Dk Slaa amshangaa Mkapa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemshambulia Rais mstaafu, Benjamin Mkapa na wabunge wa CCM kwa kile alichodai kuwa ni kuendesha kampeni zilizojaa uongo katika jimbo la Arumeru Mashariki na kwamba viongozi hao wanashusha hadhi ya Serikali.

Chadema kilifanya mkutano wake wa mwisho jana kwenye uwanja wa michezo wa Ngaresero ambako CCM walizindulia kampeni zao zilizoongozwa na Mkapa, Machi 12, mwaka huu.

Dk Slaa alisema kama viongozi wakubwa wa kitaifa wakiwa ni watu wa kusema uongo haiwezekani nchi kupata maendeleo.

“Alikuja kwenye uwanja huu, Rais mstaafu Mkapa, badala ya kusema mgombea wao akichaguliwa atafanya nini anaanza kusema Vincent Nyerere hatoki katika ukoo wa Nyerere ,….baada ya kumkosoa anaomba radhi lakini wenzake wanasambaza waraka eti Vincenti hakuzaliwa katika familia ya Nyerere,” alisema Dk Slaa.

Alisema wana CCM hao, wametoa tuhuma za kipuuzi eti, Vincent ambaye ni mtoto wa mwisho kuwa mama yake alikwenda naye kwa marehemu baba yake, Josephat Kiboko Nyerere .

“Ndugu zangu jiulizeni Vincent ni mtoto wa mwisho sasa hata kwa akili ya mtoto kweli unaweza kuhamia kwa mwanaume ukiwa tayari umezaa watoto wanne,” alihoji Dk Slaa.

Dk Slaa alisema kwa upande wa Wassira, amekuwa akimtuhumu kuwa ameiba fedha za ujio wa Papa mwaka 1991 kitu ambacho ni uongo wa mchana na licha ya kuelezwa ukweli na viongozi wa Kanisa Katoliki, ameng’ang’ania kuwa ameiba.

“Sasa mimi nahoji kama kweli nimeiba tangu mwaka 1991 na Serikali ya CCM imeshindwa kunikamata basi ikiri kuwa Serikali yake ni dhaifu, “alisema Dk Slaa.

Dk Slaa pia alimshambulia Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani kwa kutoa taarifa za uongo juu ya kufika kambi ya Chadema na kukumbatiana na mgombea Joshua Nassari na baadaye akakana na kudai gazeti hili limetengeneza picha yake huku akidai mgombea wa chadema ametishia kumuua na kumchoma moto.

“Leo(jana) Mwananchi wametoa picha tofauti ambazo zinaonyesha akiwa katika kambi ya Chadema na akikumbatiana na wanachama wa Chadema na huu ndio uongo wa viongozi hawa wa CCM,” alisema Dk Slaa.

Aliwaomba wapiga kura wa jimbo hilo kumchagua Nassari ili akadhibiti ufujaji wa fedha katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru akimfananisha na paka mwenye uwezo wa kudhibiti panya wengi wanaokula mazao ghalani.

Katika hatua nyingine, Dk Slaa alisema chama chake kimegundua makosa ya baadhi ya majina ya wapiga kura kufutwa kwenye orodha ya wapiga kura na kuwataka wananchi kwenda kwenye vituo vya kupigia kura kuhakiki majina yao na kutoa taarifa kwa viongozi wa Chadema kwenye maeneo yao ili hatua za haraka zichukuliwe kurekebisha makosa hayo ambapo kwa jimbo zima, alisema majina 55 yameondolewa bila maelezo.

Amvaa Lowassa
Katika mikutano ya jana, Dk Slaa alimvaa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kwa kumtaka kujitokeza hadharani kwenye majukwaa ya siasa, badala ya kufanya kampeni za mafichoni.

Akimnadi mgombea wa chama hicho, Nasaari eneo la Malula, Kata ya Kikatiti jana, Dk Slaa alidai kuwapo kwa taarifa kwamba Lowassa amekuwa akipita kimya kimya mitaani kumpigia kampeni mkwewe, Sioi huku akitumia chakula cha msaada kama rungu la kuwatishia wapiga kura.

“Kama Lowasa ni mwanaume kweli ajitokeze hadharani, apande jukwaani kushiriki siasa Arumeru ili Chadema tumtendee haki kwa kumpatia vidonge vyake kwa sababu yeye alishawakana Wameru kwa kukana kabila lake la Meru na kujifanya Mmaasai, leo anakuja hapa kuwadanganya na kuwatisha kwa ajili ya maslahi ya mkwe wake Sioi ili kuongeza idadi ya mafisadi bungeni,” alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema Lowassa akiwa mbunge wa Monduli (CCM) anapaswa kwanza kuchukua hatua za kudhibiti wizi na ubadhirifu unaofanywa ndani ya Halmashauri ya Monduli ambao ulibainishwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), huku kamati hiyo ikitaka wahusika wafikishwe mahakamani.

Kauli ya Dk Slaa kuhusu Lowassa imekuja wakati kukiwa na taarifa kwamba mbunge huyo wa Monduli huenda akapanda jukwaani leo kumnadi Sioi.

Mratibu wa kampeni za CCM, katika jimbo la Arumeru Mashariki, Mwigulu Nchemba alisema jana kuwa Lowassa anatarajia kupanda jukwaani wakati wowote na kwamba kwa siku atakuwa akifanya mikutano kati ya miwili na mitatu kumnadi Sioi.

Hata hivyo Mwigulu hakuwa tayari kutaja siku ambayo Lowassa ataanza kampeni hizo, lakini watu walio karibu na kiongozi huyo walisema huenda akaanza kusimama jukwaani leo.

Mwiguli alisema CCM kilikuwa kinafanya mawasiliano na mbunge huyo kwa lengo la kumjumuisha kwenye ratiba ya kampeni na kwamba ujio wake utaiongezea nguvu timu hiyo.

Wakati hayo yakiendelea, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye anatarajiwa kupanda rasmi jukwaani leo kuongeza nguvu kwenye kampeni za chama chake.

Mbowe anajiunga na timu ya kampeni baada ya kuhitimisha kuongoza harambee ya kukichangia chama hicho iliyofanyika juzi usiku mjini Arusha ambako zaidi ya Sh150 milioni zilipatikana.


Imeandaliwa na Neville Meena, Mussa Juma, Peter Saramba na Moses Mashalla.

Dk Slaa amshangaa Mkapa
 
Ama kweli, siasa za bongo zina mambo!! Cha msingi ni utaifa mbele, ujanja ujanja basi kila mtu alitendee haki hili taifa! Lakini kwa kuendelea na mfumo huu huu wa uchaguzi, kushinda ni hadi kukiwa na uchaguzi mkuu ambapo CCM watashindwa kujigawa!! Ni maoni yangu tu!
 
Wote huu ni ugomvi wa kuwania Jimbo moja la Arumeru mashariki. Hatusikilizi sera za vyama bali ni matusi na vijembe... kama SLAA anaona kuwa MKAPA na wabunge wa CCM ni waongo wapo pia wanaomuona yeye kuwa ni muongo, hiyo ndiyo maana ya siasa ili mradi ushindi upatikane.
 
Wote huu ni ugomvi wa kuwania Jimbo moja la Arumeru mashariki. Hatusikilizi sera za vyama bali ni matusi na vijembe... kama SLAA anaona kuwa MKAPA na wabunge wa CCM ni waongo wapo pia wanaomuona yeye kuwa ni muongo, hiyo ndiyo maana ya siasa ili mradi ushindi upatikane.
Ndio maana ikaitwa neno Siasa maana yake uongo njoo utamu njoo uongo wa siasa ukikukolea ndio utakapo mchagua mtu umpendae hebu tuangalie Mwisho wa uongo wa ARUMERU nani atakuwa mshindi Chademu au Si Si Emu?

Epowers.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom