TANZIA Ukiwaona Ditopile afariki dunia

Poleni watanzania wenzangu kwa msiba huu mkubwa.

Nataka pia kumpelekea JK salaam za rambi rambi kwa kifo cha BEST MAN wake. Pole sana kaka.

Dito tutamkumbuka kwa mengi ambayo yametusaidia sana kujifunza na hivyo nisifungue mjadala juu ya marehemu.
Kawaida yetu sisi wabantu katika msiba tunajadili mema ya marehemu. Hii ni kwa lengo la kumpunguzia au kumwondolea mzigo huko aendako.

Sasa dadangu Kalumuna kafariki kabla hata hajafikia kuona bidii zake zikiwakomboa watanzania kweli?? Namjua kuwa ni mtu mwenye akili na anayejua kufanya mikakati. Lakini pia alikuwa ana hamu kw andani ya kutaka kuona nchi ya Tanzania na watu wake wakikombolewa kabisa. Labda alitaka siku moja aje kuwashtukiza CCM ili usaliti wake kwa chama ulete ukombozi moja kwa moja.

Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.
AMEN.
 
hnimeipokea habari kwa huzuni kubwa kama mtanzania ambae daima mioyo yetu hutakiwa kuweka mbele ubunaadamu kabla ya mengine

nnamuomba mola aipokee roho ya marehemu nakuiweka pahala pema peponi

na wafiwa mola wape moyo wa subira na kuwafariji

hatuitendei vyema familia ya marehemu dito na yeye mwenyewe kwa kumsubukua.


ss waislam kuna maandiko yanasema

" yakumbukeni mazuri ya maiti zenu na msiyataje mabaya yake"


tukiamini kila binaadamu ana mapungufu yake lkn wakati wa msiba si vyema kuanza kusobokoana
Mtu hukumbukwa kwa yale aliyoyafanya akiwa duniani. Ni vema sisi tulio hai tukayatengeneza maisha yetu kabla siku yenyewe haijafika, sala na maombi havitasaidia kutuweka pazuri kama maisha yetu hayakumcha Mungu wakati wa uhai wetu.

Mambo yake tuyataje ama tusiyataje hayatabadili kitu mbele ya haki! Na Mungu ndiye mwenye kutoa haki kwa kila mtu kwa matendo yake.

Binafsi ningependa binadamu wote tuishi milele, lakini hilo haliwezakani ila kwa Mungu pekee!!
 
[/SIZE]
Mungu alilaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen. Poleni sana wafiwa.
Tuwape pole wafiwa, lakini tusimfanyie Mungu maamuzi. Mtu anapokufa na kitabu chake kinafungwa. Mungu ndo anajua atamfanya nini marehemu na sio sisi kumwambia Mungu amfanye nini!!
 
Najua sio kawaida yetu kusema ukweli pale mtu anapokufa . Ila mimi binafsi nimesikitika kwamba haki haikutendeka kwa yule kijana aliyemuua . Inaniuma kwamba huyu mheshimiwa kifo kimemkuta uraiani ! Huyu mheshimiwa alitakiwa afie jela ....Why are we always trying to be political correct? it is about time now to start calling a spade a spade.
 
ditopile alikuja morogoro kuyatembelea mashamba yake, alishukia HILLUX HOTEL na ndipo mauti yalipo mkuta.aliugua ghafla akiwa hapo otelini na saatatu asubuhi aliaga dunia. tusimhukumu kwa aliyoyatenda enzi za uhai wake kwasababu yupo mbele ya hakimu mkuu.
MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU
 
Kutokana na ufisadi/kulindana kuwa kwenye kila kitu hapa bongo mimi nitaamini iwapo nitauona mwili wake,kwa sasa nachukulia habari hii kama yale yale ya ugonjwa wa Daudi Balali
 
fisadi limetangulia,kazi kwake na dereva wa daladala,mimi sina masikitiko juu yake lazima mtu uwe mkweli na sio kutimiza wajibu.
 
Najua sio kawaida yetu kusema ukweli pale mtu anapokufa . Ila mimi binafsi nimesikitika kwamba haki haikutendeka kwa yule kijana aliyemuua . Inaniuma kwamba huyu mheshimiwa kifo kimemkuta uraiani ! Huyu mheshimiwa alitakiwa afie jela ....Why are we always trying to be political correct? it is about time now to start calling a spade a spade.
 
Ni kweli huyu ndugu kwa sasa ni marehemu, ila kafia hotelini na si hospitali kama mtoa mada alivyosema. Mwili wa marehemu uko hospitali ya mkoa wa Morogoro.

Sijui kimemuua nini?
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana libarikiwe! Amen!

AMEFIA CHUMBANI ALIKOKUWA AMEPANGA KATIKA HOTELI YA HILUX. KILICHOMUUA HADI SASA HAKIJAJULIKANA LAKINI TUKUMBUKE ALIPOKUWA RUMANDE VIP SECTION YA PALE KEKO ALIKUWA ANADAIWA KUWA NA KISUKARI NA SHINIKIZO, YAWEZA KUWA MAGONJWA HAYO AU KINGINE. NA MENGINE ZAIDI NITAWAPATIA NIKIPATA ANY BREAKING NEWS KUHUSU KIFO CHA HUYU MUHESHIMIWA. TAARIFA ZINGINE ZA KARIBUNI ZASEMA JANA ALIONEKANA AKIRANDA RANDA MJINI MOROGORO NA GARI LAKE AKIONEKANA KUWA NA AFYA NJEMA HUKU GARI LIKIENDESHWA NA MDOGO WAKE MAREHEMU.
 
Ya Dito inasikitisha sana. Amefariki kwa shinikizo la damu leo saa mbili asubuhi akiwa hotelini, Morogoro, tena akiwa anaangalia TV.... mwili wake unasafirishwa leo mchana huu kuelekea Dar es Salaam ambako utapitishiwa hospitali ya jeshi ya Lugalo, kabla ya shughuli ya mazishi kuendelea nyumbani kwake Upanga, Dar es Salaam. Ina Lilalh Waina Ilaihu Rajiun

Tunaomba mwenye CV yake atuwekee hapa..


ahhhhhhhhhhhh umeanza vizuri then unaanza kuchafua sasa,iwekwe CV yake ili iweje mkuu? acha hizo,yeye ameshafika mbele ya haki,mie na wewe na wote tulobakia TUOMBE HUSNIL KHATMA full stop.
 
AMEFIA CHUMBANI ALIKOKUWA AMEPANGA KATIKA HOTELI YA HILUX. KILICHOMUUA HADI SASA HAKIJAJULIKANA LAKINI TUKUMBUKE ALIPOKUWA RUMANDE VIP SECTION YA PALE KEKO ALIKUWA ANADAIWA KUWA NA KISUKARI NA SHINIKIZO, YAWEZA KUWA MAGONJWA HAYO AU KINGINE. NA MENGINE ZAIDI NITAWAPATIA NIKIPATA ANY BREAKING NEWS KUHUSU KIFO CHA HUYU MUHESHIMIWA. TAARIFA ZINGINE ZA KARIBUNI ZASEMA JANA ALIONEKANA AKIRANDA RANDA MJINI MOROGORO NA GARI LAKE AKIONEKANA KUWA NA AFYA NJEMA HUKU GARI LIKIENDESHWA NA MDOGO WAKE MAREHEMU.

Asante ma mdogo kwa info...hope mambo yatajifunua zaidi kwa kadiri siku zinavoenda...ni bahati mbaya kwamba kafia hotelini na huenda hatutajua chanzo halisi cha kifo chake ijapokuwa alikuwa na hayo matatizo kama ulivosema...ni nini kilisababisha presha/kisukari vipande?
 
He got away with Murder (ok, maybe manslaughter because allegedly he recklessly handled a gun...) because he is the friend of the president, plain and simple...may he be judged where he is going,RIP
 
Asalamu alaykum.

Sote ni wa Mwenyeenzi Mungu na sote tutarejea kwake bila ya shaka.

Huyo ndugu yetu aliyetaka CV ya Marehemu pengine ana kazi muhimu au anataka kuandika some thing tusimlaumu moja kwa moja labda anataka imsaidie kwa kazi zake.

lakini upande mwengine ikiwa anaitaka kwa ajili ya kumuundua tu marehemu basi nadhani sio vizuri bora ndugu yetu uwache maama unajau sisi watanzania naona kama tunakwenda sehemu mbaya hivi sasa yaani tunasubiri mtu aje ndio tuanze kumsifu na kumkashifu bila ya kujali maumivu ya wale familia yao kwani kila binaadamu ana ndugu, jamaa, watoto hivyo kufanya vitendo kama hivyo tunakuwa tunawaumiza wafiwa mimi nadhani kwa maoni yangu tabia hii tuanze kuiwacha ingawa ni ngumu kwa wengine kuwacha lakini wajaribu kujiwekea mazingira ya kuheshimu wenziwao ili nao waje kuheshimiwa.
naomba kutoa hoja ingawa nilipotea kw amuda mrefu lakini sasa nimerudi inshaallah .
karibuni sana kijiweni kula orojo, badia na kababu.
stone towner.
 
Back
Top Bottom