Diwani wa CHADEMA mbaroni kwa Kuchoma Nyumba Geita

Mzee wa Posho

Senior Member
Jul 14, 2011
160
13
Diwani wa CDM na wanachama wengine 9 wanashikiliwa na Polisi kwa Kuchoma nyumba ambayo walidai ipo kwenye kiwanja kwa ajiri ya kutengeneza stendi ya Mabasi! Wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa CDM,walikubaliana wakateketeze nyumba hiyo,ndio maandamano yakaelekea kwenye nyumba hiyo yakiongozwa na Diwani huyo!

Source: Taarifa ya habari ITV na TBC1 Usiku saa 2
 
hawa jamaa mbona wanatuletea siasa za kishamba namna hiyo hatua kali zichukuliwe dhidi yao
 
Wachukuliwe hatua kisheria,kamanda Barlow wahukumiwe kama waharifu dhidi ya mali(crime against property)..hizi ndio siasa uchwara.
 
Diwani wa CDM na wanachama wengine 9 wanashikiliwa na Polisi kwa Kuchoma nyumba ambayo walidai ipo kwenye kiwanja kwa ajiri ya kutengeneza stendi ya Mabasi! Wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa CDM,walikubaliana wakateketeze nyumba hiyo,ndio maandamano yakaelekea kwenye nyumba hiyo yakiongozwa na Diwani huyo!

Source: Taarifa ya habari ITV na TBC1 Usiku saa 2
haya ni matokeo ya serikali legelege huyo mganga alie kuwa anakalia hicho kiwanja ambacho kilipaswa kuwa standi/soko alitakiwa kuondoka mahali hapo tangu 1994 leo 2011 ulitaka wananchi wafanye nini, je wananchi wana asthirika kiasi gani kwa kung'ang'ani kwake kwenye kiwanja hicho, huu siyo muda wa kubembelezana...Ndiyo maana huwa nina mkubali magufuli linapofikia swala la kutekeleza kuwa hajing'ating'ati....
 
Madhara ya nchi kukosa siasa safi na uongozi bora ni makubwa sana. Tuendako JK anaweza kuleta janga la kitaifa kwa kutofanya maamuzi magumu na makini badala yake analea mafisadi kuanzia serikali kuu mpka serikali za mitaa. Wananchi lazima watafikia mwisho wa uvumilivu. Dalili zimeanza. Wala chadema wasilaumiwe kwa hilo.
 
Back
Top Bottom