Dk slaa amechakachua barua

Hiyo Press Conference ni Ya Idara ya Usalama wa Taifa; ambayo iliona UMUHIMU KUJIBU TUHUMA NZITO DHIDI YAKE.

Wengine pia wamejibu

1. Rostam
2. Lowasa
3. Ridhwani
4. Kinana
5. NEC

Serikali hii inahuruma Sana; kwa kuwa wanailea Democracy; hawataki kuonekana wanamuonea Slaa kwa kumshtaki. Ila wakiamua, wanamshtaki. SEMA ATAANZA KUTAKA UJIKO, ETI ANAONEWA; wakati ameshiriki kuchakachua barua kwa lengo zima la kuitukanisha serikali wa Wananchi na kutafuta CHEAP POPULARITY

Kama serikali hii ina huruma sana, hiyo huruma ingeonekana:

1. Kwa Watanzania kwa kupunguza matumizi ya anasa serikalini na kuboresha huduma za jamii.
2. Kwa wazee wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwalipa mafao yao kulingana na 'dollar value' kwa vile umepita muda mrefu sana walau zaidi ya miaka 30.
3. Kufanya juu-chini raslimali za nchi zinalindwa kwa udi na uvumba ili ziwanufaishe Watanzania na siyo matajiri wachache.
4. Udanganyifu unapungua ili watu wachague viongozi wao kwa haki na uhuru na pia wanaofaulu mitihani au kupata ajira wawe wale wenye 'merit' na siyo rushwa (uchakachuaji).
5. Ukuaji wa uchumi tunaousoma kwenye vyombo vya habari ungeendana na ubora wa huduma za jamii ili wananchi waondokane na umaskini unaowanyemelea kila siku.
6. Jiji la Dar es Salaam lisingekuwa linanuka kinyesi usiku na mchana kwani si salama kwa afya za wakazi na wageni wanakuja jijini!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom