Diwani amtorosha mtoto yatima ampeleka kwa mwanae kuwa mke na akaambulia kubakwa!

tete'a'tete

JF-Expert Member
Feb 10, 2010
472
62
Wana JF natumai muu buheri wa afya!

Hii habari nimeiona jana kwenye ITV imenisikitisha sana. Diwani wa kata ya Mamba, Marangu Mkoa wa Kilimanjaro na mtoto wake wa kiume wanashikiliwa na vyombo vya dola kwa kosa la kumtorosha mtoto yatima mwenye umri wa miaka 15 kwa nia ya kumsaidia kumpeleka shule lakini lengo lake likawa ni kumpeleka kwa mtoto wake wa kiume anayeishi Arusha akawe kama mke habar nilizozipata ni kwamba mtoto wa diwani alikimbiwa na mchumba mapema mwaka huu akaamua kunywa sumu ambayo walimuwahi hospitali wakafanikiwa kuokoa maisha yake...sasa nadhani kumwondolea labda stress Diwani huyo ambaye inasemekana anampenda sana mtoto wake huyo wa kiume akaamua ampelekee mke ambaye ni huyo mtoto yatima aliyekuwa anatafuta mtu wa kumsaidia kielimu. Binti baada ya kufikishwa Arusha ambako ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika huko alipelekwa kwa huyo kijana akaambiwa huyo ndio mume wako baadaye kijana alimbaka tena kwa kipigo kikubwa binti alilia kwa uchungu sana! Mungu si Athumani yule binti alitumia akili zake za kuzaliwa akafanikiwa kuchukua nguo zake akavalia sebuleni akatoroka akaelekea Arusha mjini ambako alikutana na wasamaria aliwahadithia mkasa ulivyokuwa basi walimsaidia nauli akarudi nyumbani kwao Marangu Mamba. Jamani huyu Diwani na binti aliyebakwa ni majirani zangu kweli hii imeniuma kwa sababu kitendo alichofanya huyu Diwan ambaye ni mzee ana mpaka wajukuu ni aibu kwake kwa jamii hata taifa letu kwa ujumla..Huyu Diwani ana watoto wengi tuu wa kike na wakiume kwa nini atumie cheo chake kwa kuwanyanyasa wananchi!imeniuma sana!suala hili lipo kwenye vyombo vya sheria natumaini haki itatendeka....
 
Mkuu huyu diwani anakaa kipande kipi hapa Marangu ili ikiwezekana aambiwe live?
 
atafunguliwa mashtaka mara moja si wako chini ya ulinzi!
huyu mzee nae **** tu, anatumia mbinu ya kishenz namna hii
 
Mkuu huyo diwani anakaa hapo mamba karibu na Kanisa la kiluthery ya Mkoloyonyi! anajulikana sana! we ulizia tuu...Diwani wa Mamba...
 
Nimeisikia hiyo, nadhani huyu diwani na mtoto wake wote wapewe zile adhabu za kibonde(JAHAZI LA CLOUDS) wakatwe dudu zao taratibu na kila siku kidogo kidogo mpaka ziishe halafu wamsomeshe huyo binti mpaka afike university. NYAMBAFFFFFFFFFFFFFF
 
Back
Top Bottom