Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,892
- 31,081
Send tonday, 10 October 2010 08:32 0diggsdigg
Dk Willibrod Slaa
Joyce Mmasi, Uvinza
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema Dk Willibrod Slaa jana alikumbana na wakati mgumu pale alipoelezwa waziwazi kuwa hawawezi kumchagua mgombea ubunge aliyesimamishwa na chama hicho Jimbo la Kigoma Kusini, badala yake watampa kura David Kafulika wa NCCR Mageuzi.
Kafulila aliyefukuzwa kazi makao makuu ya chadema na kuamua kukihama na kujiunga na NCCR-Mageuzi mapema mwaka huu, anagombea ubunge katika Jimbo la Kigoma Kusini.
Wananchi hao wa Uvinza, walisema hawatamchagua mgombea ubunge wa Chadema, Asanali Muslim badala yake watampa Kafulila wa NCCR Mageuzi wakati wanamfukuza (Chadema) Dk Slaa alisema ni hawezi kushindana naye kwa ni mdogo kwa cheo huku akimfananisha na sisimizi.
Wakazi hao walimwambia Dk Slaa kuwa chaguo lao la ubunge ni Kafulila wa NCCR Mageuzi ingawa kura zao za urais watampa yeye.
Wananchi hao walipiga kelele za kumkataa mgombea wa Chadema alipoitwa jukwaani na Dk Slaa ili atambulishwe kwa wapiga kura.
Dk Slaa alipowauliza wananchi kama watamchagua Muslim walijibu kwa sauti kubwa wakisema: "Tunamtaka Kafulila aliyewahi kuwa Afisa uhusiano wa Chadema kabla ya kuhamia NCCR-Mageuzi".
Baadaye Dk Slaa alianza kunadi sera zake na kuwataka watu watakaompigia kura yeye kuwa rais wanyooshe mikono na wote walinyoosha.
Naona hapa kura ya urais zipo. Lakini huku (akimpigapiga bega Muslim) hakuna. Hapa Muslim unatakiwa urudi mara kumi, alisema Dk Slaa.
Wakati akijiengua kutoka Chadema, Kafulila alizua mvutano ndani ya chama hicho huku Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe, akijitokeza hadharani kumuunga mkono.
Dk Slaa jana alizungumzia suala hilo akisema"Nasikia Kafulila anapita huko mitaani akitamba kuwa anaungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wetu, Zitto Kabwe. Nitamleta hapa kwenu (Zitto) aje athibitishe kama madai haya ya Kafulila ni ya kweli, alisema Dk Slaa.
Hii ni mara ya pili kwa Dk Slaa kukubalika na wananchi lakini wabunge wake kukataliwa mbele yake.
Mara ya kwanza ilikuwa katika jimbo la Kyela mkoani Mbeya ambako Dk Slaa alilazimika kumnadi mgombea wa CCM, Dk Harrison Mwakyembe badala ya mgombea wa Chadema ambaye pia alikuwa anamnadi Mwakyembe.
Akihutubia katika mkutano huo jana, Dk Slaa aliwaahidi wakazi mji wa Uvinza kuwa akifanikiwa kuingia madarakani, atashughulikia mgogoro wa muda mrefu kuhusu mafao na haki za waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha chumvi Uvinza waliopunguzwa baada ya kiwanda hicho kubinafsishwa.
Aligusia pia uharibifu wa mazingira unaosababishwa na kiwanda hicho kutumia nishati ya kuni katika uendeshaji wake na kuahidi kuhamasisha matumizi ya makaa ya mawe.Dk Slaa anayeendelea na mikutano ya kampeni mkoani Kigoma, pia aliahidi kuhakikisha mkoa huo unapata umeme wa uhakika utakaounganishwa na Gridi ya Taifa.
Awali mgombea Ubunge jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe alisema kuwa ujanja na mbwebwe alizokuwa nazo Bungeni, zilitokana na Dk Slaa na kwamba ndiye aliyekuwa mwalimu wake.
"Ujanja na mbwembwe zangu Bungeni nilizipata kupitia mwalimu wangu Dk Slaa,'' alisema Zitto na kuongeza; "Katika majimbo kumi yaliyopo mkoani Kigoma, ninaomba wapinzani
Wakati huo huo, Elias Msuya na Jackline Laizer
wanaripoti kuwa, Chadema kinadai kwamba kimebaini wapigakura hewa milioni tatu walioandaliwa kwa ajili ya kuibeba CCM.
Kauli hiyo ilitolewa jana na meneja wa kampeni za Chadema, Profesa Mwesiga Baregu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, hii inatokana na ukweli kuwa idadi ya wapiga kura iliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), hivi karibuni, hailingani na idadi halisi ya Watanzania ambayo sasa inafikia milioni 40.6.
Hii ni kauli ya kwanza kutolewa na chama cha siasa tangu Nec itangaze siku tano zilizopita, kuwa watu wenye sifa ya kupiga kura waliomo kwenye daftari la wapiga kura, ni 19.6 milioni.
Kwa mujibu wa Nec watu hao watatakiwa kupiga kura katika vituo 52,000 vilivyowekwa nchi nzima kwa ajili ya uchaguzi wa madiwani, wabunge na rais.
"Idadi kamili ya Watanzania ni 40.6 milioni, kati yao walio na umri chini ya miaka 15 ni asilimia 44.4 sawa na watu 18.1 milioni huku walio chini ya umri wa miaka 18 wakiwa zaidi ya milioni moja. Hivyo waliobaki ndiyo wana umri zaidi ya miaka 18. Lakini kuna watu milioni tatu ambao wamechomekwa na Nec kupiga kura," alidai Profesa Baregu.
Kwa mujibu wa Profesa Baregu, hata wale wenye sifa ya kujiandikisha kupiga kura kuna uwezekano kuwa asilimia 10 hawakujiandikisha kabisa. Kama ni hivyo alisema, idadi sahihi ya wanaotakiwa kupiga kura ni watu 16.6 milioni siyo 19.6 milioni.
Profesa Baregu alieleza kuwa kutokana na utata huo Chadema itapeleka malalamiko yake kwenye mkutano wa Tume ya Taifa ya uchaguzi na vyama vya siasa uliopangwa kufanyika kesho.
Lakini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji Lewis Makame alipinga madai hayo akisema sio ya kweli.
Jaji Makame alilieleza gazeti hili jana kuwa idadi ya watu inayotumiwa kwa sasa inatokana na sensa iliyofanyika mwaka 2002 hivyo kwa muda wote huo kuna watu walioongezeka.
Kwani sensa inayotumika kwa sasa ni ipi? Sasa tangu mwaka 2002 hapo kati kati watu si wameongezeka? Mtu yoyote anayejua kuwa ametimiza masharti ameandikishwa, alisema Jaji Makame.
Jaji Makame amewataka watu wenye shaka na takwimu hizo waende ofisini kwake kuthibitisha kwenye daftari la Tume la Wapigakura badala ya kulalamika mitaani.
Naye Moses Mashalla anaripoti kutoka Arusha kuwa, Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei ameponda matokeo ya utafiti wa Redet yanaoonyesha kuwa mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete anaongoza kwenye kura za maoni.
Mtei aliwataka Watanzania kuu upuuze utafiti huo kwa kuwa una lengo la kuwashtua na kuwakatisha tamaa.
Mtei alisisitiza kuwa matokeo ya utafiti huo yalikuwa hayana dira bali yalilenga kuwakatisha tamaa watu wanaojipanga kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya uongozi nchini.
Source mwananchi.
My Take
Nakumbuka Zitto alimpigania sana Kafulila yamkini alijua atakuja kuwa mbunge mtarajiwa