nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
• Apongeza maandamano ya CHADEMA
Na Helena Denis
MKURUGENZI mstaafu wa Usalama wa Taifa, Dk. Hassy Kitine, amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimechafuka na yeyote anayeingia madarakani anawaza kujitafutia fedha.
Amesema chama hicho kimechafuka zaidi hivi sasa kwa kuwa watendaji wake walivunja Azimio la Arusha na maadili ya uongozi.
Dk. Kitine, ambaye amepata kuwa Mbunge wa Makete, alitoa kauli hiyo jana wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Bahati Nasibu ya ‘Nina Ndoto', iliyoandaliwa na Kampuni ya Faidika inayojihusisha na utoaji wa mikopo.
Dk. Kitine alisema kuwa kutokana na uchafu huo, CCM imeamua kujivua gamba ili kujisafisha sehemu zote ilizokuwa imekosea.
"Walijiruhusu kwa muda mrefu kukaa na uchafu mpaka wameamua kujisafisha. Nani aliyewaweka uchafu kama si wao wenyewe?" alihoji Dk. Kitine.
Kitine alisema kuwa kuvunjwa kwa Azimio la Arusha, ambalo ndilo lililokuwa likiweka misingi mizuri ya viongozi wa umma, ndiko kumewafanya makada wa CCM kufanya mambo kwa utashi binafsi.
Alisema jambo kubwa lililopaswa kufanywa na makada wa CCM ambao ndio wenye kuiongoza serikali ni kujali zaidi masilahi ya wananchi pamoja na kuzingatia miiko ya kazi yao.
Hata hivyo aliisifia hatua hiyo kwamba ina lengo la kujisafisha na kusisitiza kwamba chama hicho kinapaswa sasa kuonyesha kwa vitendo kuwa kimejivua gamba.
Alisema yeye anapenda kusema ukweli kutokana na nafasi yake kwenye jamii, kwani alishalitumikia taifa katika ngazi tofauti kabla ya kustaafu.
"Mimi mara nyingi napenda kusema ukweli, lakini ninaposema ukweli viongozi wanachukia," alisema Dk. Kitine.
Akitolea mfano wa harakati za kuwania uongozi, Dk. Kitine alisema kwa hali ilivyo sasa watu wanataka uongozi ili wapate fedha badala ya kujali masilahi ya taifa.
Dk. Kitine alisema hali hiyo imetokana na kuvunjwa kwa Azimio la Arusha lililoweka maadili ya viongozi wa umma.
Kuhusu maandamano yanayofanywa sehemu mbalimbali na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambayo yamekuwa yakibezwa na CCM, Dk. Kitine alisema hauoni ubaya wake hasa kama yanalenga kuelimisha umma.
"Kama maandamano hayo ni ya maendeleo na yamelenga katika kuwasaidia Watanzania kuamka ili kujiletea maendeleo, sioni ubaya," alisema.
Akizungumzia hali ya uchumi nchini, Dk. Kitine alisema Watanzania chini ya asilimia moja ndio wanaomiliki asimilia 99 ya uchumi.
" Hali hii inatokana na kudharau miradi kama ya ‘Faidika' yenye lengo la kuwawezesha kumiliki uchumi nchini lakini kwa hali ilivyo sasa, wachache ndio wanaomiliki asilimia kubwa ya uchumi wa taifa hili, jambo ambalo ni hatari," alisema.
Akitangaza majina ya washindi wa shindano la ‘Nina Ndoto', Dk. Kitine alimtangaza mwalimu wa Manispaa ya Shinyanga, Sofia Simba, aliyeshinda sh milioni moja, Amir Othman (sh milioni tano), Makono Andrew (sh milioni tatu), Martin Lalika (sh milioni mbili) na Ferdinanda Lameck (sh milioni moja).
Dk. Kitine alisema lengo la ‘Faidika' ni kuwawezesha Watanzania kumiliki uchumi kwani hivi sasa taasisi hiyo ina matawi katika kila wilaya nchini.