Dj Steve B Vs Dj JD

dj steve b = dj bura
Mkuu hatumtendei haki Steve B! Binafsi toka JD asiwepo hewani namsikiliza Steve B kwa kuwa anajua muziki! Ndo Dj pekee ktk Madj vijana ninae mkubali kwa sasa,Steve B anajua kutumia Turn table while hao wengine ujanja wao unaishia kwenye CD! Binafsi najua hakuna kama Dj JD Tanzania ila kwasasa hakuna wa kumsikiliza zaidi ya steve B hata kama hatuipendi clouds kama mimi!
 
Mkuu kwasasa Dj Steve b anaaminika ni dj bora lakini tukumbuke Dj JD kwasasa hayupo kwenye game kivile ila Dj JD ni dj wa kukumbukwa daima kutokana uwezo wake mkubwa wa kupiga muziki,Dj JD ana vitu vingi sana ambavyo Steve B hana! Labda cha ziada kwa steve b ni uwezo mkubwa wa kutumia hizi machine za siku hizi za CD sababu ni za wakati wake na muda wote anazitumia while Dj JD ni miaka mingi hayupo kwenye game moja kwa moja.funga kazi ni kwamba Dj JD ana uwezo mkubwa mno kuliko Steve B ktk kutumia LP! Hata marekani mpaka kesho Turn tables ndio kila kitu!! Lakini u dj sio kupiga mziki tu ni pamoja na kujua sound system! Dj JD alipokuwa akíingia studio za E.A enzi hizo mpaka sound ya radio ilikuwa ina inachange! Dj JD ni mtaalamu wa Sound system na anaweza kufunga muziki wowote mwenyewe! Upande wa ku entertain nafikiri hata Dj Steve B anajua kuwa hakuna dj entertainer kama JD tanzania nzima ana mtiririko wa kupiga (mixing) ya aina yake! Yaani muziki unapenya hadi kwenye damu jinsi anavyopanga nyimbo! Kwahiyo tukichambua kila kipengele utaona Dj JD ana vitu vingi ambavyo madj wengi hawana! Najua huu mjadala umeibuka sababu ya Dj JD kushirikishwa kwenye tamasha la Anti virus na anao mashabiki wengi sana hivyo some people from other side will try to turnish his image but the guy is Everlasting Dj JD!! Lakini pia tukumbuke Dj Steve B na Dj JD ni marafiki wakubwa!!
I

Umejibu vyema, JD kiboko huwezi kumlinganisha na Steve B hata kidogo
 
Ebu tupia kura yako na 7bu zako nan mkal?na ni cku gan alikurusha kwa ngoma?aidha club au redion..yoo
nadhani jibu umeshalipata kamwambie RUGAY kuwa watu wanamkubali JD mbya na ndiyo atasababisha 26/11/2011 pale viwanja vya posta huyo Steve B bado mchanga sana..! kazi mnayo redio ya wafuuuu....
 
Ebu tupia kura yako na 7bu zako nan mkal?na ni cku gan alikurusha kwa ngoma?aidha club au redion..yoo

Hapo unalinganisha kifo na usingizi kamanda! lakini sitashangaa john dilinga a.k.a.john mkimbizi akishindwa na huyo mtoto,kama dj lumuliko mengele a.k.a.muli B aliwahi "kumshinda" john dilinga pale bilicanas siku zile basi lolote linaweza kutokea hapa si unajua wabongo na mambo ya kuchakachua tena
 
Ebu tupia kura yako na 7bu zako nan mkal?na ni cku gan alikurusha kwa ngoma?aidha club au redion..yoo
DJ JD anapiga muziki bana! Namzimikia DJ JD wa club kuliko JD wa radioni,sisahau usiku tunaukaribisha mwaka 99 club bilicanus,mpaka leo nyimbo alizotupagawisha nazo nazikumbuka zote! Tulikuwa kaunta ya juu na Dj D White tukiruka mangoma ya jamaa!!
 
Ni mesoma comments nyingi na zimemtendea haki DJ JD, na nikweli kabisa he is the BEST, sasa je tkijaribu kumlinganisha na DJ Pinyee, nani zaidi???
 
Ebu tupia kura yako na 7bu zako nan mkal?na ni cku gan alikurusha kwa ngoma?aidha club au redion..yoo

Mtoa mada inaonekana kabisa wewe ni wa juzi kwenye suala la Muziki, Kwa sababu huwezi mfananisha JD na Steve B, Coz steve ni wa juzi tu kwenye U-dj Level za Jd ni akina Dj Rico ambao ndio hasa Jd alifanya nao kazi wakiwa wame-establish Kundi lao ya ma-dj 4 (Powerful four) akiwemo yeye Jd, Rico na wengine wawili ambao majina yamenitoka. Kipindi hicho huyo Dj steve B alikuwa ndo kwanza anaibuka pale east africa radio. kwa misingi hiyo Dj Steve bado ni mdogo kwa kila kitu kumfananisha na Everlasting DJ JD!!

Kumlingamisha Steve B na JD ni kutomtendea haki kabisa JD, Steve ni mtoto kwenye game hana uwezo wa kupagawisha mashabiki club wala kuwa-entertain radioni.

Nadhani ni mbinu chafu za kutaka kumshusha huyu jamaa ambaye ki ukweli huwezi fanikiwa!!!!
 
natamani niweke hapa mix tape moja ya DJ JD ya zamani kidogo(nafikiri mwaka 99) ya JD's Explosions mnyooshe mikono kabisa kwa huyu jamaa jinsi ngoma zilivyopigwa humo!!

Naihitaji sana Hiyo Mix tape ya JD's Explosions nawezaje kuipata?
 
Mpaka sasa ndugu wasoma wa mpambano huu wa DJ JD na dogo Steve B....unaonyesha kuwa DJ JD anaongoza kwa 100%. Naomba tufunge huu mpambano manake ni sawa na kumpambanisha Obama na Yusuf Makamba teh teh teh!
 
Ebu tupia kura yako na 7bu zako nan mkal?na ni cku gan alikurusha kwa ngoma?aidha club au redion..yoo

Tafadhali 2take radhi kwenye kurasa za mbele tena za gazeti la serikali....unalinganisha bakhresa na mzamili?!slaa na jk?!dazel na kanumba?havard na udom kisa promo au?ile slang 2 akiongea.....DJ John Dilinga Matlou mlinganishie waakina Pinyee au kay slay ukipenda.ucsahau kuomba radhi ndo ungwana.
 
Ni mesoma comments nyingi na zimemtendea haki DJ JD, na nikweli kabisa he is the BEST, sasa je tkijaribu kumlinganisha na DJ Pinyee, nani zaidi???
Hawa wapo kwenye level moja upande wa professionalism ingawa kuna vitu lazima wanazidiana! Unapotazama madj wa level hizi kikubwa sana kitachowatofautisha ni ladha(taste) ambapo kila mmoja amejizolea mashabiki kutokana na taste yake! Mfano unaweza kuchukua nyimbo kumi ukawapa wapige kila mmoja akatumia skills na taste yake kuzipiga na hapo ndio mashabiki watapogawanyika.ladha kwa dj ni muhimu sana ndio maana ktk madj vijana namuhusudu Dj Steve B sababu pia ana unique taste inayofurahisha! Akipiga muziki unajua huo ni upigaji wa Dj Steve B hata kama hajaweka jingle!! steve b anakipaji longtime sema alikosa displine ya kazi mapema(kama kuendekeza pombe enzi hizo!) tofauti na Legendary Dj JD!
 
EAST AFRICAS BEST DJS ni kama ifuatavyo.1.DJ JD 2.DJ PINYEE 3.DJ STEVIE B 4.DJ RICO 5.RANKIM RAMADHAN 6.PETER MO.7.DJ COOL PARA 8.DJ 45KING 9.DJ MALIS 10.DJ PQ 11. DJ BHAA 12.DJ CUTTER 13.BUSH BABY.14.DJ BON LUV15.DJ KWA FUJO16.DJ J4 17.EMA BLAZE NA KUENDELEA
 
Steve B = gobole
JD = ground to air missile
Sasa amua mwenyewe kuna haja ya kulinganisha damage ya silaha mbili hizo?
 
EAST AFRICAS BEST DJS ni kama ifuatavyo.1.DJ JD 2.DJ PINYEE 3.DJ STEVIE B 4.DJ RICO 5.RANKIM RAMADHAN 6.PETER MO.7.DJ COOL PARA 8.DJ 45KING 9.DJ MALIS 10.DJ PQ 11. DJ BHAA 12.DJ CUTTER 13.BUSH BABY.14.DJ BON LUV15.DJ KWA FUJO16.DJ J4 17.EMA BLAZE NA KUENDELEA

namba moja na namba mbili umenena,ila kuanzia namba tatu umeharibu kila kitu mkuu
 
Mkuu hatumtendei haki Steve B! Binafsi toka JD asiwepo hewani namsikiliza Steve B kwa kuwa anajua muziki! Ndo Dj pekee ktk Madj vijana ninae mkubali kwa sasa,Steve B anajua kutumia Turn table while hao wengine ujanja wao unaishia kwenye CD! Binafsi najua hakuna kama Dj JD Tanzania ila kwasasa hakuna wa kumsikiliza zaidi ya steve B hata kama hatuipendi clouds kama mimi!

Turntable ipi mkuu??
Watu wanasugua LP itakua hizo zenu za siku hizi ambazo hata mtoto mdogo anazichezea!!!!
JD bado ni moto mkuu, labda kwa mbali afuatiwe na watu kama Dj Ommy na Dj Q.
.
Steve B = Dj Majizo
 
Mkuu nilitaka kukomenti lakini ulipomtaja Dj Ommy na Dj Q nimechoka kabisa!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom