Dk Salim Ahmed Salim: Mfumo wa serikali umeoza kwa rushwa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,009
salimahmed.jpg

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Tanzania na Waziri Mkuu wa Zamani, Dk Salim Ahmed Salim.

Na Elias Msuya

Mwananchi


MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM na waziri mkuu wa zamani, Dk Salim Ahmed Salim amesema kuwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea urais sambamba na Jakaya Kikwete waachwe wapambane naye, lakini akasema hawatamuweza.

Baadhi ya jumuiya za CCM na vikundi kadhaa ndani ya chama hicho vimeshamtangaza Kikwete kuwa mwanachama mwingine asijitokeze kupambana na Kikwete kwenye uchaguzi ujao na kwamba vinamuunga mkono kiongozi huyo.

Lakini Dk Salim, ambaye aliwahi kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Afrika (OAU), aliiambia Mwananchi katika mahojiano maalum nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana, WanaCCM wana haki ya kupambana naye kuwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho tawala..

Dk Salim alisema si makosa kwa wanachma wa CCM kujitokeza kuomba ridhaa ya wanachama kugombea urais kwa tiketi ya CCM katika kipindi cha kwanza cha rais aliye madarakani.

Alisema kwamba licha ya kuwepo kwa utaratibu wa CCM wa kumuachia rais aliye madarakani amalizie vipindi viwili vya madaraka yake, bado haoni tatizo kwa mwanachama wa chama hicho kujitokeza kugombea urais.

Alisema kwamba hata kama wanachama hao watajitokeza watapitia kwenye taratibu na mchakato wa chama wa kuwachuja.

"Huo ni utaratibu wa CCM ambao una maslahi kwa chama. Hata hivyo, watu wanaweza kujitokeza tu kugombea sambamba na Rais Kikwete. Kama watajitokeza watapitia kwenye mchakato wa chama ambacho ndicho kitaamua kimpitishe nani. Hata hivyo, kwa sasa sioni mtu wa kumshinda Rais Kikwete," Dk Salim alisema.

"CCM ina utaratibu wa kuachiana vipindi viwili. Ni utaratibu uliowekwa kwa maslahi ya chama katika mazingira ya siasa za leo. Lakini, hata kama watajiotokeza wanachama wengine, bado Rais Kikwete ana nguvu ya kuwashinda. Sidhani kama kuna mwanachama ambaye anaweza kupitishwa zaidi ya Kikwete,".

Hadi sasa mbunge wa jimbo la Maswa mkoani Shinyanga, John Shibuda ndiye pekee aliyetangaza nia yake ya kuvaana na Kikwete kuomba ridhaa ya chama kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2010.

Makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa alishaweka wazi kwamba katika mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia chama hicho mwakani ni ruksa kwa wanachama kuomba nafasi ya urais kwa kuwa katiba inawaruhusu.

Lakini kabla ya Msekwa kutoa ufafanuzi huo, makamu mwenyekiti wa zamani wa CCM, John Samuel Malecela, kundi la wenyeviti wa mikoa na wazee wa chama hicho, walitangaza wazi kwamba Rais Kikwete apitishwe amalizie kipindi chake cha pili cha uongozi kama ilivyo desturi ya chama hicho.

Mfumo wa serikali unanuka rushwa

Akizungumzia suala la mapambano ya rushwa, Dk Salim alisema mfumo wa serikali ya Tanzania umeoza kwa rushwa na hivyo hauwezi kumsaidia rais kuikabili, hivyo rushwa kutawala kuliko kitu kingine.

Alisema tofauti na wakati wa rais wa awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Nyerere wakati rushwa ilipodhibitiwa kikamilifu, wakati huu rushwa imeachiwa nafasi kubwa kiasi ambacho kinafanya hali ya Watanzania kudorora.

"Tukisema kwamba tatizo halipo tutakuwa tunakosea. Tulilokosea ni kuliachia tatizo la rushwa lishamiri kama lilivyoshamiri sasa. Rushwa haikuanza jana, haikuanza na serikali ya awamu ya nne, wala serikali ya awamu ya tatu wala ya pili. Rushwa ilikuwepo tangu awamu ya kwanza," alisema.

Lakini akasema tofauti kubwa kati ya awamu hizo na ile ya Mwalimu Nyerere ni kwamba muasisi huyo wa taifa alionyesha kwa vitendo kuwa rushwa ni jambo aliloamua kulifungia mkanda na kupambana nalo, lakini baada ya hapo tatizo hilo limeachiwa liendelee kiasi cha rushwa kugeuka kuwa utaratibu.

Alisema kwamba licha ya nia njema ya Rais Kikwete ya kupambana na rushwa na ufisadi, bado mfumo mzima wa serikali umeoza kiasi ambacho haiwezekani kupambana na rushwa.

"Rais Kikwete anajitahidi na ana nia ya kupambana na rushwa, lakini bado 'system' (mfumo) haijajitayarisha vya kutosha kupambana rushwa," alisema.

Licha ya kuitetea CCM kuwa haihusiki na ufisadi bali baadhi ya watendaji wake ndiyo wanaojihusisha na ufisadi, Dk Salim alisema rushwa ni kansa inayoitafuna nchi.

"CCM kama chama si tatizo bali baadhi ya viongozi hawafuati katiba ya chama. Rushwa ni kansa inayoathiri jamii ya Watanzania. Mategemeo ya wananchi ni kuona CCM ndiyo iwe mstari wa mbele kupambana na rushwa na ufisadi kwa sababu hata katiba na ahadi za chama zinasema rushwa ni adui, sitapokea wala kutoa rushwa. Sasa hapa ndiyo kwenye tatizo," alisema Salim.

Aupongeza uongozi wa Spika Sitta

Dk Salim alisema kwamba Bunge la sasa limepiga hatua kubwa katika kutoa kero za wananchi hasa kipindi hiki cha mfumo wa vyama vingi.

"Kwa kweli Spika Samuel Sitta amejitahidi sana kuendesha Bunge lenye viwango, hasa wakati huu wa mfumo wa vyama vingi. Bunge ndiyo sauti ya wananchi; ni njia pekee ya wananchi kutoa kero zao kwa serikali. Kwa hiyo linatakiwa liendeshwe katika 'health environment' (mazingira mazuri)," alisema.

"Tukiwa na Bunge kama hili ambalo linawapa wabunge nafasi ya kuzungumza kama hivi ni safi kwani inakuwa changamoto kwa mawaziri. Inawalazimu mawaziri kuwa na 'home work '(kazi ya ziada) kila wanapokwenda bungeni kujibu maswali," alisema Salim.
 
Last edited:
Umesema Ukweli Salim. Hongera sana maana najua kuwa hali kama hizi ndio zinashababishwa watu kushindwa kufikiwa malengo yetu kama Taifa
 
Mara nyingi ninakuwa na wasiwasi sana na matamshi ya watu hawa.Sina hakika kwamba kweli Salim anayo ongea yanatoka moyoni.Sioni kwanini aseme Kikwete ana nia ya dhati ya kupiga vita ufisadi wakati tunaona wazi kwamba hana nia hiyo.Lipi Kikwete amelifanya kuonyesha kwamba ana nia ya dhati ya kupiga vita ufisadi, tunamuomba alisema.

Matamshi haya tumeshayazoea.Ni mbinu zile zile za akina Sofia Simba,akina Makamba na wengine.Ni mbinu zile zile chafu za CCM za kuwadanganya watanzania kwamba viongozi wa chama hicho wako pamoja na wanachi,kumbe ni simba wakali wanao watafuna.
 
1;nilikuwa sijui kama dk salimu aliwahi kuwa waziri mkuu,nilikuwa nadhani aliishia kuwa naibu waziri mkuu kama mrema.
2;mkuu koba kuna uhusiano gani wa dicota na salim au thread hii yote?kama mdau che kalizozele alivyouliza sioni uhusiano wowote,tufahamishe mkuu

Mkuu Mwana va Mutwa heshima mbele.

Dr Salim A Salim alishakuwa waziri mkuu na baadaye akawa naibu waziri mkuu na waziri wa ulinzi.

Katika historia ya Tanzania ni Dr Salim A Salim na Bwana A L Mrema tu ndiyo waliwahi kupewa wadhifa wa naibu waziri mkuu ingawa cheo hicho hakimo katika katiba ya Tanzania.

Dr Salim A Salim alikuwa naibu waziri mkuu enzi za utawala wa Mzee Ruksa [Ali Hassan Mwinyi].Mheshimiwa Jaji Warioba alikuwa waziri mkuu.Katiba ya JMT isingeruhusu wazanzibar watatu kukamata nafasi zote za juu.Rais alikuwa anatoka Zanzibar A H Mwinyi,Makamu wa kwanza wa rais na waziri mkuu Warioba J S anatoka bara,Rais wa Zanzibar na makamu wa pili wa rais komamdo Salimin amour wa Zanzibar.
 
Dk Salim ni moja ya viongozi mahiri kabisa katika taifa hili.

Nadhani analitambua wazi kabisa kama nikuwa mbele nakupiga debe kuhusu ufisadi hakosi uchafu wake uliofichika kuumbuliwa kama yanayomkuta Warioba saa hivi.

Kelele za Warioba zimeishia wapi zote zile? Lazima Dk Salim aseme Jk atashinda na ni lazima ajifanye kukubali kwamba Jk ana nia ya dhati ya kupambana na ufisadi ilhali hiyo nia haipo na wala siyo ya dhati kama anavyotaka tuamini!
 
ukweli ni kuwa ccm waache hii siasa yao ya kudictect wanachama wao ati lazima amalize vipindi viwili mimi sioni logic

anaetaka kugombea na apewe fursa na kama kweli aliekuwepo ametekeleza vyema wajibu wake basi atapita tu na kama akipita kwa shida atapata muda awakujipanga vyema

pia naamini wakiachana na mpango huo wa kumpa garentee aliepo itamfanya atekeleze vyema sera za chama chake maana anaamini asipofanya hivyo hapatokuwa salama ktk kukamilisha kipindi cha pili. mie sioni kuwa huko ni kulinda maslahi ya chama

walioangalia kuwa maslaha ya chama waliangalia kwa upande mmoja, maana huenda akatokea kiongozi amabe atafanya madudu na aendelee

ccm ni chama imara naamini hili wataliangalia na kulipatia suluihu la maaana
 
Dk Salim ni moja ya viongozi mahiri kabisa katika taifa hili.
Nadhani analitambua wazi kabisa kama nikuwa mbele nakupiga debe kuhusu ufisadi hakosi uchafu wake uliofichika kuumbuliwa kama yanayomkuta Warioba saa hivi.
Kelele za Warioba zimeishia wapi zote zile??????????Lazima Dk Salim aseme Jk atashinda na ni lazima ajifanye kukubali kwamba Jk ana nia ya dhati ya kupambana na ufisadi ilhali hiyo nia haipo na wala siyo ya dhati kama anavyotaka tuamini!

Kwa maoni yangu naona kama hakuongea toka moyoni. Alikuwa anaongea ili kuhakikisha hamuweki Kikwete katika hali ngumu. Hakuna yoyote aliyedhani kwamba Hillary angeangushwa na Obama katika kugombea nafasi ya kuwa mgombea wa Democratic Party. Hivyo kama Hillary aliweza kuangushwa na Obama pamoja na pundits wote kudai kwa kila kitu kuanzia organisation, ability to raise funds n.k. Hillary alimuacha mbali sana Obama, lakini pamoja na yote hayo Obama aliweza kumuangusha Hillary.

