Disko la Mbowe litaokoa sokwe wetu na rasilimali za Taifa

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
MKUTANO WA CCM JANGWANI

Disko la Mbowe litaokoa sokwe wetu na rasilimali za Taifa?

Msomaji Raia
Toleo la 243
13 Jun 2012


MAKALA hii ilianza kuandikwa nikiwa katika jukwaa kuu la viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uwanja wa Jangwani, Jumamosi iliyopita.

Niliambiwa nikiwa pale kuwa, mpaka Ijumaa asubuhi ya wiki iliyopita, ilikuwa haijulikani ni nani atahutubia mkutano ule na ataongelea nini. Sekretariati ya CCM ilipoteza muda mwingi wiki nzima ikibishana juu ya ni nani asialikwe katika mkutano huo badala ya ni nani aalikwe na ahutubie nini.

Ubishi huo ulimuudhi sana mlezi wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam Abdulrahman Kinana na ndiyo maana alipokaribishwa ili kuwakaribisha mawaziri waweze kuzitolea ufafanuzi kero mbalimbali, alikuwa tayari amekerwa na mivutano ya chini chini, na akaishia kusema "hana muda wa kupoteza kuzungumzia siasa".

Kimsingi, mipasuko ya makundi ndani ya CCM inakiyumbisha kupita kiasi. Wale ambao hawakualikwa katika mkutano huo, au waliopendekezwa lakini wakakataliwa, wameapa kuandaa mkutano wao Kidongo Chekundu wakati wowote kuanzia sasa. Hiki ni kiwewe wala si mkakati wa kukirejesha chama katika misingi yake.

Mapema tukija uwanja wa Jangwani ilisisitizwa kuwa ni marufuku kwa watoa hotuba kurusha vijembe, kutukana wala kuwajibu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Nilisubiri kwa hamu kuona kama hiyo inawezekana ukitilia maanani kuwa palipo na Steven Wassira na Dk. Magufuli, lazima CHADEMA liwe somo kuu, na ndivyo ilivyokuwa siku hiyo.

Aliposimama Wassira haikuchukua dakika zaidi ya tatu aliishawarukia CHADEMA, na ndipo hapo nilimsikia Mzee Kinana akihema kwa tabu baada ya kusikia maneno ya kejeli yakirushwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Alipopanda jukwaani Dk. Magufuli ndani ya dakika tano za kwanza alikwishawataja CHADEMA mara saba.

Safari hii, labda kwa sababu kijembe chenyewe kilikuwa "rafiki" kidogo, Mzee Kinana hakushtuka sana, lakini makada wachache waliokaa jirani sana na jukwaa walisonya kwa uangalifu mkubwa sana. Funga kazi alikuwa ni Nape Nnauye ambaye aliamua kuwavalia njuga wana kikundi cha Uamsho cha Zanzibar akiwaita majambazi na wahuni wakubwa. Ndani na nje ya CCM, tabia ya viongozi wa CCM kurusha vijembe, kutukana na kubeza wapinzani haipendwi. Imekemewa lakini haiishi. Haiwezekani CCM ikaitisha mkutano kuwalaumu wapinzani kuwa wanaitukana CCM kisha hapo hapo na CCM ikatukana!

Mzee Wassira wiki iliyotangulia alitumia dakika 45 katika televisheni ya ITV akirusha vijembe. Pamoja na vijembe vyake, CHADEMA waliendelea na mikutano yao ukanda wa kusini na kujizolea wanachama wengi. Misingi ya CCM inazidi kutikiswa kutoka kwenye mashina, lakini mzee huyu anaona mkakati unaofaa ni kuendelea kuwarushia vijembe na kuwalaani viongozi wa CHADEMA. Hivi kumtukana ngedere anayekula mahindi yako shambani kweli inasaidia?

Hebu tuangalie kwa ufupi vijembe viwili au matusi aliyorusha Mzee Wassira pale Jangwani. Bila aibu usoni wala kusita alisema, Freeman Mbowe atapata "laana" kwa sababu hatambui kazi njema inayofanywa na CCM na ambayo baba yake Freeman (Aikaeli Mbowe) aliifanya pamoja na Baba wa Taifa (Mwalimu Nyerere). Akaendelea kusema kuwa, kama ameshindwa kazi ya siasa arudi katika biashara yake ya kuuza pombe na kupiga disko. Yote mawili hapo juu yalistahili katika mkutano wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam? Yawezekana, kwa kuwa kichwa kimejaa maneno na mdomo ukifunguka sharti maneno yatoke hata kama hayaeleweki.

