Dk john magufuli: Rais wa tanganyika mwaka 2015

Status
Not open for further replies.

ZIPOMPAPOMPA

Member
Nov 29, 2010
50
10
Nimejaribu kuchunguza upepo wa kisiasa tanzania na kusoma nyakati then nimegundua mambo yafuatayo:

Kuna uwezekano mkubwa kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hautafanyika kukiwa na tanzania kutokana na sababu nyingi moja kubwa ni kwamba kwa sasa zanzibar, inajitangaza kama nchi, na inaonekana wapo kwenye mchakato mkubwa wa kujitoa kwenye muungano, na kutaka kama ni masuala ya muungano, basi tuunganishwe na jumuiya ya afrika mashariki, kwa namna hiyo kama watafanikiwa, hakutakuwa tena na uchaguzi wa raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania.

Iwapo suala la muungano litakuwa ndoto, kuna uwezekano mkubwa wa chama cha mapinduzi kuvunjwa, kwa sababu ccm ni matokeo ya kuunganishwa kwa tanu na asp.

Kama hilo litatokea, viongozi wa ccm wa tanzania bara, wataanzisha chama kingine, na watajitokeza watu weeengi kuomba kugombea nafasi ya urais.

Mgombea atakayepitishwa ni dk. John pombe magufuli.

Kwa kuwa ccm ina sera ya kuwa-empower wanawake, hiyo ccm mpya nayo itafuata hayo hayo na hatimaye watamsimamisha prof. Anna tibaijuka, kama mgombea mwenza.

Kwa kuwa kutakuwa na mgogoro mkubwa katika chama cha chadema, juu ya nani agombee uraisi, suala hili litapekeka ushindi kwa ccm mpya. Wakati huo chama cha cuf kitaonekana kufa kabisa kwa kuwa nguvu yake ipo zanzibar.

Hayo ni maono wakuu, mwenye lake aseme.
 
..sina imani naye kutokana na ushiriki wake ktk kashfa ya kuuza nyumba za serikali.

..sasa hivi mnaona Spika Makinda naye inabidi ajengewe nyumba mpya. nina wasiwasi kwamba huenda nyumba ya Spika ilishaibiwa na Pius Msekwa kwa kushirikiana na John Magufuli.

..tena nadiriki kusema Nalaila Kiula was better than Magufuli. hasara aliyotutia ni ndogo zaidi ya hii tunayoendelea kuingia kutokana na uozo wa Pombe Magufuli.
 
Anafaa kwasababu anauza kwa kasi na anajenga kwa kasi..

Then kila mfanyakazi atakuwa na nyumba yake au siyo?
 
..sina imani naye kutokana na ushiriki wake ktk kashfa ya kuuza nyumba za serikali.

..sasa hivi mnaona Spika Makinda naye inabidi ajengewe nyumba mpya. nina wasiwasi kwamba huenda nyumba ya Spika ilishaibiwa na Pius Msekwa kwa kushirikiana na John Magufuli.

..tena nadiriki kusema Nalaila Kiula was better than Magufuli. hasara aliyotutia ni ndogo zaidi ya hii tunayoendelea kuingia kutokana na uozo wa Pombe Magufuli.

Miye pia sina imani naye kutokana na kuwa mshiriki mkubwa katika uuzaji wa nyumba za Serikali kwa bei ya kutupa ambao umeigharimu serikali zaidi ya shilingi bilioni 200. Sijamsikia hata siku moja akikemea ufisadi mbali mbali uliofanywa na mafisadi mbali mbali waliokuwemo katika awamu ya pili, ya tatu na ya nne na hadi hivi sasa katika hili sakata la Richmond/Dowans yuko kimya kabisa kama hajawahi kulisikia.

Kwa maoni yangu hafai kabisa pamoja na watu wengi kujaribu kumpigia debe kwamba ni mtendaji mzuri ambao hadi sasa mimi sijauona. Pia aliitia hasara Serikali ya zaidi ya shilingi milioni 200 katika lile sakata la samaki waliokamatwa kwa wavuvi ambao walikuwa hawana kibali cha kuvua nchi.

Yeye sio mtendaji; Mtendaji ni Katibu Mkuu wa Wizara, yeye ni Mwana-siasa ambao upewa kazi ya kuwakilisha Serikali kubishana na Wabunge wanaotetea wananchi kwa Maslahi ama ya Serikali au ya wana-siasa wenzeke wachache kama watakavyo kubaliana katika kikao chao ambacho uitwa Baraza la Mawaziri; kiukweli hawana kazi yoyote zaidi ya kuvuruga na kuiba, huyu Magufuri nadhani wanaopigia kampeni humu waache maana humu kunawaelewa na wachambuzi wajaribu vijijini anazidiwa mara 2000 na Anna Kilango, Mara 5000 na naibu wake hata sijui hawa jamaa wanatumia vigezo gani kumpa Dr. Mwakiembe awe msaidizi wa huyu Bwana Mchafu au wanataka kumchafua awe macho sana
 
Magufuli wa kubenea....hahah no way!! Hata mkijaribu kutumia waandishi wa habari kumpigia debe...hafai. Uchafu wake tunaujua...
 
Miye pia sina imani naye kutokana na kuwa mshiriki mkubwa katika uuzaji wa nyumba za Serikali kwa bei ya kutupa ambao umeigharimu serikali zaidi ya shilingi bilioni 200. Sijamsikia hata siku moja akikemea ufisadi mbali mbali uliofanywa na mafisadi mbali mbali waliokuwemo katika awamu ya pili, ya tatu na ya nne na hadi hivi sasa katika hili sakata la Richmond/Dowans yuko kimya kabisa kama hajawahi kulisikia.

Kwa maoni yangu hafai kabisa pamoja na watu wengi kujaribu kumpigia debe kwamba ni mtendaji mzuri ambao hadi sasa mimi sijauona. Pia aliitia hasara Serikali ya zaidi ya shilingi milioni 200 katika lile sakata la samaki waliokamatwa kwa wavuvi ambao walikuwa hawana kibali cha kuvua nchi.

Hata sijakuelewa.
 
anafaa sana kweny uwaziri, hata uwaziri mkuu, lakini sio Uraisi, ana element ya kutumwatumwa, na anhitaji mtu safi sana kumsimamia. Kwa kweli ni waziri wa mfano
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom