kwa maoni yangu napingana na wazo la mtoa mada.
Kugombea urais kwa dr slaa sio lazima ashinde msimu huu.
Akishindwa anarekebisha makosa ili akiibuka tena msimu ujao, ushindi unapatikana.
Mwache slaa agombea.
 
Kwa maoni yangu napingana na wazo la mtoa mada.
Kugombea urais kwa dr slaa sio lazima ashinde msimu huu.
Akishindwa anarekebisha makosa ili akiibuka tena msimu ujao, ushindi unapatikana.
Mwache slaa agombea.

Mimi kama walivyo wapenda mageuzi wengi humu JF natamani sana Dk. Slaa agombee Urais ili kumpa JK ushindani halisi na kuweza kujenga zaidi name recognition miongoni mwa wapiga kura.

Hofu yangu kubwa ni kuwa iwapo JK atashinda (na mazingira yaliyopo sasa hawezi mgombea wa upinzani kushinda), basi Dk. Slaa anaweza kutupwa kwenye political wilderness kama ilivyomkuta Freeman Mbowe na kusahaulika. Siasa za Tanzania zinachezwa Bungeni. Kama Chadema watatuhakikishia kuwa iwapo Dk. Slaa atakosa Urais, watampa Ubunge wa kiti maalumu, basi ni vyema sana sana agombee Urais. Ila kama kugombea Urais matokeo yake itakuwa atapoteza Ubunge na Tanzania itakosa uwakilishi wake kwenye Bunge in the nmext 5 years, bora Urais agombee mtu mwingine.


Dk. Slaa is our only hope. Hilo ndiyo linanifanya niwe na hofu juu ya jambo hili. Tuangalie consequences za yeye kugombea Urais pamoja na faida zake. Chadema wakithibitisha kuwa Dk. Slaa atapewa Ubunge wa viti maalum akikosa Urais basi na mimi najiunga rasmi kwenye campaign team ya Dk. Slaa for 2010. otherwise, it would be too big a price kumkosa mpambanaji huyu makini Bungeni katika miaka mitano ijayo.
 
we unapenda upinzani au maendeleo? unafikiri kama mambo mazuri upinzani ungekuwepo? mi nafikiri angegombea ingekuwa safi sana, na angeshinda lazima.
 
Kuna watu wanaopinga hii mada naona wanadhani JF = Watanzania!! La hasha!! Sisi ni wachache mno humu JF!! Tena hatuwezi kusema tunawawakilisha waTanzania!! Labda tuseme tunauwakilishi wa waTanzania wenye kisomo au ufahamu (exposure) fulani lakini la hasha, si waTanzania wote kwa ujumla.

Si jambo linalofurahisha wote, hata mimi sifurahii, lakini ukweli ni kwamba CCM itashinda uchaguzi wa Urais hata kama Kikwete hatapitishwa na hicho chama
 
Kama unafikiri UPINZANI utakuja kufanya mabadiliko Tanzania basi utasubiri sana. Nakubaliana na Mkandara kuwa kwa nchi nyingi za Africa, ni Rais ndiyo anakuwa na kila kitu. Wee waziri Mkuu unakuwa sawa na wale asilimia 70 wafuata upepo tu. Tukitaka kubadili ile nchi dawa yake ni moja tu nayo ni kumpeleka mtu magogoni asiye mwana CCM. Hapo utaona CCM wanavyoanza kulia kubadili katiba ili kupunguza madaraka ya Rais. Kama kuna mwaka rahisi kubadili Rais ni sasa kwani Muungwana kashawaambia Wafanyakazi "Hata kura zenu sitaki...."

Mkuu wangu nakubaliana sana na changamoto zako isipokuwa tu unajaribu kufikiria Kiulaya Ulaya wakati tunazungumzia Tanzania nchi ya dunia ya tatu walioingia Ubepari pasipokuusoma Ubepari matokeo yake kila mmoja wetu kabeba Msalaba wake.
Nitarudia kusema uchaguzi wa nchi zetu hasa zile zinazofuata Popular vote na mfumo ambao mshindi huchukua zote hakuna cha Bunge.. Mugabe kashindwa bungeni, Kashindwa hata Popular vote alichobadilisha ni matokeo ya Popular vote na leo ndiye kiongozi anayepanga mwelekeo wa Zimbabwe. Hakuna cha Morgan wala mjomba wake. Hivyo hivyo Kenya matokeo yake ni yale yale bunge halina nguvu ya kumwangusha Kibaki. Huyo raila yupo yupo tu kubeba miswada bungeni.