Kwanza, nijuavyo si busara kumtumia marehemu kama shahidi katika utetezi wako. Steven Wassira anadai yeye binafsi anajua uhusiano wa karibu uliokuwapo kati ya Baba wa Taifa na baba yake na Freeman, ambao wote ni marehemu na hawana njia ya kuja hapa kututhibitishia kuwa walikuwa karibu kama Wassira anavyodai.

Pili, si kweli kuwa Freeman hatambui kazi njema ya CCM iliyofanywa na Baba wa Taifa akishirikiana na watu kama baba yake mzee Aikaeli Mbowe. Lakini, si kweli kuwa kazi hiyo ya Baba wa Taifa na Aikaeli Mbowe ndiyo hiyo iliyopo ambayo Steven Wassira anamlazimisha Freeman aitambue. Kazi hiyo njema, anaweza kuwa anaifahamu Wassira peke yake kwa sasa kwa kinachoonekana ni mabaki na masalia yanayotia uchungu kwa kila mtu aliyeifahamu Tanzania ya Nyerere na Aikaeli Mbowe.

Uchungu huo ndio unaoweza kuwa ulimfanya Freeman Mbowe kuacha hiyo "biashara ya pombe na disko" na kuingia katika siasa. Biashara hiyo ilikuwa inamnufaisha yeye Freeman peke yake na familia yake, lakini kazi ya siasa anayoifanya sasa, inawanufaisha Watanzania wote na raslimali zao. Disko la kisiasa analolicheza Freeman Mbowe kwa sasa, ndilo linalookoa raslimali zetu na wanyama wetu.

Kutokana na disko la kisiasa la Mbowe, sasa tunaona Wizara ya Mali Asili na Utalii inaanza kufanya kazi chini ya Balozi Kagasheki na wale wote waliokuwa wanauza sokwe wetu, twiga wetu, na faru wanacheza "muziki" usioitikiwa. Kwa disko la Freeman katika ulingo wa siasa, sokwe wetu watapona huko Gombe, faru wetu wa bei mbaya kutoka Afrika Kusini watakuwa salama, na twiga wetu wa Tarangire watazeekea mbungani.

Enzi hizi za utandawazi, mawaziri wetu na makada wa chama tawala wawe waangalifu sana katika kauli zao maana wanaweza kukitokomeza kwa kasi chama wanachodai wanakitetea. Haiwezekani waziri wa serikali inayoendeshwa kwa kodi za wananchi wote, akawa anatumia muda mwingi kufanya kazi za kiitikadi kuliko kazi ya utendaji unaopunguza kero za wananchi.

Mimi nadhani, ulikuwa ni mkakati mbaya sana kuwaburuza mawaziri wote wale pale Jangwani eti waje kufafanua jinsi wanavyotatua kero za wananchi. Matokeo ya mkakati huu mbovu, ilikuwa ni kichekesho waziri mmoja anasimama na kusema mambo ni mazuri kwa sababu serikali inafanya vizuri katika sekta fulani, lakini akisimama mwingine anadai sekta fulani imejaa madudu na mpaka anatoa namba yake ya simu ili watu wawasiliane naye moja kwa moja.

Kazi hii ya kushinda uwanjani kufafanua mazuri yasioonekana ya CCM waachiwe makada ambao ndiyo kazi yao, mawaziri waende wizarani wakafanye kazi na tuzione bila kuhitaji waje Jangwani kuhadithia. Watanzania si vipofu wa kutokuona mema yanayofanywa na CCM. Wakati CCM inafanya vizuri, ni wananchi hawa hawa walikuwa wanatunga nyimbo kuisifia bila kulazimishwa, bendi za muziki zinatunga nyimbo bila kulazimishwa na hata wananchi wanaandamana wenyewe kuunga mkono au kupinga jambo fulani.

Hatukuhitaji polisi kutupa vibali au kutukataza na wala sikuwahi kumwona Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi wala Benjamin Mkapa akilazimika kuwaita mawaziri eti waje jukwaani kujibu hoja za wananchi. Chema hakihitaji kunadiwa, kinajinadi chenyewe na hakihitaji kutetewa kwa vijembe wala matusi.