Hivyo basi sikubaliani na SAS kwamba katika wagombea ambao watakaojitokeza kugombea pamoja na Kikwete (kama CCM itawaruhusu kufanya hivyo) ili kupata nafasi ya kuwa mgombea wa CCM hakuna mwenye nafasi ya kumuangusha Kikwete hasa tukitilia maanani hali halisi ya uongozi wa Kikwete ambayo haiwaridhishi Watanzania walio wengi hata wale wajumbe ndani ya CCM ambao wanahusika na kumchagua mgombea wa CCM. Kama Hillary aliweza kuangushwa basi na Kikwete pia anaweza kuanguka na kutopata nafasi ya kuendelea hadi 2015
 
Last edited:
..watu wanazungumza kama vile hakuna vyama vingine isipokuwa CCM.

..hakuna haja ya kuwalazimisha CCM kubadili utaratibu wao wa miaka nenda rudi.

..anayetaka kugombea Uraisi 2010, na yuko serious, basi aanze kutafuta chama mbadala kwa CCM.
 
Bubu Ataka Kusema,

..hapo kwenye posting yako umechanganya madawa.

..ungetoa mfano wa harakati za Robert Kennedy zilivyomlazimisha Raisi Lyndon Johnson asiombe nomination ya Democratic Party.

..pia ungetoa mfano wa Edward Kennedy alivyompinga Raisi Jimmy Carter asigombee kipindi cha pili.
 
Bubu Ataka Kusema,

..hapo kwenye posting yako umechanganya madawa.

..ungetoa mfano wa harakati za Robert Kennedy zilivyomlazimisha Raisi Lyndon Johnson asiombe nomination ya Democratic Party.

..pia ungetoa mfano wa Edward Kennedy alivyompinga Raisi Jimmy Carter asigombee kipindi cha pili.

Hapana Mkuu JK, sikutaka kwenda mbali hivyo, maana mfano wa Obama ni wa juzi tu. OBAMA alikuwa ameachwa kwa 25 points katika opinion polls na hakuna hata mmoja aliyempa nafasi hasa ukitilia maanani kwamba US haijawahi kuwa na Rais mweusi na Hillary alikuwa na jina kubwa na kila kitu lakini bado alianguka. Hivyo mfano wa Obama kwangu mimi una nguvu zaidi kuliko hiyo mingine.
 
Tatizo tuna wa focus sana hawa CCM, lakini ukweli ni kwamba leo hii upinzania wakiweka mtu makini kama DK Slaa kupambana na JK na uchaguzi ukawa free and fair, JK hana bao atatupwa kwa mbali saaaana. Watu wamechoka na usanii wa serikali yake.

Leo hii wananchi wanamkumbuka Mkapa, kwani wakati wake mfumuko wa bei ulikuwa controlled, hivyo walipata mahitaji yao kwa bei nzuri tofauti na hivi sasa kwa hiyo kauli za kina Salim ni mbinu ya CCM kuwapumbaza watu waione kuwa chama pekee chenye uwezo wa kutoa Rais. Tumechoka na propaganda zao.
 
Bubu Ataka Kusema said:
Hapana Mkuu JK, sikutaka kwenda mbali hivyo, maana mfano wa Obama ni wa juzi tu. OBAMA alikuwa ameachwa kwa 25 points katika opinion polls na hakuna hata mmoja aliyempa nafasi hasa ukitilia maanani kwamba US haijawahi kuwa na Rais mweusi na Hillary alikuwa na jina kubwa na kila kitu lakini bado alianguka. Hivyo mfano wa Obama kwangu mimi una nguvu zaidi kuliko hiyo mingine.

BAK,

..baada ya ufafanuzi huu nimekuelewa.

..thanks!!
 
