Diwani mwingine (CCM Mwanza) ahamia CHADEMA

Wengine wanasubiri nini kufuata nyayo? Lema ni mvuvi wa kweli mfuateni jama!
 
Mtaka vyote hukosa vyote. Ccm mmelitaka jimbo la arusha town, sasa arusha nzima inahamia chadema ni sio arusha tu. Nadiriki kutabiri kwamba kabla tufike 2014 nusu ya wabunge wa ccm watakuwa chadema, hofu yangu chadema isije ikawakumbatia mafisadi wanaoikimbia ccm wakajivua gamba na kuvaa gwanda ili waendelee kutufyeka watanzania masikini.
 
Matokeo ya kihuni ya kesi ya ubunge arusha urban.wamechokoza moto.God bless Godbless Lema!
 
Matokeo ya kihuni ya kesi ya ubunge arusha urban.wamechokoza moto.God bless Godbless Lema!

Watu wanadhani huu ni utani,safina ni kweli itafungwa maana kama wapiga kura 2015 wapiga kura wanatarajiwa kuwa 24,820,400,na chadema ikiwa na wanachama 11,000,000 ushindi ni lazima.Kwa kuwa sasa wanachama wanafikia 7,000,000 na usheh hivi,ni ehahiri safina inakaribia chadema.Watu wawahi
 
Duuhu Tumshukuru Mungu kwa wenzetu kujua kwamba nyakati za ukombozi wa nchi yetu sio za kungoja tena ni sasa na wote tuwaunge mkono

Hamisi umejipambanua vizuri kwetu sisi watu wa Mkoa wa Mwanza, Kweli unaongoza kwa vitendo wala si maneno. Heshima kubwa uliyojijengea hakika haitamomonyoka kirahisi, hongera sana mwana wa Tabasamu, Sengerema iko nyuma yako na vijana wa Mkoa wa Mwanza hakika wanakuunga mkono. Niliwahi kuuliza tarehe 18 April 2012 Jumatano saa 4.46asu, nani shujaa upande wetu? maana tunahitaji shujaa upande wetu ili kushinda, hakika ni kama masaa 24 tu, mimi ninakutangaza shujaa maana najua umejitoa kwelikweli.

Hamisi njia ulochukua ni ya watu jasiri hakika usirudi nyuma, najua unafahamu watanzania wengi ndani na nje ya mipaka ya Nyampulukano wanakuunga mkono kwa dhati na kwa ujasiri pia. Hongera tupigane kiume kujenga Tanzania yenye jamii yenye neema.
 
Back
Top Bottom