Elections 2010 Dk Shein atajwa kujitosa kinyang'anyiro cha urais Zanzibar

Nyie watu mwashangaza sana - fisi na mbuzi eti wanaishi pamoja tena kwa amani, duh. Toka lini maji na mafuta yakachanganyika au ibilisi na malaika wakashirikiana bila mikwaruzo ? Kwamba jamaa ni msafi lakini kafumbia macho uchafu uliomzunguka na kwa namna fulani ameridhika na hali hiyo kwani haimstui wala haimnyimi usingizi. Sasa atakuwa anasukumwa na nini - uwoga, uzalendo, unafiki au ulafi kama wenziwe, kalaghabaho !
 
Wazanzibari mpeni nchi MD huyu awapeleke mbele.Huyu mzee pamoja na kuifuata hiyo dini yake lakini pia maadili ya taaluma yamemuingia vema sana.Siyo mtu wa porojo porojo na kukurupuka.
Muda umefika sasa watu wa sayansi wachukue mamlaka ya juu ya nchi hii.Go Shein go!
 
Kwa data chache nilizonazo, Dr karume kamuomba sana Dr Shen agombee urais zanzibar...... akibubali basi Dr Karume ndio mgombea mweza wa JK October 2010, kisha 2015 yeye ndio raisi wa Muungango........ mwaonaje wazee wanavyochanga karata zaoooooooooo
 
Umakamu wenyewe amekaa pale kama picha ya ndege tu, hana hadhi wala utashi wa kisiasa! Washamtumia vya kutosha, akapumzike
 
2015 yeye ndio raisi wa Muungango........ mwaonaje wazee wanavyochanga karata zaoooooooooo
Nani kakwambia kuwa akiwa mgombea mwenza twenty fifteen anakuwa rais wa muungano? halafu huyu mwinyi bora akae huko huko kisiwani huku bara hatutaki mamwinyi. Above all 2015 wakikaa vizuri hiki chama kitakuwa cha upinzani!
 
Wakati ccm imepeleka majina matatu ya wagombea wa urais wa zanzibar likiwemo la dk shein ,,habari zaidi zinasema mzee wetu ana uwezo mkubwa wa kushinda hasa kwa wengi kumpendekeza na kuahidi kumpigia kura..kwaniaba ya wapenda amani,na wasioongea sana kama mimi namtakia heri nafanaka mh shein kuwa kiongozi wetu wa zanzibar mtarajiwa
wasalaam
 
Wakati ccm imepeleka majina matatu ya wagombea wa urais wa zanzibar likiwemo la dk shein ,,habari zaidi zinasema mzee wetu ana uwezo mkubwa wa kushinda hasa kwa wengi kumpendekeza na kuahidi kumpigia kura..kwaniaba ya wapenda amani,na wasioongea sana kama mimi namtakia heri nafanaka mh shein kuwa kiongozi wetu wa zanzibar mtarajiwa
wasalaam

Je! sisi wapenda amani tukubali uwezo wake na upendo wake wa amani na utulivu,wakati ataingia madarakani kwa nguvu za kiza?
 
Jamani Shein si mwanasiasa... mtakuja kuona, anatengenezwa tu na watu ili waendeleze himaya yao
 
Halisi,

Hii ndio ilikuwa mbinu ya CCM kuua CUF..Shein anaweza kutokuwa mwanasiasa lakini anakubalika kote kuliko watoto wa Karume au Mwinyi...Na lini Tanzania tumekuwa na kiongozi mwanasiasa kama sii Nyerere na Abeid Karume!..

Somo la leo:- Kuna uwezekano safari hii CCM akafunika Zanzibar.
 
Jamani Shein si mwanasiasa... mtakuja kuona, anatengenezwa tu na watu ili waendeleze himaya yao

Heshima kwako mkuu.. hakuna zaidi ya hilo. la ziada nilikua najiuliza suala moja, Marekebisho ya serikali ya mpito ikipita, Rais akiwa mpemba,makamo wa pili mpemba maalim,na wa kwanza nasikia mohamed abud mpemba, sasa waunguja wenzangu,lkn wao ccm,mimi siwezi kuwa ccm,walisema mpemba haiwezekani,itakuwaje? wanalo hao ccm wenyewe kwa wenyewe.. duuuuuuu
 
1) Kwanza kwa Upemba kule wanasema ni wa "kuchovya" maana ametoka akiwa na miaka minne, ni sawa umwambie Obama akagombee na urais Kenya....au Sepetu akawanie Ubunge kule Sikonge Tabora, au Juma Nhunga atoke Dole akawanie Bariadi alikozaliwa.

2) Dk. Shein toka ahamie Znz kuwa daktari amekuwa yye na hospitali hana social contact, hajihusishi na masual yoyote ya kijamii. Kibaya mtangulizi wake, Marehemu Dk. Omar Ali Juma, alikuwa mtu wa kujichanganya, Shein siye

3) Tokea mwaka 1995, amekuwa mtu wa kubebwa, hana utashi binafsi wa kisiasa, hata hili yeye amekuwa akimuandaa Mohamed Aboud kwa muda mrefu na kwa nia njema kabisa, sasa watu wenye maslahi binafsi wakiongozwa na...... (ntawataja baadaye) ndio wanamsukuma ili watawale Zanzibar

4) Mwaka 1995 Dk. Shein aliiingia katika siasa kwa kuombwa na kina Dk. Salmin baada ya CCM kuwa wanahaha kutafuta watu wa kushindana na CUF Pemba, sasa Shein akaahidiwa hjata akishindwa atapewa Unaibu Waziri na kweli akashindwa akapewa Unaibu wa Afya baada ya kuteuliwa kuwa mwakilishi.

5) Mwaka 1997, Dk Salmin alimuomba tena Shein kuwania ujumbe wa NEC na akamwambia akishindwa atamuomba Mkapa amteue na alipoenda akawa mtu wa pii nyuma ya Mohamed Aboud mkoa wa Kusini Pemba, na alizungukwa kwa kura hii maana yake ni kwamba hana political base.

6) Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2000, Dk. Shein aliomba kazi nje ya nchi na alipata na hiyo ni baada ya kuona kwamba yeye alikuwa kundi la Dk. Salmin na hivyo Karume asingemfaa, lakini Karume akambiwa amchukue na kumuomba tena awanie Mkanyageni, ambako alipata baada ya kushindwa na kura za "Maruhani" za CUF na akateuliwa kuwa Waziri wa Utawala Bora...

Mwaka 2001 kukatokea mauaji Januari, baada ya CUF kupambana na Ngunguri (Mahita, FFU, KMKM, JKU) na kabla hata haijapoa Taifa likapata msiba mzito wa kuondokewa na Makamu wa Rais, Dk. OMar Ali JUma, na Shein akapata tena bahati ya kuteuliwa kuwa makamu wa Rais. Hakugombea wala hakufanya kampeni.

2005 kila mtu anajua hakuwa chaguo la JK na Mkapa na wazee wakamtaka JK amteue kuwa mwenza na kwa mazingira ya wakati ule hakufanya kampeni ila JK alikua na nguvu.
 
Shein, hana kitambulisho cha ukaazi Zanzibar na hana nyumba Unguja, sasa atachagulika?

Kwa taratibu za uchaguzi Zanzibar anakubalika kushiriki?

Mpaka sasa hana timu ya kampeni sasa atashindaje huo u-Rais?

Kama alivyosema Halisi, hakuwa chaguo la JK, bila shaka nadhani ndio njia sahihi na salama ya JK Kuachana naye! Binafsi nina wasiwasi wa yeye kupita, kwani wenzake wamejiandaa mno!
 
Back
Top Bottom