Dk. Mwakyembe amrushia Sugu kijembe

hatuchagui mbunge kwa sura wala mavazi yake. Hoja ni namna ya kupeleka maendeleo kwa wananchi. Infact tukiwa jimboni tofauti ya PhD na elimu zingine ni ndogo sana kama PhD hizi hazitatui matatizo ya watu. Isitoshe, nadhani kigezo cha ubunge hakijawahi kuwa PhD maana wasokuwa nayo wasingepata ubunge. Let's talk politics na siyo characters binafsi za watu.
 
Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, amejibu mapigo ya Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Mr. II, kwamba hana ubavu wa kumng’oa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika 2015 katika jimbo hilo.

Dk. Mwakyembe amesema hayo ikiwa ni siku tano baada ya viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya mkutano katika kijiji cha Njisi Boda Kasumulu ikiwa ni mwendelezo wa operesheni ya chama hicho kuzungumza na wananchi katika wilaya zote za mkoa wa Mbeya.

Katika mkutano huo Mbunge wa Mbeya Mjini, Mbilinyi, alisema atahakikisha anamung’oa Dk. Mwakyembe katika uchaguzi mkuu wa 2015 kwa sababu ameshindwa kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wakulima wa kokoa katika suala la bei kutokana na kuwa na maslahi na makampuni yanayonunua zao hilo.

Akijibu hoja hiyo, Dk. Mwakyembe alisema Mbilinyi hana ubavu wa kumng’oa mwaka 2015 hata kama atavaa ‘hereni’ masikio yote mawili kwa sababu wananchi wa jimbo la Kyela wanafahamu mambo ya maendeleo aliyowaletea katika kipindi cha miaka mitano ambacho amekuwa mbunge wa jimbo hilo.

“Sugu (Mbunge wa Mbeya Mjini) hawezi kuning’oa ubunge Kyela hata avae heleni masikio yote mawili, kwa sababu wananchi waishio Wilaya ya Kyela wanajua kupambanua, kuchana mistari na kuchochea maendeleo yao,” alisema Dk. Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, alimshauri Mbunge wa Mbeya Mjini kwamba kwa kuwa bado ni mwanasiasa mchanga hivyo aelekeze nguvu zake katika kuwatumikia wananchi wa jimbo lake analoliongoza na siyo kukimbilia katika majimbo ya watu wengine kueneza propaganda ambazo haziwezi kumjenga kisiasa.

Dk. Mwakyembe alisema Mbilinyi kama mwanasiasa mchanga anayechipukia anapaswa kutambua kuwa hawezi akapata umaarufu kisiasa utakaomfanya aendelee kuaminiwa na wananchi wa Mbeya mjini kwa kwenda kwenye majimbo mengine.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Japo kuna utani but there is fair comment. Magamba siipendi lakini Mwakyembe naona yuko tofauti
 
Namuunga mkono Dr Harrison. Joseph hakuwa na sababu kwenda Kyela kuropoka maneno ya kusema atamwangusha ubunge Dr. yeye atulie jimboni kwake Mbeya mjini apige kazi watu waone. so watu wa mjini mbeya wamchukulieje joseph ikiwa next term anategemea kwenda kyela ku contest? hata mwaka mmoja jimboni kwako hujamaliza na chochote cha kuonyesha mkononi unaruka kusema utakwenda mwangusha mwenzio jimboni kwake?what a stupidity!!!!!!!!!!!!
 
Huyo Mbiliyi sio mwanasiasa kwanza ni mwehumwehu tu hana lolote yeye akusanye hizo pesa za pension akipata aendelee na mziki wake.

