TANZIA Ukiwaona Ditopile afariki dunia

Uchunguzi wa Jf unasemaje ,maana huyu jamaa alikuwa na kesi ya kuua ,huyu jamaa ni rafiki wa CCM, kesi ilikuwa bado ipo mahakamani.
Je safari yake kuelekea Moro ilianzia wapi ni nani na nani wakifuatana nae ,kabla ya kufikiwa na Kifo Chake ni sehemu gani alikuwa akitembelea ,amewahi kuhudhuria kongamano la aina yoyote yaani kwa muda wa mwezi inabidi mwenendo wake ujulikane,historia yake kiafya.
Kuna vifo vya kutatanisha Tanzania vinavyowakumba viongozi na kila siku vinazidi idadi.Na kuna ufisadi na Mafisadi ambao kifo cha mmoja kinaweza kikapoteza ushahidi wa wote.Wale wakuu wa Ufisadi naona bora mkimbie yaani kama mimi ndio Chenge ,hapa msingeliniona tena ,ningejiuzulu na kusema napumzika ,yaani ningetoa sababu yeyote tu na kuyoyomea kusiko julikana ,maana kuna mtu aliokota dola kama milioni 4 au arobaini hivi,Mjini Califonia eti akazirudisha polisi ,jamaa walimshangaa alipoulizwa akasema hajui atazitumiaje !!
Mwenyezi Mungu amjaalie afueni Ditopile kwani siri ya kesi iliyomkabili ukweli wa undani wake anaeujua ni yeye Mwenyewe mwenyezi Mungu,kwani yeye ndio Hakimu mjuzi.
 
RIP brother Dito.
May be Hassani Mbonde (commuter bus driver) alipeleka kesi yake kwa Sir God baada ya kuona serikali ya "Tengaruzi" haimtendei haki.
 
Ras-Nungwi
...unaanza hivyo. CV ya nini na mtu ameshafariki??. lililobaki ni kumuomba mungu amuweke pahala anapostahiki. AMEN

stone towner.
Sote ni wa Mwenyeenzi Mungu na sote tutarejea kwake bila ya shaka.

Huyo ndugu yetu aliyetaka CV ya Marehemu pengine ana kazi muhimu au anataka kuandika some thing tusimlaumu moja kwa moja labda anataka imsaidie kwa kazi zake.

lakini upande mwengine ikiwa anaitaka kwa ajili ya kumuundua tu marehemu basi nadhani sio vizuri bora ndugu yetu uwache maama unajau sisi watanzania naona kama tunakwenda sehemu mbaya hivi sasa yaani tunasubiri mtu aje ndio tuanze kumsifu na kumkashifu bila ya kujali maumivu ya wale familia yao kwani kila binaadamu ana ndugu, jamaa, watoto hivyo kufanya vitendo kama hivyo tunakuwa tunawaumiza wafiwa mimi nadhani kwa maoni yangu tabia hii tuanze kuiwacha ingawa ni ngumu kwa wengine kuwacha lakini wajaribu kujiwekea mazingira ya kuheshimu wenziwao ili nao waje kuheshimiwa.
naomba kutoa hoja ingawa nilipotea kw amuda mrefu lakini sasa nimerudi inshaallah .
karibuni sana kijiweni kula orojo, badia na kababu.

Ndugu zangu, nadhani kwa kawaida watu huandika kitu kinaitwa "Buriani/tanzia" ambacho hujumuisha maisha ya marehemu na mtu anayeandika huwa ni yule anayeguswa kwa karibu na msiba husika na kwa hili, ni kwamba kuna mtu aliyenipa ombi hilo akiwa na nia ya kuandika Tanzia ya anavyomfahamu Ditopile lakini akapenda kupata official CV yake ili aweze kuboresha anachokusudia kuandika na kwa kweli itasaidia wana JF wengi zaidi. Tukubali tusikubali, pamoja na mapungufu yake ya kibinadamu, Ditto alikua mtu muhimu sana kwa Taifa hili la Tanzania, ambalo limejaa, akina "Makamba" kibao
 
Tukubali tusikubali, pamoja na mapungufu yake ya kibinadamu, Ditto alikua mtu muhimu sana kwa Taifa hili la Tanzania, ambalo limejaa, akina "Makamba" kibao

Halisi ,

Unaweza ukatuelezea Dito ni umuhimu gani haswa unaongelea hapo juu?
 
Jamani sio wote wanaamini dini zenu. Mimi nitamkumbuka kama mtu aliyeshutumia kuua ambaye sheria ilimuacha kwa sababu ni rafiki wa rais wetu. Namuombea aende motoni kama upo. Pamoja na hayo isije ikawa usanii maana hii ni bongoland.
 
