Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
<br />Hata wakati wana wa israel wanatolewa utumwani misri kuna ambao walimlalamikia musa kuwa amewapeleka ili wakafie jangwani na walitamani kurudi misri kwa hiyo siyo ajabu kwa huyu diwani kurudi misri (ccm)
Sizitaki mbichi hizi!!Afadhali wajiondoe, bado Yule mpumbav* Shibuda. . . Tokeni Cdm, UKOMBOZI HAUKO MBALI.
Mbona walishaondoka akina Kaborou CDM haijaanguka? Huyu Diwani upeo wake umekaa kimagamba! Ndani ya "utulivu na amani" kuna ufisadi wa kutisha na bila kuwapelekesha mchakamchaka Magamba yatakula bila kufuta midomo!
Huyu Diwani hakuwa katika kusimamia haki za Watanzania shida yake ni uongozi na kuzitafuna haki za Watz, hao ndio wale wale, Gamba la kuvua, amepima akaona CDM hakuna za kutafuna, akaona arudi kwa system aliyoizoea, tazama kauli yake ya mwanzao "Nimeamua kujiuga Chadema bila kushawishiwa na mtu" alafu kauli ya pili "Nilijiuga kugombea kupitia CDM nilishawishiwa na wananchi" je ajatujuza kurudi CCM ni nani amemshawishi, na kauli ya kuwa huko anapotoka kunachochea vurugu au uvunjifu wa amani, ni kauli ya nani!??? Hawa ni baadhi ya viongozi ambao Watz wanatakiwa kuwa makini nao sana, hawa ni mizimu inayokunywa damu ya Watz. hata huko walipomtosa wanamfahamu ya kuwa huyo jamaa ni kipofu wa mawazo ni mcheza karata asiyekuwa na turufu.WAKATI ikiwa katika mgogoro na madiwani wake wa Arusha, Chadema imepata pigo baada ya mmoja wa madiwani wake Singida kujiengua na kurudi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), akidai hataki kuwa sehemu ya machafuko nchini.
Diwani huyo, Simon Tyosela wa kata ya Urughu, Iramba Magharibi, alisema hayo jana katika Ofisi ya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, mbele ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM anayeshughulikia masuala ya Uchumi na Fedha, Mwigulu Mchemba.
Tyosela aliyehamia upinzani wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 baada
ya kuanguka katika kura za maoni ndani ya CCM, alisema hakushawishiwa kuihama Chadema na kurejea CCM, bali amenusa hatari kwa taifa katika siku za usoni.
Alisema, maandamano yenye sura ya uchochezi kila kukicha, yamemkosesha amani na
kujiona msaliti mbele ya Watanzania.
Haya ya kushinikiza wananchi kuiga maandamano katika nchi za wenzetu, tena yasiyo ya amani, binafsi yamenishinda. Chadema hakuna demokrasia ya kweli na nilitarajia ingekuwa mstari wa mbele kuhangaikia maendeleo ya wananchi. Nimejiondoa kwa sababu mimi ni mpenda amani kwa nchi yangu.
Kwa mtindo huu niliona kabisa hatuwezi kufikia malengo ya millennia, kwa sababu
kila kukicha ni maandamano, hakuna la maana linalofanyika kwa ustawi wa nchi
yetu, alisema diwani huyo.
Alisema, hana cha kujutia kwa sababu wananchi ndio waliokuwa wamemshawishi kuingia Chadema wakitaka atumie chama kingine chochote kuingia madarakani, baada ya kushindwa kura za maoni.
Mchemba alimpongeza na kuitaka jamii kutokubali kuburuzwa na vyama vingine vya siasa kwa maslahi ya watu wachache wenye mwelekeo wa kulazimisha kushika madarakani kwa nguvu.