Dkt. Gharib Bilal Makamu wa Rais kwanini hasikiki sana au si maarufu sana kwenye vyombo vya habari?

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,378
3,825
Kwanini Makamu wa rais Dk Gharib Bilal hasikiki sana au si maarufu sana kwenye vyombo vya habari?

Nilifanya kama kautafiti fulani au kama kautani hivi nikauliza watu wapata 10 au zaidi randomly "hivi makamu wa raisi ni nani?"

ni watu wanne tu waliweza kujibu kwa haraka kwa usahihi mmoja alipatia baada ya kufikiri kidogo. wote waliweza kuwataja Mheshimiwa spika na Waziri mkuu bila kusita

Je, hii ni ishara kuwa vyeo vingi katika ngazi ya taifa viangaliwe upya?
 
Jacksonmichael umeniambia kitu kumbe Bilal ni mchapa kazi na si muuza sura eh
 
Ungewauliza mkata UTEPE maarufu tangu dunia iumbwe ni nani?
Hapo wangeweza kukujbu
 
Dr Bilali siasa si fani yake. Ameng'ang'ania tuu kwakweli. Angebaki kwenye taauluma yake

angekuwa amefanya mengi significantly. Sasa ameishia kuwa anafanya shughuli za uzinduzi tuu.

Sijawahi kumsikia akiaddress any serious issue kwakweli. Ila kama ulaji amepata, kwanini apige

kelele? Si ndo utaratibu wa Tanzania? Au wakina Kombani, Simba unawasikia?
 
Bilal ana kazi mbili kama makamu wa rais kukata utepe na kufungua mikutano baaaaaaaaaaasi top
 
Mie sijawahi kumsikia katika shughuli yoyote zaidi ya kufungua vitu huko mikoani, amekuwa mtembea mikoa na bosi wake mtembelea nchi za watu. Kama anafanya engine basi labda sijaona.

Ila duh yeye na mkasi kukata ma riboni kumekucha.

Ila raisi angemfagilia kidogo basi ampe safari ya kwenda nchi za nje mara nyingi nae afanye shopping ale raha.
 
Thank u all sasa napata kujua kuwa cheo ni dhamana lazima kiongozi afanye kitu katika jamii kuwasogeza kutoka hapo walipo kwenda mbele zaidi potelea mbali hata kwa kukosea! itakuwaje wewe mtu uwe wa sherehe tu wakati wote? maana kuna watu hawana vyeo serikalini tena ni vijana tu lakini wananchi wanawaona wanawafahamu... wanawa-admire
 
Sioni kazi ya Dr.Bilal.Kuna haja ya kuangalia upya umuhimu wa kuwa na makamu wa rais kwenye katiba mpya.Kwa sasa hana mashiko ya kiutendaji.Kazi ya kukata utepe hata balozi wa nyumba kumi anaweza kufanya.
 
makamu wa rais kazi yake ni kukaa standby rais akifariki achkue nchi, kama vile spare Tyre haina kazi imekaa tu lakini lazima iweko kazini, kwa maana hii VP = spare tyre.
 
hata yule makamu wa pili wa rais aliyemtangulia tulikua hatumsikii...tumekuja kumsikia baada ya kua Rais wa zenj... naonaga makamu wa rais anachaguliwa mtu ambae si mkorofi na ambaye ni weak..kwamba hawezi kufanya kazi akaonekana ni mchapa kazi kuliko rais mwenyewe...
 
Kwa nini Makamu wa rais Dk Gharib Bilal hasikiki sana au si maarufu sana kwenye vyombo vya habari?
Nilifanya kama kautafiti fulani au kama kautani hivi nikauliza watu wapata 10 au zaidi randomly "hivi makamu wa raisi ni nani?"
ni watu wanne tu waliweza kujibu kwa haraka kwa usahihi mmoja alipatia baada ya kufikiri kidogo. wote waliweza kuwataja Mheshimiwa spika na Waziri mkuu bila kusita
je, hii ni ishara kuwa vyeo vingi katika ngazi ya taifa viangaliwe upya?

Makamu wa Rais yuko kwenye media kila siku maana ana ziara nyingi (na ndefu) mikoani ambapo ni mzinduzi wa majengo na miradi mbalimbali.

Sikubaliani nawe kuwa hafahamiki!
 
Mie sijaelewa mantiki ya hii thread.

Kama kazi anazo, ikiwemo ya kukaimu nafasi ya rais asipokuwapo rais.

Pia; endapo rais atalazimika kuachia ngazi kabla ya mandate yake kuisha kwa sababu yeyote ile, makamu wa rais atakamata urais hadi muda wao umalize
 
Kwa nini Makamu wa rais Dk Gharib Bilal hasikiki sana au si maarufu sana kwenye vyombo vya habari?
Nilifanya kama kautafiti fulani au kama kautani hivi nikauliza watu wapata 10 au zaidi randomly "hivi makamu wa raisi ni nani?"
ni watu wanne tu waliweza kujibu kwa haraka kwa usahihi mmoja alipatia baada ya kufikiri kidogo. wote waliweza kuwataja Mheshimiwa spika na Waziri mkuu bila kusita
je, hii ni ishara kuwa vyeo vingi katika ngazi ya taifa viangaliwe upya?

Nilitegemea ungekuja na thread ya kutaka kujua nafasi ya Makamu wa Rais katika Katiba mpya lakini kwa kujifanya umefanya utafiti wa kuwa Makamu aliyepo anafahamika amamla umeenda choo cha nje, maana umeanza kwa kumtaja jina hali inayoonyesha kuwa unamfahamu na hawa unaotaka wamjadili wanamfahamu. Kumbuka pia kuwa uongozi sio kupiga makelele na kupaza sauti katika media ama kusaka umaarufu usio na tija, nakushauri soma Katiba na kisha achana na tabia ya kuweka thread kwa nia ya kuongeza posts. Jumapili njema
 
Bwana Bonny Makene hayo ni mawazo yako na wengine wametoa mawazo yao. Nami nililenga hukohuko kwenye katiba kwa sababu kila cheo au nafasi katika uongozi wa taifa ni gharama na ni lazima iwe productive. wazo kwamba tunamweka mtu ili akifa mwingine yeye arithi lakini huku nyuma alikuwa akpokea masurufu na mishahara wewe walionaje? suala la ratiba ya si hoja sana kwani ratiba na tija ni kitu kilekile? labda ungenieleza ya kuwa nchi bila makamu itakuwa vigumu. huku katika JF kuna Great thinkers wanaoweza kutoa mchango mzuri sana katika mstakabali wa taifa letu. sina nia ya kuongeza tu posts mimi husoma mawazo ya wana JF na kutafakari zaidi sehemu kubwa najifunza zaidi haya mawazo makuu ya wana forum. kuwa makamu wa rais bila kufahamika wewe unachukulia lightly jaribu kutafakari kidogo. kujulikana kwa kiomgozi mantiki yake ni yale anayoyafanya si sura yake. watu wanaijua sana ligi ya England kutokana na nini? hawijui ligi yaIindia kwa nini? hivohivo watu wanamjua sana Magufuli kuliko waziri mwingine kwa nini? hayo ni maswali muhimu ya kujiuliza usijibu kijujuu tuu. think great my dear!
 
Huyu jamaa asione utepe atatakaaa aukate anatembea na mkasi mfukoni,hamna haja ya kua na makamu wa rais,awe rais then waziri mkuu
 
Back
Top Bottom