Kithuku, asante kwa dissertation hiyo japokuwa sijaisoma yote nimepitia kidogo. Nimekuta mapungufu mengi sana yakiwemo yafuatayo.
1. Sijaona mahala inapotaja ni dissertation kwa ajili ya ku-fulffil requirements za degree gani yaani kama ni ya uzamili au shahada au Udakatari wa falsafa.
2. Sijaona mahala alipotaja methodology yake zaidi tu naona ni simulizi na pia utaoji maoni kwa upande mmoja usiozingatia misingi ya uchambuzi yakinifu
3. Upangiliaji wa dissertation hiyo kwa ujumla umekiukwa. Sifahamu chuo anachosomea kama hakina standard formats za references, fonts n.k
4. Kama alifanya mahojiano na watu haoa aliowataja mwishoni mwa dissertation yake, alipaswa kuweka mifano ya instruments alizotumia pia kuweka copy kadhaa ya mahojiano na kama si yote.
Mapungufu ni mengi na nisingependa kwenda kwenye kipengele cha lugha maana tutakesha ila kwa ujumla huyu bwana amejitahidi mno ukizingatia hali halisi ya uandishi nyumabni.
Maswali haya sasa ni kwako wewe uliyetoa hii tasnifu ya huyo mhusika;
1. je, ulipata wapi hii dissertation?
2. Je huoni kama kuileta hapa ikiwa kamili na jina la mwandishi bila idhini yake au ya chuo utakuwa umekosea maana hii ni copyright property ya chuo na kuna utaratibu unaotumika kwa kupata documents kama hizi. Unless kama chuo alichosomea kimezianika kwenye mtandao wa kwao au mwenyewe aliamua kuianika.
3. Ulihitaji kupata mawazo ya aina gani kuhusianana na dissertation hii? Je ya kumsaidia huyu mwandishi au labda ya kuichanganua?