Na kibaya zaidi ni kwamba sisi wote akili zetu ni kumchagua rais... uchaguzi wetu is all about the PRESIDAA wengine watajipanga nyuma yake na ndio maana ukitazama Wabunge na Madiwani wa CCM walioshinda wakati wa JK 2005, wengi wao hawana hata elimu wala sifa yoyote ya Uongozi. Watu wameshinda kienyeji enyeji tu.. Yaani Bungenikumejaa uozo kutokana na tiketi ya JK na kama unakumbuka Wabunge wenyewe baada ya ushindi walikiri kwamba ushindi wao umetokana na JK.. JK alipata support kubwa ya chama kutokana na uwezo wake kununulika na sii sifa yake ktk Uongozi.. Mwaka huu mambo yamebadilika na JK mwenyewe ameanza kulikoroga. Jk ameacha miaya mingi ya mashambulizi kiasi kwamba haitakuwa kazi kubwa sana kumtwanga magoli.. Na zaidi ya hapo safari hii ni lazima JK apande kizimbani kujitangaza.. akiingia mitini tunapata tena sababu nyingine ya kumshindilia. Nafasi ya Urais iko wazi kuliko mnavyofikiria.. kinachotakiwa ni vyama vya Upinzani wasijichuuze na kuanza kufikiria kila mmoja waoanaweza kushinda..Hofu yangu kubwa ni CCJ ambao binafsi nafikiri ni pandikizi la CCM kupotosha watu haswa wakati issue ya Richmond ilipokataliwa Bungeni. Kwa kuhofia kelel za wananchi ikazaliwa CCJ kutupotosha akili zetu ktk kufikiria maanake sote tunasubiri mwokozi. Nasubiri tu kuona wamejoipanga vipi nyuma ya vyama vya Upinzani laa sivyo hiki ni chama kilichopandikizwa kutuzuga kwamba wana uchungu sana na serikali hali ni baadhi ya watu ambao hawana uhakika na ushindi wao ndani ya CCM.
 
Ni jambo lililo wazi kabisa kwamba Dr.Slaa anaweza kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015.Kinachotakiwa sasa hivi ni CHADEMA kuhakikisha kuwa wanaweka au TUNAWEKA wagombea wanaokubalika katika nafasi zote za ubunge.

Pia Slaa aendeleze nguvu zake bungeni na kuweka mikakati mizito kipindi hiki 2010-2015. Pamoja na umaarufu wa CHADEMA wa sasa,bdo tunahitaji pyramid-like structure katika kujiandaa kukabiliana Vilivyo na CCM mwaka 2015.ni lazima tuahkikishe tunajikita vijijini kwa nguvu zote na kutoa alternative solution kwa matataizo yanayotokana na uongozi wa kata hadi ngazi za mitaa.CHADEMA ihakikishe kuwa viongozi hata kama ni wa mtaa,wana uwezo au wawezeshwe kuonyesha tofauti na wananchi waone ni kwa nini CHADEMA ni mbadala.

Kwa BAVICHA.Hili ni Baraza la vijana la CHADEMA,ni sawa na UVCCM...simaanishi kimtazamo au kitabia,kimaadili nk.Hili ni Baraza ambalo kwa kweli kama CHADEMA tukiweka mikakati,hili baraza litasaaidia kuunganisha vijana wote Tanzania na linaweza kuwa powerfull sana ktk kujenga ushawishi kwa vijana.Hili ni baraza ambalo linatakiwa kujitangaza na kujitandaza nchi nzima.Asilimia zaidi ya 65% ya population ya Tanzania ni vijana.Kwa hiyo kama tunataka kujenga ushawishi ni lazima tuwe karibu na vijana na tujenge mtandao,tuhakikishe tunawashawishi kujiandikisha na kupiga kura.Vijana walio na miaka 15-17 saba mwaka huu ni wengi,hao watakuwa wapiga kura wa mwaka 2015.

Pia BAVICHA ni lazima ijitahidi kutumia mbinu kali na kuhakikisha wanajitahidi kuingiza puppet governments ktk vyuo vikuu vyote vya umma ambao watakua wana-pose kama watu ambao wako above partisan politics.viongozi wa hizo serikali ni lazima wawe na ushawishi mkubwa kwa wanafunzi

Pia BAVICHA lazima waanzishe kitengo au idara maalumu ya kushughulikia ajend za wamachinga,vijana jobless nk ili kujenga matumaini na kutafuta uungwaji mkono.Zaidi ya yote,BAVICHA ihakikishe inajitafutia vyanzo vya mapato na vitega uchumi ,raslimali ambazo zitazidi kuwapa nguvu ya kupambana na UVCCM

Pia,Wabunge wa CHADEMA wajitahidi bungeni,wajenge hoja zaenye mshiko na kusaidiana kutafuta resources kwa ajili ya uwekezaji majimboni mwao.

