kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kusitisha mara moja kutangaza matokeo ya urais kwa madai kuwa kuwa kura hizo 'zimechakachuliwa'.
Dk. Slaa anataka uchaguzi urudiwe na si kurudia kuhesabu kura.
Mwenyekiti wa Nec, Jaji Lewis Makame amemshangaa Dk. Slaa kwa kuwa hajafanya mawasiliano yoyote na tume hiyo.
Jaji Makame amesema, kama Dk. Slaa ana uhakika , apeleke nyaraka zake ili zilinganishwe na nyaraka zinazotumika kutangaza matokeo.
Akizungumza jana katika mkutano aliouitisha wa waandishi wa habari Dar es Salaam, Dk Slaa aliitaka Nec isitishe kutangaza matokeo ya urais, ambayo mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amekuwa akiongoza, mpaka haki itakapotendeka.
Dk. Slaa ambaye katika matokeo yaliyokwishatolewa na Nec mpaka sasa ameachwa mbali na Kikwete.
Alidai katika matangazo ya kura hizo, maeneo mengi yanayotangazwa, kura zake zimebadilishwa ili kuiwezesha CCM kuibuka na ushindi.
Baada ya kuona hali hii niiombe Nec kama tuna utashi mwema na nchi, ifute matokeo yote ya urais kwa nchi nzima na kurudia kama ilivyofanya katika jimbo moja kwa kuwa hatuwezi kukubali matokeo ya vyombo vya dola kwa kuwa tulihisi muda mrefu, alisema Dk. Slaa.
Ametoa mfano wa Jimbo la Same Mashariki, ambako alidai ni kielelezo cha wizi wa kura.
Amedai kuwa, katika fomu yenye namba 03182, CCM ilipata kura 92 wakabadilisha na kujipa kura 123, Chadema ilipata kura halali 66 zikapunguzwa na kubaki 33.
Tumetumia njia nyepesi ya sampuli kujua wizi huo maana aina ya pili ya wizi waliotumia ni kubuni kituo hewa, kuna kituo hewa Na 002586, kituo halali ni namba 002582 kura zinafanana katika fomu halisi hapo CCM walijipa kura 190 na Chadema 26, alieleza.
Hata hivyo katika utangazaji wa matokeo ya urais, Nec haitangazi matokeo ya vituo vya uchaguzi kama mifano ya Dk. Slaa inavyoonesha, bali imekuwa ikitangaza matokeo ya jumla ya jimbo.
Dk Slaa pia amemtaka Mkuu wa Usalama wa Taifa , kujiuzulu mara moja wadhifa huo kwa madai kuwa, kwamba ameshindwa kuwajibika ipasavyo na kuonekana kuwa upande wa chama kimoja.