Dkt. Mwakyembe aandika waraka wa siri!

ukitaka kugombea uongozi ccm sasa hivi ni lazima uhakikishe kwamba kila unapotoka nyumbani umekunywa kichupa kimoja cha anti-dot, dawa ya kuzuia sumu mwilini. magamba mpo juu!
 
Kama kweli Dr. Mwakyembe amelishwa sumu na mtu ama kikundi cha watu kwa sababu za kisiasa ama nyingine wanazozijua wao, na kama Dr. atakufa kwa sababu hiyo ama nyingine kwani kifo kipo na tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye pekee anayepanga ni mauti ya aina gani yatamkuta binadamu na kwa wakati gani, waliofanya jambo hilo dhambi hiyo itawarudia na iwe iwavyo itawarudia na kwa njia hiyo hiyo itawaangamiza wao na vizazi vyao.


Mwenyezi Mungu amjalie Harrison Mwakyembe apate kupona kwa maradhi yanayomsumbua na awajalie ndugu, jamaa, marafiki na familia yake kwa ujumla moyo wa imani na nguvu ya kukabiliana na kipindi kigumu kinachowakabili kwa sasa.
 
Dr. Mwakyembe ameandika waraka ya kuhisi kwamba kawekewa sumu na kuwahisi baadhi ya watu kwamba ndiyo wanahusika kumwekea sumu. Waraka wa kuhisi ni mpaka ushahidi kamili upatikane vinginevyo haitasaidia kitu hapo. Namshauri awaombe watendaji wa serikali ambao wapo upande wake wamsaidie kupata ukweli wa mambo kwasababu inaonekana kwa asilimia kubwa hapati support ya kiupelelezi. Ila aishukuru serikali na wananchi kwa kumpatia matibabu ya gharama kubwa kwa kutumia fedha za walipa kodi.
 
Mbona kama vile sioni kipya, tanzania daima vipi?


Mbinu zote mnazijua, mipango yote mnaijua, walengwa wote mnawajua, mliowapanga kufanya ufilauni huo mnawajua, Jipya utaliona wapi labda baada ku-meet objectives mnazokusudia!
 
Amwagaye damu isiyo na hatia hawezi kubaki salama. Damu ya mtu inaongea na inadai kisasi (refer case ya Abel na Kaini). Sema wafanyao mauaji kama haya wengi hawawezi kelewa ninachosema hapa maana walishamuasi Mungu na kufanya ushirika na Ibilisi.
 
Mwakyembe atatapatapa maisha yake kujaribu kujikosha dhambi aliyowafanyia Watanzania kwa kuzua na kufikia kuwawacha kiza kwa taarifa yake ya majungu kufikia kuzimwa mitambo ambayo imesababisha janga na madhara makubwa sana kwa taifa, mbali ya vifo, na sasa mitambo hiyo hiyo imewashwa tena na inatumika na yeye na wengine wako kimya. Jee, sumu ndio imewafanya wakae kimya?

Nnasema hivi, Mwakyembe hafi upesi, atakufa na huku anateseka kwa kupukutika mwili kidogo kidogo, kama tusikiavyo. Hayo ndio malipo ya dhulma hapa duniani. Na hii ni kwa wote waliokuwa wanamuunga mkono huku wanajuwa kuwa alikuwa na maslahi binafsi.
 
Nimekua nikimini na kusikitika sana juu ya Bwana mkubwa wetu nikiamini kalishwa sumu,lakini nimebaini from a reliable source kua sivyo kama sisi tunavyofikiri.Dr wa Appolo(jina kapuni) Ambaye huwa anashugulikia A/c za madeni kwa matibabu za wakuu wetu wanapokwenda kutibiwa Appolo alitukata duku duku letu nikiwA na waziri(jina kpuni) baada ya kummuliza ni nini hasa kinachomsumbua mkuu wetu maana mneno yamekua ni mengi mtaani.

Jibu alilotupa lilikua ni moja,kua huyu jamaa yetu anatafuta pakulalama tuu ila ukweli wa mambo ni AMEUNGUA/NGWENGWE.NimeshAngaa kusikia hivyo na I had to take back my words kwasababu nilimchukia sana Manumba kwa kauli yake na nikamuita MKATILI nikidhani anakwepesha ukweli wa mambo kwa kusema ugonjwa wake hAuusini na sumu.Kumbe alikua alikua anajua alisemalo.

Tumekua na wazo moja tuu la sumu,lakini hatukuwa tunafikiria upande mwingine wa shilingi.Mkuu wetu si ana file lake la Appolo,kwanini haliweki wazi?anaacha wtu walumbane tuu wakati ni kitu kidogo sana cha kuweka file wazi.MtAkuja amini ivi karibuni,time will tell.Hili ni dokezo tuu
 
kuna kitu DR. Mwakyembe anaogopa kukiweka wazi sijui kuendelea kufanya hivyo kuna msaidia nini ingali anatekekea kwa sumu
 
[
akiwa ofisini kwake huku akitaja majina ya watu anaowatuhumu kuwa nyuma ya mpango huo ambao gazeti hili kwa sasa linahifadhi majina yao.
[/QUOTE]
mnasubiri a'dead ndio mtaje majina ya wahusika?
 
Data hizi zinaelekea kutoa jibu, tuvute subira. Mpaka hapo sumu kawekewa na mahali ni ofisini kwake. Na nani subiri watatajwa tu. Lakini pia wananchi hakuna asiyejua kuwa Dr. Mwakyembe aliripoti matukio yote polisi na kila mara alipuuzwa kwa kuwa hawapi kitu kidogo na mafisadi walihudumiwa kwa upendeleo kwani ndio wanawalipa polisi mishahara mikubwa kuliko ile wanayopewa na serikali. Ndiyo maana hali iko hivi.
 
UKWELI utajulikana lakini si vizuri tukaanza kutoa tuhuma kwa vitu tusivyo na uhakika, mwakyembe ni mgonjwa uenda hali hiyo ndo inamfanya atoe shutuma zisizo na UKWELI. Mungu ndo anajua sina iman sana na viongozi wa CCM, wanatafuta umaruhufu tu.

wewe una uhakika gani kuwa shutuma anazotoa mwakyembe hazina ukweli?

unataka tusimuamini mwakyembe ila tukiamini wewe?
 
Pole sana ujui usemalo, Tatizo la ugonjwa alionao mwakiembe linagusa public interest na limegubikwa na mazingira tata hivyo kwa nchi makini inayojali na kulinda watu waake na kuwathamini

haiwezi ikawa bubu kiasi hicho lazima ingetoa tamko na uchunguzi wa kina wa jopo la madaktari na vyoma vya usalama kushirkiana ili kulinda mstakabali wa raia wake, Ikiwa hayo alifanyiwa kiongozi katitaka serekali namna gani raia wa kawaida? huoni kua hali hii ikiachiwa athari zake ni kubwa kwa amani ya nchi na watu wake?

Huoni ikiwa kunawatu wamefikia hatua kunyweshana sumu hakuna tofauti na mtandao wa kigaidi ambao kwa nchi makini laziama upelelezi wakiaitelejensia ungefanyika?

Tukiacha ushabiki hili si jambo dogo hata kidogo hebu jiweke katika position ya Mwaikiembe then uone kama ni wewe ungefanya nini na serekali yako inayopaswa kulinda raia wake ndiyo hiyo tena haina msaada na wewe inakutumia kama kondom then hainampango na wewe eti kwa jibu rais tunahifadhi siri ya mgonjwa ****** mtupu.

Unapozungumzia serikali makini, Tanzania haimo kabisa!! Ndo maana viongozi wake wengine wameamua kuita kuwa ni serikali yenye siasa uchwara mfano wa maji taka.!!!
 
MKuu Invisible, hebu tumiminie report yenyewe kabla zege halijawa kaukau!!! Please do it now!!! Common man!!!!!
 
I AM NOT SURE IF THIS IS THE NOTE U NEED BUT IT HAS SOMETHING IMPORTANT.

Taarifa kamili ya Dk. Mwakyembe hii hapa:
“Nimelazimika leo Jumamosi, tarehe 18 Februari, 2012 kutoa taarifa hii kwa vyombo vya habari kufuatia mkutano wa DCI Robert Manumba na waandishi wa habari jana (17/02/12) kuongelea, pamoja na mambo mengine, hali yangu ya afya na kuhitimisha, kienyejienyeji tu kuwa “sikunyweshwa sumu” ila naumwa tu ugonjwa wa ngozi bila kufafanua ugonjwa huo wa ngozi umesababishwa na nini!
“Napenda nisisitize mapema kabisa kuwa msimamo huo wa Jeshi la Polisi umenikera sana katika hali niliyonayo ya ugonjwa, kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake unaoendelea hospitali ya Apollo nchini India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu; pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa “sikunyweshwa sumu” wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu;
“Na tatu kwa Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.
“Itakumbukwa kuwa tarehe 9 Februari, 2011 nilimwandikia barua IGP Said Mwema kumtaarifu kuhusu njama za kuondoa maisha yangu na ya viongozi wengine. Kwa kutambua kuwa Jeshi la Polisi la Tanzania daima husisitiza kuletewa ushahidi kwanza ndipo lifanyekazi, nilihakikisha nimeainisha katika barua hiyo kila ushahidi nilioupata au kupewa.
“(Utaratibu huu wa Jeshi la Polisi kusubiri kuletewa ushahidi mezani, kama ambavyo mahakimu wanavyosubiri ushahidi mahakamani, haupo popote pale duniani (ila Tanzania tu) kwani kazi ya msingi ya Polisi si kuletewa, ni kutafuta ushahidi. Polisi wanachohitaji duniani kote ni kupata clue au tetesi tu.
“Hiyo inatosha kufukua ushahidi wote unaohitajika). Pamoja na kujitahidi kuanika kila aina ya ushahidi niliokuwa nao, mambo manne yalijitokeza ambayo yalionyesha wazi kuwa Polisi hawakuwa na dhamira ya dhati ya kupeleleza suala hilo:
(i) Siku chache baada ya kumkabidhi IGP barua hiyo, nilitumiwa timu ya “wapelelezi” ofisini kwangu kuja kuchukua maelezo yangu ya ziada. Timu hiyo ilikuwa inaongozwa na ACP Mkumbo, afisa wa polisi ambaye wiki chache zilizokuwa zimepita alikuwa miongoni mwa askari waliotuhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kumbambikizia madawa ya kulevya mtoto wa Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, suala ambalo mpaka leo hii uongozi wa Polisi umeshindwa kulitolea maelezo ya kuridhisha. Kwa msingi huo, nilikuwa nimeletewa mtuhumiwa wa rushwa/ ujambazi kuendesha uchunguzi wa watuhumiwa wengine wa ujambazi! Nikatambua mara moja kuwa zoezi zima lilikuwa la mzaha, tena mzaha mkubwa!
(ii) Wiki chache baada ya barua yangu kuwasilishwa kwa IGP na timu ya ACP Mkumbo “kuanza kazi”, Jeshi la Polisi likachukua hatua ya kuwapongeza na kuwazawadia askari niliowatuhumu kushirikiana na majambazi! Huhitaji kuwa profesa wa falsafa kuelewa kuwa huo ulikuwa ujumbe tosha wa kunipuuza.
(iii) Hivi karibuni tuhuma za askari polisi kujihusisha na vitendo vya ujambazi mkoani Morogoro zilipopamba moto na kuwagusa askari “wale wale” niliowatuhumu kwenye barua yangu, IGP alichukua hatua ya kuwahamishia mikoa mingine!
(iv) ili kunikatisha tamaa kabisa, barua yangu ya “siri” kwa IGP ikavujishwa kwa makusudi kwenye vyombo vya habari na kuchapishwa kama habari ambayo ilikebehi na kukanusha taarifa nzima niliyotoa, sijui kwa faida ya nani! Lakini huu ni mchezo wa kawaida kwa polisi kwani hivi karibuni Mhe. Waziri Samuel Sitta alipohojiwa na ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi ofisini kwake, wakiwa wawili tu, taarifa ya kikao hicho ikawa magazetini ikikebehi ushahidi aliotoa Sitta! The integrity of the police force leadership is on the line.
Nimeelezea vizuri katika barua yangu kwa IGP kuwa kundi hilo la mauaji lilikuwa limeelekezwa kuniua kwa kutumia sumu, taarifa ambayo kwa karibu mwaka mzima Polisi hawakutaka kuifuatilia kwa sababu wanazozijua wenyewe. Sasa huu msukumo mpya wa Jeshi la Polisi kutaka kujua kama nilipewa sumu au la na kukurupuka kutoa tamko hata kabla ya kunichunguza nilivyo, kunihoji mimi na wasaidizi wangu ofisini na hata kuongea na mabingwa wa Kihindi wanaonifanyia uchunguzi, umetokea wapi?
Aidha napata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matatibabu yangu au walisoma taarifa “nyingine”, na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au “walisomewa”! Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa wandishi wa habari hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukidhibiti/ kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi na bila aibu: “hakulishwa sumu”, “hakulishwa sumu”!
Nimesoma darasa moja Kitivo cha Sheria Mlimani na DCI Manumba. Baadaye IGP Mwema alikuwa mwanafunzi wangu wa sheria Mlimani. Vigogo hawa wawili wa usalama wa raia nchini hawajanitendea haki, nao wanajua. Wanajua vilevile kuwa sitakaa kimya au kumung’unya maneno come what may pale ambapo haki inakanyagwa.
Tuendelee kuombeana afya na uhai ili kutendeane haki na vilevile tuitendee nchi yetu haki kwa kuvimalizia viporo vinavyokera vya Dowans, EPA, Kagoda n.k. kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
Mungu Ibariki Tanzania.
 
nimekua nikimini na kusikitika sana juu ya bwana mkubwa wetu nikiamini kalishwa sumu,lakini nimebaini from a reliable source kua sivyo kama sisi tunavyofikiri.dr wa appolo(jina kapuni) ambaye huwa anashugulikia a/c za madeni kwa matibabu za wakuu wetu wanapokwenda kutibiwa appolo alitukata duku duku letu nikiwa na waziri(jina kpuni) baada ya kummuliza ni nini hasa kinachomsumbua mkuu wetu maana mneno yamekua ni mengi mtaani.

Jibu alilotupa lilikua ni moja,kua huyu jamaa yetu anatafuta pakulalama tuu ila ukweli wa mambo ni ameungua/ngwengwe.nimeshangaa kusikia hivyo na i had to take back my words kwasababu nilimchukia sana manumba kwa kauli yake na nikamuita mkatili nikidhani anakwepesha ukweli wa mambo kwa kusema ugonjwa wake hauusini na sumu.kumbe alikua alikua anajua alisemalo.

Tumekua na wazo moja tuu la sumu,lakini hatukuwa tunafikiria upande mwingine wa shilingi.mkuu wetu si ana file lake la appolo,kwanini haliweki wazi?anaacha wtu walumbane tuu wakati ni kitu kidogo sana cha kuweka file wazi.mtakuja amini ivi karibuni,time will tell.hili ni dokezo tuu

kijana kuwa makini unapopost vitu vya kipuuzi kwenye mijadala makini! What is kuungua/ngwengwe?
Huu ni ******!
 
Back
Top Bottom