Mwaka 2015,CCM kutakua na jnga kubwa la uongozi na hasa kuanzia mpasuko utokanao na uchaguzi huu hadi 2015,kuna kazi.Lazima tujitahidi kuvuna katika huu msiba.Sina huruma nao hata kidogo.

Pia,kama CCJ watapata usajili wa kudumu,basi CHADEMA iangalie jinsi ya kufanya nao strategic alliance pamoja na CUF.Nina uhakika ikifika mwaka 2015,Dr.Slaa au mgombea wa CHADEMA akisimama huku run mate wake akiwa mtu wa CCJ au CUF vs mgombea wa CCM,basi upinzani utaingia madarakani.

Sasa hivi viti vingi vitakavyopatikana bungeni vitasaidia kuanzisha vuguvugu la kudai Katiba mpya.Msukumo wa hii movement utaleta radical Reform.Nje ya bunge CHADEMA itumie wanaharakati,wanahabari,na powerfull department BAVICHA kudai haki kwa kutumia new approach kama maandamano ya amani na migomo mizito yenye misimamo bila kujali vitisho.Bado nitaendelea
 
...

Hofu yangu kubwa ni kuwa iwapo JK atashinda (na mazingira yaliyopo sasa hawezi mgombea wa upinzani kushinda), basi Dk. Slaa anaweza kutupwa kwenye political wilderness kama ilivyomkuta Freeman Mbowe na kusahaulika. Siasa za Tanzania zinachezwa Bungeni. ......

Acha uongo wewe, Mbowe hajasaulika!
 
OMBI KWA WANA JF: Wilbrod Slaa abaki Bungeni. The nation desperately needs him. Imagine Bunge la Tanzania bila Slaa. It will be a political nightmare!

Kama Taifa linamhitaji basi na tumfanye agombee ili awe rais wa nchi nzima. Wasiwasi wangu wewe unaonekana kama unamuendorse JK vile. Kwa sababu kama Slaa atagombea basi ataongeza idadi ya kura na hivyo kuongeza idadi ya wabunge wa viti maalum katika kambi ya upinzani ambao wametoa mchango mkubwa katika bunge hili linaloisha.
 
Mimi kama walivyo wapenda mageuzi wengi humu JF natamani sana Dk. Slaa agombee Urais ili kumpa JK ushindani halisi na kuweza kujenga zaidi name recognition miongoni mwa wapiga kura.

"Hofu yangu kubwa ni kuwa iwapo JK atashinda (na mazingira yaliyopo sasa hawezi mgombea wa upinzani kushinda), basi Dk. Slaa anaweza kutupwa kwenye political wilderness kama ilivyomkuta Freeman Mbowe na kusahaulika. Siasa za Tanzania zinachezwa Bungeni.
Kama Chadema watatuhakikishia kuwa iwapo Dk. Slaa atakosa Urais, watampa Ubunge wa kiti maalumu, basi ni vyema sana sana agombee Urais. Ila kama kugombea Urais matokeo yake itakuwa atapoteza Ubunge na Tanzania itakosa uwakilishi wake kwenye Bunge in the nmext 5 years, bora Urais agombee mtu mwingine.

Dk. Slaa is our only hope. Hilo ndiyo linanifanya niwe na hofu juu ya jambo hili. Tuangalie consequences za yeye kugombea Urais pamoja na faida zake. Chadema wakithibitisha kuwa Dk. Slaa atapewa Ubunge wa viti maalum akikosa Urais basi na mimi najiunga rasmi kwenye campaign team ya Dk. Slaa for 2010. otherwise, it would be too big a price kumkosa mpambanaji huyu makini Bungeni katika miaka mitano ijayo."

Fareed, hayo mawazo yako nawasihi sana viongozi wa Chadema wayafanyie kazi (ikwa ni pamoja na Dr. Slaa mwenyewe kukubali kugombea Urais mwaka huu).Kukubali kushindwa kirahisi kwenye urais na JK, ni kumpa pumzi ili aje na nguvu mpya ya kupandikiza anayemtaka mwaka 2015. Dawa ni kukumbana naye mwaka huuna ''kumjeruhi'' ili 2015 tunamalizia kwa ushindi. Kumbuka kwa Dr. Slaa kugombea mwaka huu jina lake litasikika na kujijenga zaidi vijijini na 2015 atakuwa hana kazi kubwa! Chadema msifanye makosa ya kumwachi mtu kufunga kirahisi eti ukisubiri utarudisha. YES, Dr. SLAA FOR PRESIDENCY 2010 & 2015!
 
Hakujawahi tokea wakati nikaamini kuwa CCM inaweza kushindwa. Lakini kipindi hiki ninaamini kwa sehemu kubwa CHADEMA ikipata candidate mzuri itafanya biashara tamu ya kwenda ikulu na kujaza wabunge mjengoni. Iacheni CCM iendelee kujiamini kupita kiasi. Itashangaa wanaume wakiapishwa. Mwacheni Dr. Slaa aende zake Ikulu. Panamfaa na nchi inahitaji mzalendo mfuatiliaji na msimamiaji asiyechoka mwenye afya nzuri

Fareed nakubaliana kabisa na tahadhari yako. Lakini nawashauri mpunguzi woga kidogo makamanda wangu.
 
Hakujawahi tokea wakati nikaamini kuwa CCM inaweza kushindwa. Lakini kipindi hiki ninaamini kwa sehemu kubwa CHADEMA ikipata candidate mzuri itafanya biashara tamu ya kwenda ikulu na kujaza wabunge mjengoni. Iacheni CCM iendelee kujiamini kupita kiasi. Itashangaa wanaume wakiapishwa. Mwacheni Dr. Slaa aende zake Ikulu. Panamfaa na nchi inahitaji mzalendo mfuatiliaji na msimamiaji asiyechoka mwenye afya nzuri

Fareed nakubaliana kabisa na tahadhari yako. Lakini nawashauri mpunguzi woga kidogo makamanda wangu.

Ni ukweli mtupu wakati na mazingira tuliyonayo yanaruhusu kabisa CCM kushindwa katika uchaguzi. Hamna sababu ya kumzuia Dr Slaa kugombea kama ataamua kugombea tena tumuunge mkono.

Ukweli ni kwamba watu wengi wanatamani Dr agombea ili wapate mtu wa kumpa kura zao. Watanzania wamechoka na kiburi cha CCM. JK hataki kura za wafanyakazi, wanaojaribu kumzuia Dr watuambie kura zetu wafanyakzi tumpe nani? JK ? maisha wafanyakazi hatukotayari kumpa mtu anayetukana.

Ombi letu wafanyakazi kwa Dr Slaa, tunaomba ajitokeze kugombea tuko naye katika vita hii ya kuiondoa nchi hii katika aibu. Tumechoka sana.

Wafanyakazi tumeshaanza kuhamasishana kuleta mabadiliko katika nchi hii, mwaka ndio mahali pa kuanzia
 
....Mtazamo wangu baada ya kutafakari hali inavyokwenda nchini, ninaona ili upinzani washinde mwaka huu, wakubali kuungana kwa kupendekeza chama kimoja kitoe Rais na kingine Waziri Mkuu (sijui kama kikatiba au taratibu zingine zinaruhusu hilo). Mfano, Lipumba ametangaza kugombea Urais, basi vyama vingine vimsaidie ashinde kwa makubaliano ya kupewa madaraka ya Uwaziri Mkuu, hivyo ataongoza shughuli za Bunge. Na watangaze mapema ili watu wajue na waanze mikakati ya ushindi. Sehemu nyingi, inaonesha ili wapinzani kushinda wanahitaji kuwa wamoja! Ninawasilisha
 
Dr.Slaa ana kila kitu cha kumushinda JK, kinachotakiwa ni kambi ya upinzani kukubaliana kusimamisha mgombea mmoja badala ya kila chama kuweka mgombea, na matokeo yake kuzigawa kura. Pia ni wajibu wa kila mpenda usitawi wa taifa letu awe mwalimu wa kuwaelimisha wapiga kura, kwamba sasa si wakati wa kuirudisha madarakani serikali dhalimu ya CCM.
 
Mimi nachoona ndugu zangu wanaJF ni kuwa Prof Lipumba amegombea mara nyingi sana, Dr Slaa kugombea uraisi siogopi kitu acha agombee ila running mate wake awe Prof Lipumba sasa sijui kama Prof atakubali. Vile Vile tusiogope jamani! kundi kubwa la wasomi tayari tunalo niletu limeshakashfiwa na JK (wafanyakazi) hawa ndo wakutupeleka madarakani tena ndo hao wakutupa mikakati mbadala jinsi ya kung'oa CCM 2010.

Naona 2010 election kuna neema tupu, tusiogope acha Dr agombee uraisi hata akikosa kuna wapambanaji wengine kama Lisu watakuwemo mjengoni hakuna shaka watatusaidia sana.
 
Back
Top Bottom