Uchunguzi wa Jf unasemaje ,maana huyu jamaa alikuwa na kesi ya kuua ,huyu jamaa ni rafiki wa CCM, kesi ilikuwa bado ipo mahakamani.
Je safari yake kuelekea Moro ilianzia wapi ni nani na nani wakifuatana nae ,kabla ya kufikiwa na Kifo Chake ni sehemu gani alikuwa akitembelea ,amewahi kuhudhuria kongamano la aina yoyote yaani kwa muda wa mwezi inabidi mwenendo wake ujulikane,historia yake kiafya.
Kuna vifo vya kutatanisha Tanzania vinavyowakumba viongozi na kila siku vinazidi idadi.Na kuna ufisadi na Mafisadi ambao kifo cha mmoja kinaweza kikapoteza ushahidi wa wote.Wale wakuu wa Ufisadi naona bora mkimbie yaani kama mimi ndio Chenge ,hapa msingeliniona tena ,ningejiuzulu na kusema napumzika ,yaani ningetoa sababu yeyote tu na kuyoyomea kusiko julikana ,maana kuna mtu aliokota dola kama milioni 4 au arobaini hivi,Mjini Califonia eti akazirudisha polisi ,jamaa walimshangaa alipoulizwa akasema hajui atazitumiaje !!
Mwenyezi Mungu amjaalie afueni Ditopile kwani siri ya kesi iliyomkabili ukweli wa undani wake anaeujua ni yeye Mwenyewe mwenyezi Mungu,kwani yeye ndio Hakimu mjuzi.

Hii inaleta changamoto,,nitarudi.
 
Mungu tunakushukuru kwa kutumzisha,mwache dito apumzike, ina maana Mzee Kikwete amepoteza mtu wake wa karibu
 
The guy was a killer, he deserves to die like a fly. Sina sababu ya kuwa mnafiki na nafahamu fika pesa ya walipa kodi itapotea tena kwa kuzika uaji hili.
 
Binadamu akifanya makosa tunamshutumu na kumshambulia akiwa hai, ili shutuma na mashambulizi hayo yamsababishie maumivu, aadhibike aache maovu anayofanya au atufidie kama inawezekana. Lakini anapokuwa ameshakufa, hana tena nafasi ya kusikia maumivu wala uchungu, bali wenye majonzi ni wale wafiwa ambao sisi hawajatukosea lolote. Kwa hiyo tunapotoa salamu za faraja katika msiba, hatumlengi aliyekufa maana yeye hazihitaji, tunawalenga wafiwa, ndio wenye uchungu. Na hata kama marehemu alitukosea, hao wafiwa hawajatukosea chochote, na hata wangetukosea bado kipindi cha msiba si mahali pake kumwadhibu mwenye majonzi kwani ni sawa na mgonjwa, ni kumnyanyasa. Jukumu la kumhukumu marehemu si letu, na hata tukijaribu kuliingilia, kwanza hatutaweza kumhukumu kikweli, na pili tutakuwa tunawaumiza kihisia watu wengine tofauti kabisa ambao hawahusiki wala hawakushiriki hatia ya marehemu huyo. Kwa hiyo wote wenye matatizo na Dito wasiyaingize msibani, kama kuna hukumu basi ndio sasa yuko huko, inamhusu mwenyewe na Mungu wake. Sisi tumeachiwa watu wenye huzuni, wafiwa, na ni wajibu wetu wa kibinadamu kuwapa pole na kuwafariji.
 
Hivi hii thread si ingekuwa kwenye siasa? Leo hii habari ya kifo cha Ditto imekuwa "matangazo madogo madogo?"

Ama kweli hujafa hujaumbika!
 
Mwenyezi Mungu, Mungu muumba wa Mbingu na Nchi, aliyemuumba Ditopile hatimaye amemrudisha kwake.
Bwana alitoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe. Amen.
 
The guy was a killer, he deserves to die like a fly. Sina sababu ya kuwa mnafiki na nafahamu fika pesa ya walipa kodi itapotea tena kwa kuzika uaji hili.

Dua that is too much. I can see how you are frustuated with the fact that justice was not done. But we can not reverse it. Wenye ndugu ndio walie tu, labda wamuombe mungu anaweza kuwasikia!
Lakini kumbuka, pamoja na yote hayo sioni kama ni vema kumkashifu na kumsemea mabaya huyu ndugu. Tulikuwa na thread nyingi zilikuwa zinatoa platform za kumsema akiwa hai. Let us use this thread kukumbuka vimbwanga vyake na mazuri yake, binadamu ana mazuri na mabaya!
 
