DJs Redio Free Africa mnaniboa

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
49
Naamini wana JF mtakubaliana na mimi katika hili, hawa DJ wa redio free Africa sijui hawajasomea mpangilio wa burudani au ni jeuri tu, yaani utasikia usiku saa 4 na kuendelea muda ambao walio wengi tumepumzika, zinapigwa ndombolo, kwasa kwasa nk badala ya kupiga miziki raini wao wanavanga vanga tu, upuuzi mtupu

Nawashauri wajifunze kupitia redio nyingine nyingi, au Mh Diallo wapige msasa kidogo vijana wako.
 
Nadhani ikumbukwe kuwa radio husikilizwa na watu wengi, na kuna wasikilizaji muda huo wa usiku wapo ktk shughuli zao nyingi tu,hivyo muziki kama huo unaweza kuwa unawaweka sawa wasipitiwe na usingizi.
 
teh teh..sa achen mada hizo..leteni za ukweli..we saa nne usiku kwani hulali waanza skiza mindombolo..kwenda kulala.
 
Naamini wana JF mtakubaliana na mimi katika hili, hawa DJ wa redio free Africa sijui hawajasomea mpangilio wa burudani au ni jeuri tu, yaani utasikia usiku saa 4 na kuendelea muda ambao walio wengi tumepumzika, zinapigwa ndombolo, kwasa kwasa nk badala ya kupiga miziki raini wao wanavanga vanga tu, upuuzi mtupu

Nawashauri wajifunze kupitia redio nyingine nyingi, au Mh Diallo wapige msasa kidogo vijana wako.
miziki laini ni ipi?
 
Kaitaba, unajua maana ya radio Free Africa? unataka wapige miziki laini wakati sio utamaduni wao? ulishawahi kusikia nyimbo yoyote ya lil wayne RTD?.RFA inapatikana karibia africa nzima kwa hiyo ni lazima wapige nyimbo ambazo zina hasili ya africa .pia kuna kipindi chao cha usiku ambacho kinaitwa HAKUNA KULALA,sasa unategemea nini kipindi kinaitwa hakuna kulala hafafu wakupigie nyimbo laini ili ulale?
 
Nakuunga mkono JosM. naamini kama hauna utata music haikuzuii kulala. kuna walinzi wa doria, machangudoa, polisi wa zamu wanahitaji music wakati huo
 
Nawashukuru wana JF kwa maoni yenu, nimejifunza kitu, kuwa wale sela yao ni hakuna kulala,

Hivyo basi ni redio ya machangudoa, majambazi, maana askari hawawezi kuisikiliza badala yake wana redio calls.

All in all nawashukuruni sana
 
Mkuu naona unafika mbali huko sasa.Ina maana wewe unataka wapige nyimbo laini kwa kuwa radio nyingi zinafanya hivyo? ni utaratibu wao tu walio jipangia,kama unaona wanakuboa usisikilize radio yao.
 
Kaitaba wewe Muhaya wa wapi? kaka siubadilishe FM station au umelazimishwa kusikiliza hiyo RFA.
Wadau wa 9t shift wengi husikiliza RFA.
 
Mkuu naona unafika mbali huko sasa.Ina maana wewe unataka wapige nyimbo laini kwa kuwa radio nyingi zinafanya hivyo? ni utaratibu wao tu walio jipangia,kama unaona wanakuboa usisikilize radio yao.
Mkuu uliyosema hapa tuko pamoja, hata hivyo kwani ndhombolo au kwasakwasa zinatakiwa kupigwa muda gani kama si usiku. Kuna wengine muda huo ukifika wanaondoa kwenye redio zao ama cassette, cd,dvd,mp3,santuri, nk na kuendelea kula mangoma ya RFA bila wasiwasi. Ikumbukwe pia maeneo mengi inakosikika hayana umeme kinachotumika ni betri za kawaida, ukipiga kanda moja betri kwishnei, unaenda dukani tena kununua betri nyingine, lakini kwa redio, unatune tu RFA disco linaendelea kama kawa, hamna noma wala nini!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom