DIT VS COeT, UDSM!

kila jambo huanzishwa kukdh malengo fulan! thnk of long term planners and short term planners, c kwel kwamba BSc. in ....... eng. & BEng zpo sawa in terms of contents wanazofundshia au compitenc in solv'g problems within a related fields! wapo wanaoandaliwa kuwa short term problem solver na wapo wanaoandaliwa kuwa long term problem solver! dogo kabla haujaamua fanya juu chini upate PROSPECTUS(Muhtasar wa chuo huska) ili kujua contents za coarse unayotaka kusoma! hapo ndo utajua hatma yako whether to be short term problems solver au long term problems solver! we are not here to decide for you brother, tutakushaur nn cha kufanya ile uwe na maamuz sahh! be blessed then!!!
 
UDSM wakikutana na DIT wanakuwa wapoooole...ngoja wakutane na UDOM,TEK,TIA,MUCCOBS..mwe!mwe!mwe! hizo kelele chacha!

Mie ni experienced Engineer na niko kwenye uajiri pia,practically wote sawa hakuna tofauti kubwa coz ni tatizo la mfumo wa elimu,hata walimu wao wakija visiting kwenye industry huwa wanashangaa tofauti ya wanayofundisha na wanayoyakuta,but theoretically COET are better ukifananisha na DIT,naongelea Engineering level for both na sio otherwise.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wakuu vipi kuhusu MBEYA UNIVERSITY (MUST) hasa upande wa B Eng. Electrical & Electronics anayefahamu
 
UDSM iko juu ya DIT. Kwa kuwa zile Faculties ambazo kwa sasa ni colleges zinazotoa taaluma mainly chini ya UDSM.Sasa DIT kwa mfano haitoi uhasibu, uchumi, education, nk, haiwezi kuwa sawa na UDSM.DIT ni bora wakipambana na CoET kwa kutoa wahandisi watendaji na siyo wahandis wazungumzaji. Lakini pamoja na yote hayo, lazima graduate Eng ajengewe uwezo kwanza ndipo atafanya kaz, hii haijalishi katoka chuo gani. Zile desa hazitumiki kupata haya maghorofa na barabara, bali kuna njia za kitaalam zaidi ya nadharia zile za wahadhiri.
 
MUST n nzur sana kwa jins ya mpangilio wake wa coz ukilinanisha na udsm

Kweli hawa wasomi wetu wa leo,, Umeulizwa kuhusu MUST upande wa B Eng Electrical & Electronics pamekaaje,, unaanza kulinganisha Must na Udsm, msaidie kuhusiana na hiyo course sio kutoa comparison ya vyuo
 
UDSM iko juu ya DIT. Kwa kuwa zile Faculties ambazo kwa sasa ni colleges zinazotoa taaluma mainly chini ya UDSM.Sasa DIT kwa mfano haitoi uhasibu, uchumi, education, nk, haiwezi kuwa sawa na UDSM.DIT ni bora wakipambana na CoET kwa kutoa wahandisi watendaji na siyo wahandis wazungumzaji. Lakini pamoja na yote hayo, lazima graduate Eng ajengewe uwezo kwanza ndipo atafanya kaz, hii haijalishi katoka chuo gani. Zile desa hazitumiki kupata haya maghorofa na barabara, bali kuna njia za kitaalam zaidi ya nadharia zile za wahadhiri.

Mr chaza, Engineer ( Civil ) akishagraduate na kwenda kujiregister kama Graduate engineer, mda ule anasubilia kusajiliwa, anaruhusiwa kufanya kazi sehemu nyingine, au atakuwa anashughulika na Test na project anazopewa ili kumpima kiwango chake ili asajiliwe..natanguliza shkrani
 
Anaruhusiwa kufanyakaz kama Mhandisi, lakini chini ya prof engineer hasa inapokuja jambo linalohitaji maamuz, kisheria graduate engineer haruhusiw kufanya maamuz, hasa ukizingatia bado serikali haijakuamini na kupewa mihuri na leseni(Practising Licence). Kwa hiyo watu nawashangaa kwa ushabiki wa kitoto eti chuo fulani ni bora na kwa mfano mtu unaposema chuo fulani kinatoa short term na kingine long term engineers au sijui wengine engineer bora kwa kupitia diploma mara form6 ukijumlisha na miaka4 pale CoET ndo ubora. Hayo yote hayana msingi wowote.ERB hupima Wahandisi wake na kuwapa leseni na mihuri kwa kuangalia muda aliokaa kwenye field, miradi aliyoshiriki na ushahidi wa wahandisi waliomsimamia. Mara nyingi wahandisi washauri(consulting Engineers) lazima wathibitishe kwa kugonga mihuri yao. Ikumbukwe moja ya watu ambao wako strict ni Consulting Engineers, kamwe huwezi kuandika ripoti ya uongo ukadanganya kwa mfano ulishiriki ujenzi wa mliman city na BICO, Millenium towers mpya chini ya UNDI Consult, au mradi wa NORPLAN, COWI,NIMETA Consult au TanConsult,InterConsult na nyingine wakati hukushiriki, never huwezi kugongewa. Ni kwa umakini huu wa consulting firms ERB kamwe hawawezi kukusajili kama hujafanya kazi na hawa wahandisi washauri. Hakuna narudia hakuna chuo chochote ambacho kinatoa mhandisi bora eti kwa zile lecture notes na madesa, lazima uje mtaani upikwe upya. Kwa kumalizia, Engineer ni trainable person ambae anakua fit akipigwa msasa, ila huwezi leo kumaliza chuo fulani halafu ukapewa mradi udesign retaining wall, daraja au ghorofa 20 ikiwa na basementl,kamwe hutaweza,ila ukikaa kwenye game ukapikwa utaweza tu bila kujali umetoka chuo gani, na ndo maana ERB wanatoa practising Licence na siyo theoretical licence kama mdau mmoja aliposema UDSM ni bora theoretically than DIT. Engineering hasa ni Practical aporoach ili kitu kitokee kwa maana ni uumbaji ambao ni tofauti na ule wa Mungu muweza ambae yeye alitamka tu KUWA na kitu kikatokea. Engineering lazima ufanye ili kitu kitokee na siyo siasa.
 
Kwa hiyo Grad Eng anafanyakaz za kihandisi bila shida yoyote ila kisheria chini ya maelekezo ya Prof Eng, nikijibu swali lako Mr. Dansel
 
Chaza mashukuru kwa maelezo yako hakika yamenifumbua, Sasa naachana na ushabiki wa kitoto kuhusiana na chuo, Kinachohitajiwa ni kutoa wahandisi ambao wako fit sio waandisi wa kisiasa siasa.. Ningependa kujua wakati Graduate engineer anafanya kazi chini ya Prof Engineer inabidi huyo graduate awe anafanya kazi serikali au anaweza kufanya kazi katika private company?
 
Kwa hiyo Grad Eng anafanyakaz za kihandisi bila shida yoyote ila kisheria chini ya maelekezo ya Prof Eng, nikijibu swali lako Mr. Dansel

Hapo nimeanza kupata idea nzuri ya kiuhandisi. nashukuru sana.
 
Anafanya kazi popote, private na serikalini, na atalipwa mshahara kama kawaida kutegemea na scale za sehemu husika. Wakati akifanya anaweza kujiunga na mafunzo ya kujenga uwezo kitaaluma kwa wahandisi graduates,( SEAP Program), hii huwa ni miaka 3, na unatakiwa ujue mambo ya management angalau mwaka1, Maintenance angalau mwaka1 na design mwaka mmoja. Sasa uhandisi wenyew ni kusimamia miradi iliyofanyiwa design na wahandisi washauri( Consultants) yaani site/ field supervision. Je utaendelea kusimamia tu walicho design wahandisi washauri bila ya wewe mwenyewe kwenda kujua hiyo design? Ndipo ERB ikatoa sharti kuwa mwaka mmoja katika SEAP program lazima graduate Engineer aende kwa wahandisi washauri akashiriki kudesign yeye mwenyewe, badala ya kufanya vitu ambavyo tayar vilishabuniwa, na ERB wanajua chuoni huwez kujua hiyo actual design. Kwa hiyo unaweza kuandika ripoti ya SEAP ukiwa na mwajiri ambae ana prof Engineer ili akuidhinishie kuwa kweli ulifanya kazi site au ofisini na management ila kwa kuwaarifu ERB na kujiridhisha kama huyo prof Eng anavigezo na scope ya kazi inaendana na content ya ERB, vinginevyo watapendekeza sehemu za wewe kwenda kufanya kazi ili kumeet learning content. Ila inapokuja issue ya design, hapo lazima uombe kibali cha mwaka1 uende kwa Consulting Firms kama nilizokutajia kwenye thread ya mwanzo. Hivyo ubora wa Engineer kwa kiasi kikubwa unatokana na jinsi alivyopikwa na wadau. Kwa mfano Eng A kutoka CoET ameshiriki ujenzi wa uwanja wa Taifa, labda Mlimani City au mradi wa miundombinu mabasi yaendayo kasi hawezi kufanana na Eng B kutoka CoET aliyesimamia ujenzi wa bar, au madarasa ya shule ya msingi. Kwa hiyo ubora siyo chuo bali ni utaalam na changamoto
 
Asante Chaza na ubarikiwe, hivi ndo tunavyotaka na si comparison ya vyuo. safi hapa nafikiri ntakuja kuwa engineer mwenye malengo na si kujisifu eti COET yangu ni bora kuliko vingine .. Athante na uzidi kubarikiwa.
 
Ubarikiwe ndugu Dansel. Ikija tena mada nyingine ya kubishana kuhusu ubora wa vyuo vya Eng, we wakumbushe tu haya niliyoyaandika halafu watapima wenyewe, wewe unakaa pembeni.
 
Asante Mr. Chaza, hii ni kwa maanufaa ya wana Jf wote. Asante
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom