Dk. Mwakyembe amrushia Sugu kijembe

Sio kweli ka sugu kapata ubunge kibahatibahati, ckia alimzidi mpinganzi wake zaid ya kula elfu ishirini, so cjui kama ni bahati. By the way jamaa alichaguliwa na vijana wengi. Alikubarika kiukweli
 
Mimi sina chama ila Mwakyembe nilimshusha thamani ile siku alivyotangazwa kuwa waziri. Nikabishana na washkaji ambao wao wakimpenda mtu hata afanyeje wanakufa nae. How can you be a subordinate to someone you criticised openely? Tena nikasema huyu jamaa ndo kaisha kisiasa kwani yaweza tokea mabadiliko ya baraza akatemwa na hatoweza kupiga domo tena kama zamani! Nikasema ni njaa. Na nadhani nilitoa comments hata JF kuwa jamaa kaisha. Wengine wakasema ooh anaenda ku engineer changes from within. Waapi? Sasa hivi nae anajibu maswali magumu alokuwa anauliza wenziwe akiwa mbunge.

Kwa ufupi amejiunga na wasema uongo!
 
Hata kama Mwakyembe kachokwa Kyela ,wananchi wa Kyela, Rungwe Magharibi na Mashariki hawawezi kuchagua mwanahip-pop....Kwa tulioishi huko tunawajua wale watu. Moja hawana njaa na hii inawafanya wengi wao wawe na kiburi na cha muhimi zaidi wanaheshimu sana shule ya darasani na majina ya Mwa..... Mbeya mjini na Tunduma ni rahisi kupata kwa yoyote kwa kuwa kuna makabira mchanganyiko na wengi wa wapiga kura ni vijana na wafanya biashara. Nafikiri sugu aliongea vile ili kunogesha siasa ila anajua wazi kule hawezi gusa,, Mbombo mbalapala kula!
 
Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, amejibu mapigo ya Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Mr. II, kwamba hana ubavu wa kumng’oa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika 2015 katika jimbo hilo.

Dk. Mwakyembe amesema hayo ikiwa ni siku tano baada ya viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya mkutano katika kijiji cha Njisi Boda Kasumulu ikiwa ni mwendelezo wa operesheni ya chama hicho kuzungumza na wananchi katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya.

Katika mkutano huo Mbunge wa Mbeya Mjini, Mbilinyi, alisema atahakikisha anamung’oa Dk. Mwakyembe katika uchaguzi mkuu wa 2015 kwa sababu ameshindwa kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wakulima wa kokoa katika suala la bei kutokana na kuwa na maslahi na makampuni yanayonunua zao hilo.

Akijibu hoja hiyo, Dk. Mwakyembe alisema Mbilinyi hana ubavu wa kumng’oa mwaka 2015 hata kama atavaa ‘hereni’ masikio yote mawili kwa sababu wananchi wa jimbo la Kyela wanafahamu mambo ya maendeleo aliyowaletea katika kipindi cha miaka mitano ambacho amekuwa mbunge wa jimbo hilo.

“Sugu (Mbunge wa Mbeya Mjini) hawezi kuning’oa ubunge Kyela hata avae heleni masikio yote mawili, kwa sababu wananchi waishio Wilaya ya Kyela wanajua kupambanua, kuchana mistari na kuchochea maendeleo yao,” alisema Dk. Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, alimshauri Mbunge wa Mbeya Mjini kwamba kwa kuwa bado ni mwanasiasa mchanga hivyo aelekeze nguvu zake katika kuwatumikia wananchi wa jimbo lake analoliongoza na siyo kukimbilia katika majimbo ya watu wengine kueneza propaganda ambazo haziwezi kumjenga kisiasa.

Dk. Mwakyembe alisema Mbilinyi kama mwanasiasa mchanga anayechipukia anapaswa kutambua kuwa hawezi akapata umaarufu kisiasa utakaomfanya aendelee kuaminiwa na wananchi wa Mbeya mjini kwa kwenda kwenye majimbo mengine.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Ndiyo utajuwa kuwa hata hao wasomi tunaowategemea kwenye uongozi wa Taifa letu,wengi wao ukiwafuatilia utagundua ni hasara tupu kwa Taifa.Especially wanafiki kama Mwakyembe.Badala ya kujibu hoja,anaanza mudsliding...Eti hata kama akivaa hereni mbili,sasa linahusiana vipi na zao la kakao.Ama weli kusoma si sawa na kuelimika.
 
hatuchagui mbunge kwa sura wala mavazi yake. Hoja ni namna ya kupeleka maendeleo kwa wananchi. Infact tukiwa jimboni tofauti ya PhD na elimu zingine ni ndogo sana kama PhD hizi hazitatui matatizo ya watu. Isitoshe, nadhani kigezo cha ubunge hakijawahi kuwa PhD maana wasokuwa nayo wasingepata ubunge. Let's talk politics na siyo characters binafsi za watu.

Mshtudanganye jamani.Kuna mambo ambayo mtu akiyafanya yanaonyesha wazi kwamba mtu huyo mawazo yake ni duni na hana morals kabisa.That inturn means he can't destinguish between good and evil.This incudes kuvaa vipini and earings.To me mtu kama huyo ni mhuni tu.Kama kweli Sugu anavaa earings na yuko bungeni kweli watanzania tumekwisha, maana sasa bunge limekuwa la wahuni.Call me old fashion,I don't care.Infact nilishangaa Sugu kuingia bungeni.Hii inanipa picha kwamba waliomchagua na jamii nzima ya watanzania nayo ni ya wahuni.Usiniambie kwamba mziki sio uhuni,it depends on what type of music you are talking about.As regards to the usefulness of a Ph.D, sioni haja ya kuongelea,kwa msomi it is obvious.I can't argue on such an obvious thing.Vihiyo ndio walioharibu intergrity ya Ph.Ds.Otherwise genuine Ph.Ds remain useful.
 
Mshtudanganye jamani.KunaMambo ambayo mtu akiyafanya yanaonyesha wazi kwamba mtu huyo mawazo yake ni duni na hana morals kabisa.That inturn means he can't destinguish between good and evil.That incudes kuvaa vipini and earings.To me mtu kama huyo ni mhuni tu.Kama kweli Sugu anavaa earings na yuko bungeni kweli watanzania tumekwisha maana sasa bunge ni la wahuni.Infact nilishangaa Sugu kuingia bungeni.Hii inanipa picha kwamba jamii ya watanzania nayo ni ya wahuni.Usiniambie kwamba mziki sio uhuni,it depends on what type of music you are talking about.
Wewe utakuwa lazima ni extremist.Huna nafasi kwenye jamii ya sasa....No wonder unashangaa...Endelea kushangaa.
 
  1. Ukweli: Sugu kamsema Mwakyembe nyumbani kwake Kyela na akashangiliwa
  2. Ukweli: Wakati anamsema Mwakyembe hakuna Mwanakyela aliyemzomea.
  3. Ukweli: Mwakyembe ni Waziri mdogo baada ya kuteuliwa na Kikwete.
  4. Ukweli: Mwakyembe alimsetiri Kikwete kwenye ripoti yake kuhusu Richmond.
  5. Tetesi: Yawezekana kitendo chake hicho kimemwezesha kuukwaa Uwaziri.
  6. Ukweli: Toka ateuliwe kuwa Waziri amepoa kama maji ya mtungi au ni mnafiki.
  7. Tetesi: Yawezekana huo uwaziri alipewa kwa masharti ya kufunga zipu mdomo.
  8. Ushauri: Badala ya kumjibu Sugu akiwa Dar es Salaam, afanye hivyo akiwa Kyela.
  9. Ushauri: Jema zaidi angeenda na yeye Mbeya akarudishe mapigo huko huko kwa Sugu.
  10. Ukweli: Bashiri Mrindoko wako wizara moja kama Naibu Katibu Mkuu.
  11. Swali: Anajisikiaje anaposhirikiana naye huku alimhusisha na kashfa ya Richmond ?
  12. Swali: Kwa kuwa ameamua kuoga kwenye dimbwi la tope, ni msafi kiasi gani ?
 
  1. Ukweli: Sugu kamsema Mwakyembe nyumbani kwake Kyela na akashangiliwa
  2. Ukweli: Wakati anamsema Mwakyembe hakuna Mwanakyela aliyemzomea.
  3. Ukweli: Mwakyembe ni Waziri mdogo baada ya kuteuliwa na Kikwete.
  4. Ukweli: Mwakyembe alimsetiri Kikwete kwenye ripoti yake kuhusu Richmond.
  5. Tetesi: Yawezekana kitendo chake hicho kimemwezesha kuukwaa Uwaziri.
  6. Ukweli: Toka ateuliwe kuwa Waziri amepoa kama maji ya mtungi au ni mnafiki.
  7. Tetesi: Yawezekana huo uwaziri alipewa kwa masharti ya kufunga zipu mdomo.
  8. Ushauri: Badala ya kumjibu Sugu akiwa Dar es Salaam, afanye hivyo akiwa Kyela.
  9. Ushauri: Jema zaidi angeenda na yeye Mbeya akarudishe mapigo huko huko kwa Sugu.
  10. Ukweli: Bashiri Mrindoko wako wizara moja kama Naibu Katibu Mkuu.
  11. Swali: Anajisikiaje anaposhirikiana naye huku alimhusisha na kashfa ya Richmond ?
  12. Swali: Kwa kuwa ameamua kuoga kwenye dimbwi la tope, ni msafi kiasi gani ?

Nimefurahishwa sana na analyisi yako! Mwakyembe wa sasa si yule wa zamani! Tayari ameshaitwaa damu ya KIFISADI
 
Back
Top Bottom