Diwani wa CCM afariki India

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,690

Diwani wa CCM kata ya Mpwapwa amefariki huko India aikoenda kwa matibabu, amefariki usiku wa kuamkia leo baada ya kupigana na ugonjwa wa ini uliopelekea figo zake kufeli kabisa. Huko India alienda kwa nguvu za familia baada ya madaktari wa bongo kumshauri asiende huko, sasa wanainchi wanajiuliza gharama za kurudisha maiti zitakuwa za nani. Diwani huyu alijulikana kwa jina la Dr. Noah Maiseli ni msomi aliyesomea mambo ya vetenali na alikuwa amestaafu kazi serikalini.


MY TAKE : Chadema inaweza kuchukua kata hii kwa sababu Kigaila aliisha waamsha miezi kadhaa iliyopita na teyali wemiisha fungua ofisi na kadi zinauzwa kama njugu. Ila wakati Kigaila anawaamsha kiongozi mmoja wa CDM toka mkoa upande wa akinamama akijulikana kama EVA Mpagama aliwatukana walimu wanawake wa Mpwapwa kwani anabeaf nao mmoja wao anachukuliwa na mme wake walioachana kwa hiyo hafai kuja huku kifanya kampeni kwa sababu walimu wanawake wanaweza kupiga kura ya chuki.
 
kimajungu jungu mchanganyiko wa habari. Mambo ya CDM na mtu kuchukuliwa mume MBONA HAVIENDANI!
 
mkuu, kwanza tuwape pole wafiwa, then siasa zitakuja baaaadae kabisaaaaa,
 
Hizi habari zilete kaama taarifa za msiba wa mwanasiasa basi haya mambo ya cdm kuchukua hiyo kata na nani anatembea na nani huu sio wakatu wake wala hapa sio mahali pake!! mungu ailaze mahali inapostahili roho ya marehemu Diwani
halafu sijaelewa vetenali ni kitu gani au you mean veterinary??
 
CCm kumbe njema. hata ukiwa diwani unakwenda kutibiwa India!:nono:
 
Diwani hiyo atachaguliwa siku moja na kamanda Lema wakati anarudishiwa Jimbo lake,ambaye atakuwa wa CDM
bila shaka.Maana moto wa M4C hakuna wa kuuzima
 
Apumzike kwa amani!
Waliompeleka ndio watakaomrudisha!
Kwanza gharama ya kusafirisha maiti ni rahisi zaidi kuliko mzima!
 
Poleni sana wana-Mpwapwa hasa wale wa Mitaa ya Igovu. Marehemu Dr. Maiselli, namfahamu sana alikuwa ni mtu makini sana japo alikuwa CCM.
 
Poleni Wafiwa na Wana-CCM,

Ukifika wakati wa kampeni nitaongea zaidi.




MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Neema inazidi kuishukia cdm kujiongezea kata. RIP to him
 
Tunataka wafe wabunge bwana diwani wa nini sasa ..jamanii mbona mnauana kwenye mambo yasiyofaa tulteeni msiba wa mbunge wa ccm tuanze kazi
mkuu umenifanya nicheke sana. adui yako muombee njaa.
 
CCm kumbe njema. hata ukiwa diwani unakwenda kutibiwa India!:nono:

Ndo maana mimi huwa ninasema, ukiona mtu anaipenda ccm ujue aidha ni mjinga au Fisadi/anafaidika na ufisadi, bwana Shomari, soma vizuri, mstari wa pili wa hiyo report ya mdau kutoka Singda, anasema hivi, "Juhudi za kumpeleka India zilifanywa na wanafamilia, sasa wanajiuliza watarudishaje mwili wa marehemu? So usisema kuwa ccm ni njema, uwe unasoma vizuri kabla ya kuchangia.

Poleni wafiwa, Bwana alitoa na Bwana ametwa, Jina lake libarikiwe!
 
APUMZIKE KWA AMANI,KATA YA CHADEMA HIYO TOKEA AWALI WALICHAKACHUA TUNAJUA SASA TUTAICHUKUA KAMA KIRUMBA NA KIWIRA NA ARUSHA MJINI BAADAe
 
Back
Top Bottom