Baadhi ya mawaziri nilioongea nao pale jukwaani walisema wazi kuwa huu mkakati hawaupendi kwa sababu unawachonganisha na wenzao ambao hawakuitwa na hata wale waliotaka kuja wenyewe baadhi yao wamezuiwa kwa sababu za kimakundi. Haiwezekani Maprofesa kama Tibaijuka na Maghembe waburuzwe jukwaani kuanza kueleza mambo ambayo hayajapikwa sawa sawa ili kumridhisha Steven Wassira na Nape kuwa wanakitetea chama.

Mahali CCM kilipofikishwa na uzembe wa kutokuchukua hatua, hakihitaji mikutano ili kukitetea. Ni chama chenye dola, chenye bajeti, na ridhaa ya wananchi. Kinapaswa kutenda kazi bila kumwangalia "nyani wala sokwe" usoni kisije kikamhurumia. Ni chama ambacho kinatakiwa kizinduke na kuachana na dhana ya sasa ya "utawala bora" au "utawala wa sheria" ambayo kimsingi inawalinda majizi na mafisadi.

Chama hakilazimiki kukumbatia watu hawa kwa sababu, kuwa mwanachama wa CCM si suala la haki ya kibinadamu. Ni suala la mtu kufuata misingi na imani ya CCM, vinginevyo, vyama ni vingi si lazima mtu abaki CCM.
 
Kifo cha mchawi huwa na mbwembwe na maneno mno!magamba yanakufa sasa,japo yanakukuruka hayataki kufa kimyakimya kama CUF bara!lakini msishangae ndio aina ya vifo,mwengine atakukuruka kidogo na kujamba hapa na pale kama wachawi lakini wengine ufa bila mateso kama wasabato
 
Safi sana. Umeandika ukweli mtupu, usiochanganywa na chembe chembe za uongo wala unafiki.
 
safi mkuu....! hawa jamaa hawakusema walicho ahidi bali walikuja na ahadi kama wapo kwenye kampeni...! 2015 is around the corner tukawazke vizur...!
 
Vizuri kamanda ungesikia na kile kituko cha kampeni za Arumeru mashariki yale matusi ndo ungechoka kabisa lakini
hii inaonesha ni type gani ya viongozi tulionao ,tuliowachagua na tunaowaamini .
 
Acheni unafiki. Ulichosema kinajulikana. Acha siasa za CDM hapa.

kimba la kijani wewe kifupi wannchi walikeleka upumbavu wenu wa jangwni,mnapiga kampeni za kikwete kwa mara ya pili wakati mlishachakachua matokeo alafu mnaongea pumba majukwaani kama magufuli,mwakyembe,nape na wasila kifupi mnapelekwa lekwa kama mambuzi na cdm,moto uliowaka kuuzima ni ndoto kufeni kimya kama mtatilo na cuf yake.
 
Nampa hongera mwandishi kwa uchambuzi wake wa kina, nimependa sana avivoandika kwa umahiri na upeo mkubwa. Huu ni ukweli kwa CCM kwamba inaweza kurudisha imani ya wanachama wake na sisi tuliohama tukarudi, tena wenyewe bila kulazimishwa kinachotakiwa ni effective and serious govenment.

CCM isiitukane Chadema ila ijitukane yenyewe kwa sababu imeshindwa kuwa na serikali yenye utendaji na ufanisi. Imetuundia serikali ya wahuni, mafisadi na wezi wa rasilimali za nchi yetu. Isitulazimishe sisi tuone kwamba ni chama kilichounda serikali nzuri acha tuseme wenyewe. Mbona tunakubali kwamba baadhi ya mawaziri wanafanya kazi nzuri!
 
Huo huo mziki (Disko) wa mbowe ndio tunaupenda na tunaucheza, CCM hana mziki
 
Nimeishia kusoma hapa baada ya haya maneno yako kuniudhi. HIVI WEWE CHIZI KUVAA MAKANINI, MAWINGU, MAKAKI, MATAIRI YA GARI NA KWENDA KUPANGA FOLENI YA KUNUNUA SABUNI NA CHUMVI ALIYOTUACHIA NYERERE NA BABA TAKE MBOWE NIYAKUJISIFIA? Rubbish.
MKUTANO WA CCM JANGWANI

Kazi hiyo njema, anaweza kuwa anaifahamu Wassira peke yake kwa sasa kwa kinachoonekana ni mabaki na masalia yanayotia uchungu kwa kila mtu aliyeifahamu Tanzania ya Nyerere na Aikaeli Mbowe.
 
Back
Top Bottom