Kwenye kundi la Nchimbi kuna Asha Kigoda ambaye kila Spika bila aibu anakazana kwa sauti kumwita Dr.Asha Kigoda .
Dr Aisha Kigoda hawezi kuwa kwenye kundi la Nchimbi kamwe. Aisha amesomea udaktari katika ngazi inayoitwa Assistant Medical Officer, ambao nchini Tanzania wanatambulika na pia wana leseni kutoka Baraza la Madaktari, na katika leseni zao hizo hutambuliwa na kuandikwa Dr (kabla ya jina la mhusika). Kwa hiyo Dr Aisha Kigoda "hajajiita" daktari, bali kapewa cheo hicho na Baraza la Madaktari baada ya kufikia kiwango ambacho Baraza hilo linakubali aitwe hivyo. Na wala hajafoji vyeti, maelezo yake anayotoa kwenye wasifu wake ndiyo elimu halisi aliyo nayo, na vyuo alivyosoma ni vya Tanzania na vinatambulika. Msimwonee dada wa watu.