Mi nakubaliana kabisa na Dr Salim, na nadhani ameongea toka moyoni. Tatizo linalotukabili Bongoland sasa hivi ni kuwa mfumo mzima wa utawala umejaa rushua (Mzee Mwinyi huiita hivyo). Chama tawala ndo nguzo kuu ya rushwa na uozo, rais ameingia madarakani kwa kutumia mbinu hizohizo za rushwa. Wabunge wameingi bungeni kwa kutoa rushwa, watu wanaajiriwa kwa kutoa rushwa. yaani kila kitu ni rushwa, rushwa, rushwa. Unategemea ujasiri wa kupambana nayo hao watu watautoa wapi? Sasa hivi TZ wala rushwa ndo mashujaa wanapokea standing ovation kila wanakopitia, ajabu sana!
Inatakiwa kiongo menye moyo mgumu kama jiwe kuweza kuwageuka wenzie na kuipiga vita rushwa kwa kudhamilia.
 
SAS hapa anauma na kupulizia tu. Hakuna lolote ambalo JK anaonyesha kuwa anapambana kwenye vita dhidi ya rushwa. Kumsifia JK kwa kitu ambacho hafanyi ni kujipendekeza tu kwake na SISIEMU kwa ujumla.
SIMAMA UHESABIWE.
 
Ningekuwa Salim ningeachana na CCM. Kwa yeye kudai kuwa serikali ina rushwa wakati serikali hiyo hiyo inaongozwa na kamati kuu ya CCM ambayo yeye ni mjumbe wake ni kontradikshen.
 
Dr Salim A. Salim ni mjumbe wa CC na NEC. Siku Bwana Sitta akisulubiwa na mafisadi pale Dodoma, yeye alikuwa wapi? Kwanini hakusimama kuwakemea hao waliokuwa wanamkejeli Sitta?

Haya mambo yanasikitisha sana, wakiwa kwenye vikao vyao vya Chama hawasemi kitu, wakija huku nje ndio wanaanza kutuzuga mara uongozi wa Sitta ni mzuri, mara sijui CCM inapiga vita ufisadi, mara sijui Katiba ya CCM inapinga rushwa ... wizi mtupu!

Kuwepo kipengele cha kupinga rushwa ndani ya Katiba ya CCM haimaanishi kwamba kinafuatwa na kutekelezwa kama uongozi wa juu umezama kwenye lindi la ufisadi na rushwa. Ni sawa na kuwa na sheria halafu kusiwe na mtu wa kusimamia kuhakikisha sheria hiyo haivunjwi.

CCM wako makini na ufisadi wa hela za chama chao, lakini siyo ufisadi wa mali ya umma. Kama kuna mtu anabisha aende akamuulize Mujuni Kataraiya aliyekuwa katibu wa CCM pale Singida na Maregesi aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Wazazi. Hata vita ya rushwa ndani ya CCM inategemeana ni nani anahusika, wengine huwa wako out of reach hata kama watashikwa na kithibiti. Usanii mtupu.
 
Ningekuwa Salim ningeachana na CCM. Kwa yeye kudai kuwa serikali ina rushwa wakati serikali hiyo hiyo inaongozwa na kamati kuu ya CCM ambayo yeye ni mjumbe wake ni kontradikshen.


Na kile kikao cha CC cha hivi karibuni ambapo mafisadi na wakinga kifua wao walimzodoa Sitta na yeye kama alihudhuria kikao kile bila kutia neno kuhusu kuzodolewa kwa Sitta hadi alipohojiwa na gazeti la Mwananchi haileti picha nzuri kwa kweli. Huyu ni mmoja wa watu ambao Watanzania wengi tunamwamini sana na ana hadhi kubwa hata katka jumuiya ya Kimataifa lakini kwenye hili la kuuma na kupuliza kwa maoni yangu amevurunda. I hope atakuwa anaongea mara nyingi tu katika kipindi hiki cha kuelekea October 2010 hasa ukitilia maanani nchi yetu inavyoenda mrama.
 
Back
Top Bottom