Hivi ndivyo nimkumbukavyo huyo dito wenu,

1. HILI JAMAA LILIKUWA LINATEMBEA NA WAKE ZA WATU. LIKIULIZWA LINAJIBU NYIE KINAWAUMA NINI KAMA MWENYEWE HAKIMUUMI.

2. HILI LIJAMAA LILIKUWA LINATOROKA KAZI TBR LINAKUJA KUFANYA UHUNI DAR

3. HILI JAMAA LILIUA KWA MAKUSUDI ETI TAA YA GARI LAKE IMEKWANGULIWA. KWA AKILI ZAKE TAA ZA PRADO YAKE ZILIKUWA NA THAMANI KULIKO UHAI WA MTU - SIONI KWA NINI NYIE WENGINE MNALIONA LINAHITAJI KUOMBEWA

4. BAADA YA KUUA LIKAHONGA NA KUTOLEWA MAHABUSU HALAFU LIKAHONGA LIKABADILI KESI YAKE.

MAMTU YA NAMNA HII HAYATAKIWI KABISA KUISHI. SIJUI LILITUBU MAKOSA YAKE AU LILIENDA NA DHAMBI ZAKE!
 
Asante ma mdogo kwa info...hope mambo yatajifunua zaidi kwa kadiri siku zinavoenda...ni bahati mbaya kwamba kafia hotelini na huenda hatutajua chanzo halisi cha kifo chake ijapokuwa alikuwa na hayo matatizo kama ulivosema...ni nini kilisababisha presha/kisukari vipande?

...moja ya sababu kuu za kummaliza mtu mwenye kisukari n presha ni ongezeko la mapigo ya moyo[msukumo wa damu] ..inaweza kutokana.. TENSION[MAWAZO,KAZI NYINGI],MATUMIZI YA DAWA AU KITU CHOCHOTE KINACHOWEZA KU STIMULATE MAPIGO YA MOYO KUWA JUU[STIMULANTS]..Ie CAFEINE,VIAGRA ets
 
Hata maiti nitaishutumu tu hawa mafisadi ndio waliotufikisha huku tunako kwenda, wengine pesa ya kuiba ya walipa kodi wanaita vijisenti halafu ati wakifa tusahau, give me a break! wanaokufa Muhimbili kwa kukosa dawa ya kutibiwa ni akina nani? Wao kila uchwao ni matanuzi na matembezi ya kwenda kutibiwa Ulaya kama kawa acha wafe na siwezi kutoa hata chozi la damu kama lingeweza kutoka.

Hatuwezi kuwa na matabaka ati alikuwa kiongozi - kiongozi mwizi? Kwani tulikuchagua uibe. Huyu ndiye ndugu zake walipiga waandishi wa habari siku ya kesi yake na leo sisi ndio tuwe na huruma zaidi. Publically ameua na kutishia wananchi wengine na bunduki.

Same way as R. Mugabe ati akifa leo ubinadamu, huo ndio unafiki ambao hutuutaki limekufa liache life PERIOD! Na hii ni laana kwa mafisadi wote wataficha pesa lakini wataziacha hapahapa duniani. Leo hii meli iko njiani na silaha za kwenda kuua wananchi wasio na uwezo wa kujitetea, mbona Mwamwindi hakuna aliyemlilia? Acheni unafiki.
 
remmy ongala aliimba;

kifo kifo ,

kifo ungalikuwa unaonekana..

kifo ungekuwa tajiri sana..

kifo tungetoa rushwa ..

kusudi tuishi milelee.."

kifoo kifoo ,kifo ni kiboko yao..

kifoo kifo kifo ni koboko yetu!!!

Mungu ameweka fumbo kuu kwenye kifoo..pamoja na wazee wake yule fukara MBONDE ..kukubali rushwa ..wakakaa kimya..pamoja na MAHAKAMA kunyamaziswa..
MOLA naweza kutufundisha kuwa kama akiona tumeshindwa kutenda haki..basi hatakawia kutuonyesha.

hili ni funzo kwetu..tusitegemee mamlaka nyingine yoyote ya duniani..pale tunapowakosea wenzetu au kwa lolote..mamlaka pekee ya kutegemewa ni ile kuu ya MUNGU..mmoja!!!!!
 
Hivi habari hizi kuwa Ditto ni marehemu ni za kweli? mimi bado sijaamini,mazishi lini?
 
Back
Top Bottom