Maishamapya
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 1,279
- 375
Vyama vya siasa vijifunze kutafuta watu waaminifu, na wenye uzalendo wa kweli, watu kama hawa wanaweza kushusha sifa ya chama kwa kutokuwa wavumili katika harakati!!!
Nafikiri huo ndio mtihani mkubwa sana kwa CHADEMA maana uaminifu haupimwi kwa kauli za juu juu tu. Nadhani uaminifu unaweza kupimwa kwa dhamira ya dhati ya mtu ya kutaka kuleta maendeleo kwa wananchi wake. Na hii haijifichi kwa sababu inaonekana katika uzalendo wa mtu. Hatetei hoja kwa vile zimeletwa na chama chake bali anatetea maslahi ya taifa.
Nimesoma hoja nyingine katika thread hii zinasema CDM wajihadhari kuchukua watu wanaokuwa wameachwa/ kubwagwa kutoka CCM. Mimi natoafautiana nao. Maana kama ni hivyo basi leo tusingekuwa na Dr. W. Slaa.
Nadhani CDM inahitaji kuangalia kwa dhati dhamira ya watu itakaowasimamisha kugombea nafasi mbalimbali kwa kuangalia track record zao. Je wana dhamira ya kweli ya kuwasaidia wananchi wao na taifa kwa ujumla? Na hii haitajalisha ama wako ndani ya CDM au ni wahamiaji. Hakuna chama kitakachoepuka kupata wahamiaji wakati wowote. CDM hivi majuzi wamempata Profesa Safari ambaye ametokea CUF; tusemeje hapo?
CDM inao kina Shibuda sasa hivi ambao wamekuwa mwiba sana kwa chama.Track record ya Shibuda ni ya uchu wa madaraka. Naomba kurudia, Shibuda (mkazi wa upanga, mtaa wa Kalenga) ana uchu wa madaraka. Hii imeonekana alipokuwa kwenye vyama vya wafanyakazi na ndani ya chama kilichomlea. Mtu kama huyu hakufaa kukaribishwa kwenye chama chochote na hasa chama makini kama CHADEMA.