TANZIA Ukiwaona Ditopile afariki dunia

Na mimi nimeisikia TBC-1 ila wamesema kafia hotelini alipofikia morogoro!
Mungu amlaze pema peponi na bila shaka watakutana na dereva wa daladala.Wasameheane ili utukufu wa mungu utawale.



Kazi kwa Brother Ditto watakapokutana na yule dereva maana sio ajabu ndie aliyepiga debe huko aliko kuwa Ditto naye amfuate.
 
Bro. Dito ametangulia, hakuna atakaye pona hii ni safari yetu zote hata na mafisadi...........

'Tulitoka kwa udongo, tutarudi kwa udongo" bwana alitoa na bwana ametwaa......
 
Wakuu,

Hii si mungeiacha kwenye siasa angalau kwa leo? Vinginevyo watu watakuwa wanakuja JF na kufungua threads mpya.
 
hnimeipokea habari kwa huzuni kubwa kama mtanzania ambae daima mioyo yetu hutakiwa kuweka mbele ubunaadamu kabla ya mengine

nnamuomba mola aipokee roho ya marehemu nakuiweka pahala pema peponi

na wafiwa mola wape moyo wa subira na kuwafariji

hatuitendei vyema familia ya marehemu dito na yeye mwenyewe kwa kumsubukua.


ss waislam kuna maandiko yanasema

" yakumbukeni mazuri ya maiti zenu na msiyataje mabaya yake"


tukiamini kila binaadamu ana mapungufu yake lkn wakati wa msiba si vyema kuanza kusobokoana
 
Ebwana hata mie nimekonfirm kwa washkazi wa bongo...apumzike kwa amani na mungu amuondolee zambi zake zote za hapa duniani palipojaa vishawishi....ameeeeeeni
 
habari ni kweli ila baba h kuwa na utu ss sio mahakimu cha msingi ni kumtakia mema mwenzetu sisi tiko kwenye safari na hatujajua mwisho wetu utakuwaje.

tumuombe mola atupe mwisho mwema hilo ndio la kuomba na sio kufurahia na kukejeli msiba wa mwenzetu
 
Mbali ya brother Dito ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo lakini pia kuna yule Binti Leocardia Kalumuna ambaye Gazeti la Mwanahalisi lilimuorodhesha kwamba aligawiwa "vijisenti" na Mzee wa suti za Ulaya Andrew Chenge, naye amefariki dunia usiku wa kuamkia jana mjini Morogoro!

kabla ya kifo chake Kalumuna alikuwa ni katibu wa Vijana wa CCM wilaya ya Mbeya mjini.Kalumuna ni rafiki wa Karibu wa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma na mbunge wa Iringa mjini monica mbega.

CCM ilimtegemea sana katika kuvunja mtandao wa Mwandosya mbeya na kabla ya kifo chake aliongezewa nguvu nyingine kwa kupelekewa katibu mwanamtandao na rafiki binafsi wa Emmanuel Nchimbi,Rhoda George kuwa katibu wake wa vijana wa CCM mkoa wa mbeya.
 
Yes Dito is no Longer in this world. May God Rest his Soul in Heaven.

Hapa ndipo bin adam tunatakiw akujua kuwa maisha ya hapa duniani ni mafupi.. ukiwa na nafasi ya kufanya mazuri kwa jamii fanya.. usiwe kama mzee wa Vijisent
 
Binadamu ni mavumbi,hawezi ishi milele,
Hata awe na vitimbi, au mpiga kelele,
mbele ya kifo hatambi,lazima aende kule
Tenda wema nenda zako, tukukumbuke daima!
 
Ya Dito inasikitisha sana. Amefariki kwa shinikizo la damu leo saa mbili asubuhi akiwa hotelini, Morogoro, tena akiwa anaangalia TV.... mwili wake unasafirishwa leo mchana huu kuelekea Dar es Salaam ambako utapitishiwa hospitali ya jeshi ya Lugalo, kabla ya shughuli ya mazishi kuendelea nyumbani kwake Upanga, Dar es Salaam. Ina Lilalh Waina Ilaihu Rajiun
 
Ni kweli huyu ndugu kwa sasa ni marehemu, ila kafia hotelini na si hospitali kama mtoa mada alivyosema. Mwili wa marehemu uko hospitali ya mkoa wa Morogoro.

Sijui kimemuua nini?

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana libarikiwe! Amen!
 
Back
Top Bottom