Dk. Slaa apata ajali avunjika mkono mwanza

Status
Not open for further replies.
Oooh, pole mpiganaji! Naamini kuanguka huku hakutakuwa na mkono wa mtu. Ila tahadhari ichukuliwe vilevile, maana sipati picha hilo bafu ambalo Rais mtarajiwa alikuwa analitumia lilikuwa ni la namna gani hadi liwe na utelezi uliosababisha aanguke. Lets not just say its normal rather, we need a critical analysis. Ama wenye hotel walifanya mtego au kuna uzembe umefanyika katika kulifanyia usafi hilo bafu kiasi cha kusababisha utelezi. Au kuna jambo lingine zaidi lililojificha...
 
Labda kuna mkono wa mtu.... maana moto mkali anaousambaza unaweza kuwakasirisha wengi.
 
hotel ambazo hazina viwango/ukaguzi wa idara ya afya kazini (OH&S) Occupational Health and safety. Risks are not controled in most of the hotels in Tanzania.

Na lazima bafuni kuna zile tiles za kuteleza 'kung'a" badala ya kuwekwa zenye 'rafu' ugumu fulani hive ili kama zinapata unyevunyevu zisiteleze kirahisi.
Dr anaweza kuwashtaki na kujichotea hela za ajabu.

Nenda Mheshimiwa Slaa. NEnda baba!

Ata Kikwete ugonjwa wake wa kupotezapoteza nguvu ghafla bin vuu ungemtokea akiwa hotelini zingesingiziwa tiles...Tafakari!!!
 
Maombi wapwa si mnakumbuka yule wakala wa ibilisi (pweza mtu) alivyotabiri? In spiritual world kina effect kubwa but thank's to Jesus cause He died for us and for His precious blood we are protected from the evil
 
Hii habari imetushitua sana natumaini ni ajari ya kawaida. Pole sana DR. Slaa,mpiganaji tunakuombea upone haraka, Safari ni ndefu, tunakuomba sana sana usikate tamaa!! Maana huku njiani kuna milima na mabonde. Wanachi Wanyonge na wa kawaida tuko nyuma yako!! Mungu akuponyeshe, akulinde baba na kukuongoza kila uendako! Get well soo!!
 
jamani hakuvunjika mkono ameteguka tu. Bora yuko safi na mapambano kama kawa yaendelea!
 
Kwa sisi tulio na uzalendo na nchi yetu, tunapenda wagombea wote waanze shughuli salama na wamalize kwa amani. Sasa hii taarifa kuhusu kuumia Dr Slaa, mwenye taarifa kamili basi atujulishe. Hii habari mara kapata ajali, mara kadondoka bafuni inatuchanganya. Mwenye taarifa za uhakika atujulishe. hii hali kama ni hivyo, inanikumbusha mwaka ule Mh Mwai Kibaki alipoumia mguu wakati wa kampeni, lakini mambo baadaye yalikuja kuwa mazuri, mguu umepona.


hata kuanguka bafuni ni ajali pia, sio lazima ya gari heheeeee, twende kwene kitimoto tukampe pole ze dokta ze rais t camu

 
Kuna habari kuwa katibu mkuu wa CHADEMA na mgombea mtarajiwa wa urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2010 Dr. Wilbroad Slaa amepata ajali na kuvunjika mkono. Dr. Slaa alipatwa na masahibu hayo akiwa jijini mwanza kwa shughuli za kazi za chama chake. Dr. Slaa alitereza na kuanguka bafuni hatimaye kuvunjika mkono akiwa katika hoteli aliyopanga jijini humo. Wasaidizi wake na wafanyakazi wa hoteli hiyo walimkimbiza katika hospitali ya rufaa ya Bugando ambapo baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari ilithibitika kuwa mkono wake mmoja umevunjika. alipatiwa matibabu na kuruhusiwa kutoka hospitali.

Source: RFA news bulletin.

My take: Pole sana Dr. Slaa nikiwa mmoja wa wapenda maendeleo na mchukia mafisadi nakuombea upone haraka ili urudi katika harakati zako za kupigania haki Tanzania.
 
Haya ndomakombora yameanza nini? Haya tutasikia na kuona mengi. Pole Dr Slaa, Upone haraka uendeleze mapambano
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom