Elections 2010 Diwani wa CHADEMA (na member wa JF) atekwa Igunga

Nanyaro upatapo muda weka hii habari vizuri, je kweli au laa!!!!!!
 
Hii picha ilikuwa tamu kweli. Watu wanapigana wakati gari ipo kwenye mwendo.. Je diwani aliumia baada ya kupewa kipigo na kuchomoka kutoka kwenye gar?.
 
Haya mambo haya sasa naanza kutoyaamini!!
Crashwise, hiyo story yako ina matundu mengi sana.

1)akamrukia dereve...........washirika wa dereva wakakimbia, je gari ilikuwa imesimama au inatembea? na ni station wagon, right?
2) dereva aliyepewa roba au ambaye anapambana na mtu aliyeng'ang'ania steering wheel huku gari ikitembea, aliwezaje kumpa kipigo Ephata, na kumtupa nje ya gari?? na huyo mwenzake Ephata alikuwa anafanya nini??

hizi story zinaanza kuniudhi sasa!!

Katika wa2 mizigo humu jamvini huyu Best ni mmoja wao! Utafikiri kalazimishwa kuja humu. Mtu mwenye uwelewa wa kujua mambo yalivyo hana haja ya kujikanyagakanyaga humu. Kama una kichwa maji acha kuingia humu nenda kwanza Mirembe ama Muhimbili ukatibiwe,Kondoo wee! Unahabarishwa news unaleta mambo yako ya mwaka 47 humu. Kwenda zako kondoo wee!
 
Diwani wa CDM Ndg Nanyaro Ephata alitekwa yeye na mwenzake mmoja aitwaye Boniface na kupelekwa kusikojulikana. Wakiwa njiani kurudi hotelini ghafla walivamiwa na watu ambao walikuwa katika Toyota Landcruiser S/W T 203 BKW na kutekwa.

Huo ulikuwa ni usiku wa saa saba ambapo walikuwa wamemaliza kikao chao na kwenda kupaki magari mbali kidogo na hoteli waliyofikia ambayo haina parking. Wakiwa ndani ya gari, waliambiwa kuwa wasali sala zao za mwisho kwani kiherehere chao ndicho kilichowaponza! Baada ya kusikia hivyo Nanyaro ambae ni diwani wa Chadema Arusha kata ya Revolosi alijipanga ama afe yeye au wao nao wafe, hivyo alimrukia dereva na kuanza kung'an'gania steringi ili gari lipoteze mwelekeo. Kuona balaa limeanza jamaa mmoja alikimbia katika hao watekaji na kubaki watatu.

Dereva alipoona anashindwa kulimudu gari alimpa kipigo Nanyaro na kumsukuma nje ya gari yeye na mwenzake na kuondoka kwa kasi. Huo ulikuwa ni usiku na porini, kibaya zaidi katika purukushani ile jamaa walidondosha simu katika gari lile. Wakajitahidi kufika mjini na kupata msaada toka kwa viongozi wa CDM na kwenda kulipoti tukio hilo polisi ambapo walipofika walikuta tayari wameshafunguliwa kesi na wale jamaa kuwa walitaka kuwateka hao jamaa na wao walifanikiwa kuwadhibiti na kuwapora simu! Basi ikabidi nao watoe maelezo ambayo yalipelekea kurudishiwa simu zao!

Angalizo langu, tabia hii ya utekaji watu naona imeanza kushamiri, tabia hii ni mbaya na inapaswa kukomeshwa mara moja.

CCM wamechoka wamechakaa, mambo wanayoyafanya si ya kawaida kabisa. hawana tofauti na Maharamia wa somalia.
Kamanda Nanyaro nimeongea naye yupo salama, mapambano yanaendelea kama kawaida.
 
Katika wa2 mizigo humu jamvini huyu Best ni mmoja wao! Utafikiri kalazimishwa kuja humu. Mtu mwenye uwelewa wa kujua mambo yalivyo hana haja ya kujikanyagakanyaga humu. Kama una kichwa maji acha kuingia humu nenda kwanza Mirembe ama Muhimbili ukatibiwe,Kondoo wee! Unahabarishwa news unaleta mambo yako ya mwaka 47 humu. Kwenda zako kondoo wee!
Unanitafutia Ban tu we dogo!!!
Don't get Angry, get Even
 
Ni dhahiri kwamba utekaji, ujambazi, na mambo mengine ya uhalifu unafundishwa na chama cha mapinduzi. ndiyo maana uhalifu hauishi nchi hii.
Dawa ni kuipindua tu serikali ya chama cha mapinduzi ili uhalifu wa aina yoyote ukome nchi hii.
 
Duh!
Kuna habari nyingine zinakuharibia mudi hadi unashindwa kuchangia! Hata bia inaenda kwa mawazo sasa....!?
 
Ni vibaka tu wa Igunga hakuna utekaji hapo!

When mzee Hoarace was silenced, our hearts started to cry! It had been crying from that time and the trauma goes very deep.
Na sasa uvumilivu (sio amani na utlivu) unakaribia kwisha na kipimo ni kesho.
 
Mtoa taarifa ebu tupe maelezo ya nini Polisi imefanya juu ya Jambo hili.
 
Hii picha ilikuwa tamu kweli. Watu wanapigana wakati gari ipo kwenye mwendo.. Je diwani aliumia baada ya kupewa kipigo na kuchomoka kutoka kwenye gar?.
Hii habari inachanganya kwa kweli...
 
Hii habari inachanganya kwa kweli...
habari hii itasadikika tu pale nanyaro mwenyewe atakapoweka wazi, lakini kwa maelezo ya mtoa mada inakuwa ngumu kusadiki, mazingira yanakataa kufikirika.
 
Back
Top Bottom