It shows how your mind works like crazy on the matter of collecting money rather than concetrating on working for development for yourself and your society as well ****** wewe
 
haupo sahihi inamaana tumeshamsahau mwakyembe mda huu,amakweli mfali mbuzi binadamu atakuudhi tu

Mwakyembe hana sababu ya kukumbukwa kwani ameweka ubinafsi na matumbo yake mbele ya mapenzi kwa nchi yake na ndio maana alituficha mambo mengi ambayo alipaswa kutueleza kwenye ripoti yao ya Richmond!! Angekuwa ni ni mtu mwenye msimamo na sio mchumia tumbo hata huo unaibu waziri angeukataa kwani imedhihilika kuwa alipewa kumhadaa tu na ndio maana wale waliopendekezwa na tume yake kufukuzwa kazi ndio kwanza wanapandishwa vyeo na serikali!! Kelele zote zilikuwa ni kutafuta ulaji tu ambao walidhani Lowassa alikuwa anawabania.
 
Kutoka kwenye technical perspective Mbeya walikosea kwa "Sugu" hata akiongea hana objectivity in his approach. I can only wish Mbeya a serious leader in the future.
 
Malafyale ni mmoja ya watu waliompiga sana vita Mwakalinga aka Mtanzania wa JF kabla ya uchaguzi. Pamoja na kuwaeleza maelezo ya uhakika, ila wao bado walilala mstari mmoja kumtetea Mwakyembe. Wengi walimchagua Mwakyembe kwa sababu kadhaa:

1. Kuwakomoa Mafisadi ambao ilisemekana walikuwa wakitaka kumuondoa na kummaliza kisiasa.

2. Kumkomoa Mwakipesile ambaye ilisemekana kuwa alikuwa akimfanyia fitina Mbunge....

3. Kwa sababu wabunge wengi zamani walikuwa kwa miaka 10 , sasa Mwakyembe na kusoma ile ripoti kwa nini wamuondoe?

4. Wengi waliahidiwa vitu kibao na kuna Kibabu kiliweka sahihi hadi makaratasi kuwa kitapata gari ila sasa imekula kwake na kazi wamekifukuza kiaina. Ushahidi wote ulichomwa moto na hakubaki hata na copy............. Mnyakyusa Mjinga kumbe!!!!!

Sasa ona wanavyosema hawa vijana wake wa Tusk Force wa Jamiiforums kwa sasa:





Hebu soma walioshangilia ushindi wa Mwakyembe mwaka jana na leo wanasema nini? Nyambala bado upo? Bado wachekacheka kama mwaka jana? Hahahaaaaa :)

https://www.jamiiforums.com/tanzania-2010-2015/68676-kyela-elections-2.html


Nimeclick hiyo link, Dah humu JF kuna watu ni double standard na wanafiki vibaya! Kha!
 
Hakika Mwakyembe hafai tena kuwakilisha wana-Kyela.

Huyu alitumia mamilioni ya kodi yetu kwenye kamati yake ya richmond, akaja na maazimio lukuki, lakini yote serikali ikayapuuza na kuyatupilia mbali. Serikali hiyohiyo iliyoponda kazi ya kamati yake ikamhonga uanibu waziri naye akakenua meno. Angekuwa mkweli ndani ya nafsi yake angekataa uteuzi ule uanomfanya awe sehemu ya hii irresponsible govt.

Fisadi sawa na anaowatuhumu ufisadi.

AMA KWELI JF HAKUNA HOJA TENA ILA HAJA, TENA HAJA KUBWA! Huyu mpiga mziki ameingia jimbo la mwenzake na kumshambulia kwa wapigakura wake. Sisi, kwa ushabiki wetu wa kisiasa tunamlaumu Dk. Mwakyembe kwa kumfunda kijana huyu ambaye inaelekea hata Kanuni za Bunge hazijui za Wabunge kuheshimiana ndani na nje ya Bunge! Tunataka Dk. Mwakyembe aseme "Yoo, that wat was good man, Yoo!" Hapana, tusiwe vichekesho pamoja na freedom of expression tuliyonayo! Mwakyembe kampaka Sugu kisawasawa, asirudie tena kwani Sugu anamhitaji Dk. Mwakyembe jimboni kwake kumwongezea barabara moja au mbili! Kama kuna watu ambao wanajali utaifa kwanza na si vyama, ni Dk. Mwakyembe na Dk. Magufuli. SUGU, HII COMNBINATION NI MBAYA, USIICHOKOZE BILA SABABU. NANI kakudanganya kuwa Kyela wanasikiliza Bongo Flava zaidi ya ngoma zao? Nani kakudanganya kuwa Kyela wanahusudu zaidi mistari kuliko elimu?
 
Usionge ki2 usicho kijua, mbeya tumefanya right choice. Tunamwamin sugu,
Huyo mwakyembe wenu aache kutudharisha watu wa mbeya "kwani mwakyembe ni nani katika mbeya?"
hata elimu yake imeshindwa kumfanya aonge maneno ya Busara, ashindwe tena
hawezi kabisa kutufananisha na watu wa kyela. Mbeya kuna demokrasia.
Mwakyembe usilopoke tulia jibu kwa makini, busara na kwa kisomi usiwe kama watu walio ishia chekechea.
 
Mimi nikishamuona mwanaume mwenzangu anavaa hereni sikioni basi huwa namfananisha na Elton John yule mwanamuziki wa UK
 
Kumbe Sugu ana vaa heleni sikioni! Mmmmmh hii ni aibu kwa watu wa mbeya mjini! Mbunge ana vaa heleni!
What is hereni......??? Kama ingekuwa ni issue basi wangemfanyia kama wale wa CUF waliowapa VIMADA pass za kusafiria............. Au wangemtimua kama Amina Chifupa alivyotinga na mavazi ya kiaina
 
Mwakyembe anatakiwa aende Kyela,alikozomewa na kumwekea mawe ktk njia ili aendelee na mkutano,mambo hayo yalifanyika kama Sugu hajafika kyl.Yeye aende kyela ndio akaongee hayo
 
Usionge ki2 usicho kijua, mbeya tumefanya right choice. Tunamwamin sugu,
Huyo mwakyembe wenu aache kutudharisha watu wa mbeya "kwani mwakyembe ni nani katika mbeya?"
hata elimu yake imeshindwa kumfanya aonge maneno ya Busara, ashindwe tena
hawezi kabisa kutufananisha na watu wa kyela. Mbeya kuna demokrasia.
Mwakyembe usilopoke tulia jibu kwa makini, busara na kwa kisomi usiwe kama watu walio ishia chekechea.

Unaweza ukatueleza ni kitu ganu alichofanya Sugu mpaka sasa kinakachoweza kuwafanya wanaMbeya waone uamuzi walioufanya kumchagua ulikuwa uamuzi sahihi?
 
Dk. Mwakyembe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, alimshauri Mbunge wa Mbeya Mjini kwamba kwa kuwa bado ni mwanasiasa mchanga hivyo aelekeze nguvu zake katika kuwatumikia wananchi wa jimbo lake analoliongoza na siyo kukimbilia katika majimbo ya watu wengine kueneza propaganda ambazo haziwezi kumjenga kisiasa.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Heh! Kumbe Watu wana Majimbo yao! Sijui nani amewauzia mpaka kuyaita ya kwao! Au wameshagawana, na sie wengine tuonataka kuwa viongozi itabidi tutengeneze majimbo yetu!

Au nani aliyemwambia Mwakyembe kwamba Kyela ni Jimbo aliloumbiwa yeye! Inashangaza. Ndio Wasomi wetu hao!
 
Hivi kumbe mtu akivaa heleni anakua na upeo mkubwa wa utendaji?maana sijaelewa kwa nini mwakyembe ametoa kauli kama hiyo.
 
sugu ni mtu wa mademu na bangi bana asikwambie mtu kitu..2015 ubunge atauskia tu kwani amepata kibahati bahati ttuu..
 
Back
Top Bottom