Dk. Slaa amlipua Lukuvi; Awarushia pia kombora Chami, Simbachawene

WanaJF,
Nimezoea kuitwa majina, mwongo,mpayukaji na kadha wa kadha. Lukuvi labda haelewi hoja. Lakini kwa leo namchallenge, Tangu amepewa kibali hicho ataje ni lini alipewa kibali, na ni shule ngapi amepeleka mbao hizo? Anahitaji miaka mingapi kupasua mbao za kutosha kabla hajapeleka shuleni. Atoke hadharani kujieleza kwa hoja badala ya kutukana kwa kuwa nilijenga hoja, nikatoa ushahidi hadharani nikasema ni "conflict of Interest". Lukuvi na Chami sasa watoe hoja na waweke hadharani ushahidi wao kama nilivyofanya mimi hadharani pale Mafinga. Wana JF si kwamba tunataka tu kulipua, nchi hii inahitaji viongozi waadilifu, siyo viongozi wa kiujanja ujanja. Ni lazima wananchi tusimame kidete kulinda rasilimali za nchi yetu. Sembuse Lukuvi angelipeleka mbao shuleni au madawati, nisingelisita kumpongeza hata yeye anajua hivyo. Lukuvi toka hadharani weka ushahidi wa kupunguza makali kwa shule kwa mbao zilizotokana na ujazo wa mita 1000 uliojipatia.


Chami, Lukuvi wamshukia Dkt. Slaa


Na Mwandishi Wetu

Gazeti la majira; Mei 20, 2011

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dkt. Chyril Chami na mwenzake wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Bw. William Lukuvi wamemshukia Katibu
Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa na kusema kuwa anachanganya maana ya neno 'ufisadi', badala ya kulipua wenzake, anajilipua mwenyewe.

Mawaziri hao walitoa kauli hizo jana kwa nyakati tofauti walipozungumza na gazeti hili kufuatia madai ya Dkt. Slaa kwamba viongozi hao na wanasiasa wengine wanafanya ufisadi kujigawia vitalu vya kuvuna magogo katika msitu wa Sao Hill, Mafinga mkoani Iringa.

Akizungumzia madai hayo, Dkt. Chami alisema tatizo la Dkt. Slaa ni kushindwa kuelewa ukweli katika suala la vibali vya uvunaji magogo hayo na kuchanganya maana ya neno 'ufisadi'.

"Vibali vya kuvuna magogo kwenye msitu huo sio kitu cha siri, ni jambo la wazi, kila mwananchi anaruhusiwa kuomba, wanaokubaliwa majina yao yanabandikwa ubaoni ni mamia ya watu. Hapa Dkt. Slaa anakosea, anashindwa kuelewa maana ya neno ufisadi na kupotosha umma," alisema Dkt. Chami.

Alifafanua kuwa vitalu vya msitu wa Sao Hill ni mali ya serikali na havimilikiwi na mtu yeyote bali umekuwepo utaratibu wa kuvuna mbao kila mwaka ambao hauna tenda na wananchi kwa maelfu wamekuwa wakiomba na kupata vibali hivyo.

" Maelfu ya wavunaji huomba na kupata vibali vya kuvuna magogo kwa utaratibu wa kuandika barua, ni lazima uandike barua kila mwaka kuomba na kulipia kibali hicho. "

"Dkt. Slaa hawezi kuthibitisha kuwa nimejimilikisha kitalu kwasababu hakuna mtu mwenye uwezo wa kujimilikisha msitu wa serikali,"alisema Dkt. Chami na kuongeza kuwa aliomba kibali hiyo kwa nia njema ya kupata mbao za kusaidia ujenzi wa shule mbalimbali jimboni kwake.

Kwa upande wake Bw. Lukuvi alisema mbali ya mawazo yake kuwalipua mawaziri hao, Dkt. Slaa amejilipua mwenyewe kwani ameropoka jambo asilo na ushahidi wake.

Alisisitiza kuwa msitu huo ni mali ya serikali na hakuna yeyote mwenye uwezo wa kumiliki eneo ndani ya msitu huo.

"Dkt. Slaa asome hata vitabu vya sheria, msitu huu ni mali ya serikali, hakuna aliyemilikishwa. Uvunaji wake umewekwa kwenye utaratibu wa wazi kwa kila mtu, hapa ufisadi haupo!" alisema Bw. Lukuvi.

Akaongeza "Niliomba kibali ili nipate mbao za kwenda kuezeka shule ya Idodi iliyoungua kwenye jimbo langu, nilifanya hivyo kupunguza gharama za bidhaa hiyo, nikapata kibali nikavuna mbao za kutosha kama 1,000 nilipomaliza kazi hiyo sikuomba tena kibali kiliisha siku ilele. Anachozungumza Dkt. Slaa ni mambo ya mwaka juzi na hayana ufisadi wowote.

" Fedha nilizolipa kwa Idara ya Misitu kama ushuru na kodi ya kupasua mbao hizo ni 2, 835,330/- Mimi natoa ushauri wa bure kwa Dkt. Slaa asiwe mzee wa mipasho na milipuko. Katika hili, amejilipua mwenyewe baada ya kukubali kupokea maneno na kuropoka bila utafiti, aige mfano wa mbayuwayu" alisema Bw. Lukuvi na kuleza kwamba anamfahamu na kumheshimu Dkt. Slaa kutokana na huduma mbalimbali za shirika la CCBRT mkoani Iringa lakini kwa hili ameteleza
 
Dr.Slaa amini pamoja na majina yote wanayokuita lakini watanzania tuko nyuma yako tukiamini maneno na matendo yako, umekuwa ni kinywa cha wanyonge na msaada wa sisi wanyonge. inawezekana walishindwa kukuelewa kwa sababu ya ama uwezo wao mdogo wa kuchanganua mambo au kwakuwa wamekengeuka na kulewa madaraka. kuchukua mbao kiasi kikubwa tofauti na kibali ni ufisadi, sasa lipi lisiloeleweka kwao.
 
Dr Slaa endelea na harakati za ukombozi,jua kuwa watanzania tulio wengi tunakuunga mkono.Endelea kukemea ufisadi na pia endelea kuwataja mafisadi mbali ili watanzania wawajue wezi wa mali yao.
 
Inaonekana wewe ni magamba, ukiwa waziri kwenye ofisi ya umma kwa nini ujichulie tender, usiache watu huru. lukuvi na chami wanatakiwa kuchagua moja biashara ya ujasiliamali au uwaziri. ila kwa sababu magamba ndio utaratibu wao hatushangai sana, ila the time is coming sio mbali tutawang'oa waende na magamba yao.
 
sasa naamini kuwa chadema wanatumiwa na mapacha watatu kwani hii staili yao ya kutwanga kotekote imelenga kuwaokoa mapacha watatu.kwanini wameanza kipindi hiki wakati walikuwa wanayajua yote hayo? Halafu wanakazana kuwashambulia kina sitta na wengine wanaopambana na mafisadi ndo kabisa wanaonyesha kuwa wanatumiwa.kwa staili hii vita dhidi ya ufisadi itakuwa ngumu sana na nchi itaendelea kuliwa na wenye pesa.

Kama hata chadema imenunuliwa basi watz mjue kuwa ukombozi wetu uko mbali sana! Nyie hamjiulizi kwanini hata gazeti la mbowe la tanzania daima nalo linatumiwa na rostamu? Amkeni jamani na msifikiri chadema kuwa ni chama makini bali ni wanafiki tu!


avatar yako haiendani na kile unachoandika,hivi unamjua vizuri huyo mmiliki wa hiyo avatar.

Acha hayo ni maneno ya akina mama wakiwa wanasukana. Behave basi.
 
Asante mkuu kwa analysis nzuri,i wish kila mwana JF angeipitia@
Mwandishi wa habari hii ameandika vizuri sana, sijui shida iko wapi, labda uvivu kwa baadhi ya watu kusoma tu au umamluki.

Hoja ya Dr Slaa ipo kwenye mgongano wa kimaslahi na si kwenye ushindani. Kwa kuwa wale waliopewa dhamana ya kusimamia huo ushidani uwe fair, ndio wa kwanza washiriki then dhamana hiyo haitamsaidia mtu wa kawaida. Viongozi wetu wamekosa kuitii miiko ya uongozi. Utetezi wa Lukuvi kuwa alivuna msitu ili kupasua mbao za ujenzi wa shule haina mantiki kwa kuwa shule aliyoipa msaada inajulikana, kuna uongozi wa shule, shule hiyo ingeliweza kuomba kibali, yeye akatoa msaada huo wa fedha. Alikuwa hana haja ya kutoa fedha and at the same time kwenda kufanya kazi ya kuvuna magogo na kuwapelekea mbao. Msaada wa shule hapa naona kama ameutumia kama kivuli kununua huruma ya watanzania. Ni vyema akatoa details, kibali chake kilikuwa cha kuvuna hekari ngapi za misitu, alivuna kiasi gani na je hiyo shule ilijengwa k
 
Ingawaje inataka roho ya mwendawazimu kumkosoa Dr. Slaa humu JF lakini mimi naridhia matokeo ya kitendo hicho.

Nilikuwa namuangalia Lukuvi katika ITV usiku huu na alitoa maelezo ambayo kwa kweli yana-make sense ya hali ya juu kwa vile kule Mafinga kuna msitu ambao upande mmoja unamilikiwa na SPM na upande wa pili unamilikiwa na Sao Hill na haujabinafsishwa kiasi cha watu kumiliki vitalu.

Kinachotokea ni kwamba mtu akitaka kibali cha kuvuna msitu anaomba kwa Meneja wa Msitu kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii halafu ukifanikiwa ndo unavuna. Utaratibu huu ndiyo ninaoufahamu mimi na nakumbuka hata jamaa zangu ninaowafahamu ambao ni wachuuzi wa mbao wamekuwa wakifanya.

Hii kiu ya kutaka kuonekana kwamba wewe ni mtu wa kulipua mabomu, wakati mwingine bila kufanya utafiti wa kina kuhusu usahihi wa taarifa ambazo mara nyingi huzipata kupitia kwa watu wengine, inaweza kumvunjia heshima na mwisho anaweza kujikuta akiwa kama bwana Lyatonga alivyokuwa katika miaka ya 90 mpaka akaonekana mzushi. Natoa tahadhari tu!

Natumaini wewe ni mheshimiwa Lukuvi. endelea kujitetea mpaka wakuelewe.
Kama sera zingekuwa wazi kihivyo msingekuwa mnapigiwa kelele na watu walala hoi wa nchi hii.
Kiongozi na mishahara miwili tena yote toka serikarini; huu ni wizi mtupu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom