Mbutunanga
Senior Member
- Feb 15, 2011
- 182
- 45
Sasa naamini kuwa chadema wanatumiwa na mapacha watatu kwani hii staili yao ya kutwanga kotekote imelenga kuwaokoa mapacha watatu.Kwanini wameanza kipindi hiki wakati walikuwa wanayajua yote hayo? Halafu wanakazana kuwashambulia kina Sitta na wengine wanaopambana na mafisadi ndo kabisa wanaonyesha kuwa wanatumiwa.Kwa staili hii vita dhidi ya ufisadi itakuwa ngumu sana na nchi itaendelea kuliwa na wenye pesa.
Kama hata chadema imenunuliwa basi watz mjue kuwa ukombozi wetu uko mbali sana! Nyie hamjiulizi kwanini hata gazeti la Mbowe la
Tanzania daima nalo linatumiwa na Rostamu? Amkeni jamani na msifikiri chadema kuwa ni chama makini bali ni wanafiki tu!
Ingawa inaonekana unataka kupindisha point ya muhimu inayojadiliwa katika uzi huu, binafsi ningependa CCM waamini kuwa Chadema wanawatetea mapacha watatu na kwa kuwa huwa wanafanya vitu kuwapinga chadema hapa watalazimika kuwawajibisha hao mapacha watatu ili mradi tu waonekane kuwa wanapambana na chadema na sie waDanganyika kufaidika kwa kuwajibishwa kwa hao mafisadi. Ila pia ninachoshangaa ni kuwa CCM ndo wana mamlaka ya kuwawajibisha hao, kwa nini hawafanyi hivyo?