Elections 2010 Diwani wa CHADEMA (na member wa JF) atekwa Igunga

Pamoja mkuu, poleni sana na dhahama hilo.
Wakuu,ni kweli green guard walituteka usiku,tukielekea kulala,ghafla gari ilifunga break mbele yetu,kisha mabaunsa wakatuteka,na gari aina ya Landcruiser kuondoka kwa kasi ya ajabu,kuelekea porini,ndani ya gari tulilazimishwa kunyanyua mikono juu,
Tukiwa ndani ya gari,hawa mabaunsa wanne walitutaka tuombe sala za mwisho,kwani ndio mwisho wetu,porini gari ikapunguza mwendo sana,kama vile inataka kusimama,ndipo ghafla nikarukia kwenye sterling,hivyo gari kukosa mwelekeo na kusimama porini na hapo purukushani ikaanza,sisi tukipambana nao,ndipo wakatuzidi na kututupa porini,tukakomaa porini hadi asubuhi
Asubuhi tukaenda polisi kuripoti ndipo tukakuta tayari hawa wahuni walishafika na kudai eti sisi ndio tumewateka,baada ya kutoa maelezo upelelezi unaendelea
Kimsingi bado tupo Imara,na mapambano yanaendelea
 
Back
Top Bottom