Disemba 9 kila mwaka: Tunasherehekea uhuru wa nchi ipi?

hapa ni uelewa tatizo viongozi wetu wanakurupuka wanaona aibu kusema tanganyika kwani wataonyesha utengano

Ni nchi gani lilpata uhuru desemba mosi 1961????
Je Tanzania imetokana na nini?
Je Tanganyika ndo Tanzania siku hizi?
Nini asili ya jina Tanzania???

Of all the People Nisimuone Nape katika maazimisho hayo, sababu alipata kusema yeye hajui Tanganyika ni kitu gani.........
Pili Itabidi mgeni rasmi aliweke wazi suala hili la kuwa tunaadhimisha miaka ya taifa lipi........wanaweza wakaona ni jambo dogo lakini kumbe ni kati ya mambo yanayopelekea taifa kutojielewa...its a psychological thing

Nchi moja ina katiba 2, serikali 2, Marais 2, Mambunge mawili -- Kazi kweli kweli. Pia tuna majeshi mawili- JKU na JKT, tuna Ikulu mbili, Polisi mdebwedo na Polisi wezi wa maiti montuary, hivi karibuni tutakuwa na Mahakama Mbili -Kadhi na mahakama walarushwa. Kazi kweli kweli.

Tanganyika ilizaliwa 9th Dec, 1961. Baadaye ikaungana na Zanzibar kufanya muungano wa Tanzania. Serikali ya Tanganyika iliunganisha kwenye serikali ya muungano, kwa hiyo hapo tunasherekea Uhuru wa Tanganyika ambayo ni Tanzania vilevile. Tar 26.04.2014 tutasherekea Muungano wa Tanzania na wala siyo Uhuru wa Tanzania. Kwa kifupi Tanganyika ilipata jina la Tanzania, lakini umri unabaki palepale. Kuna Uhuru wa Tanzania na Muungano wa Tanzania.

Hivi kumbe historia imebadilika siku hizi? Ni kweli kuwa Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuunda Tanzania ambayo ni ufupisho kutoka katika majina mawili ya nchi zilizoungana. Lakini hili la kuwa uhuru wa Tanganyika ndio uhuru wa Tanzania mimi sijawahi kulisikia kwani Tanzania haijawahi kupata uhuru bali ni muungano wa nchi mbili ambazo kila moja ilipata uhuru kivyake na kwa tarehe yake. Kwa ufupi hakuna uhuru wa Tanzania kwani haijawahi kupata uhuru.

Ni nchi gani lilpata uhuru desemba mosi 1961????
Je Tanzania imetokana na nini?
Je Tanganyika ndo Tanzania siku hizi?
Nini asili ya jina Tanzania???
• Nchi iliyopata uhuru Decemba mosi 1961 ni TANGANYIKA
• Tanzania ni muungano wa majina mawili taani TANganyikaZANzibarIA
• Tanganyika ni sehemu ya Tanzania na herufi zake tatu za mwanzo zilichukuliwa kuunda jina la Tanzania.
• Asili ya jina la Tanzania ni muungano wa majina ya TANGANYIKA na ZANZIBAR.

• Nchi iliyopata uhuru Decemba mosi 1961 ni TANGANYIKA
• Tanzania ni muungano wa majina mawili taani TANganyikaZANzibarIA
• Tanganyika ni sehemu ya Tanzania na herufi zake tatu za mwanzo zilichukuliwa kuunda jina la Tanzania.
• Asili ya jina la Tanzania ni muungano wa majina ya TANGANYIKA na ZANZIBAR.

Mkuu hayo majibu uliyoyatoa ni ya Kisiasa Zaidi na inakuwa ngumu kuweka katika ukweli,
Unapoitaja Tanzania unakuwa umeunganisha Tanganyika na Zanzibar, ambapo hakuna uhuru wa nchi inayoitwa Tanzania bali tunakuwa na siku ambayo Tanzania ilizaliwa kwa maana ingine siku ya muungano.
hiyo tisa december ni uhuru wa Tanganyika ambapo wanasiasa hawataki kusikia hilo neno Tanganyika.

Mods..naleta hoja mbele yenu ya ku-sticky hoja hii. Nawaomba mfanye hivyo! Kinachojadiliwa hapa ni ukweli mtupu! There is no tanganyika, ilizikwa tarehe 26.4.1964, ni mawili,either tusherekee (kwa huzuni) kumbukumbu ya miaka 50 ya uhuru wa tanganyika iliyokufa au turudishiwe tanganyika yetu kamili bila longolongo!

Hii kazi kweli kweli, kwahiyo ikifika tareh 26.04.2014 ni miaka 50 ya muungano.

Sasa bendera gani itakayopandishwa wakati wa sherehe, Tanganyika
Wimbo gani wa miaka 50,
raisi gani atakaekuwa mgeni wa heshima. tanganyika haina raisi
Mafanikio gani yatazungumzwa, tanganyika

Na wewe unaesema ati tunachokoza muungano, ufikie kikomo sasa, kwanini zanzibar ina state na Tanganyika haina
Nani aliyeafiki?
Sisi wengine tulikuwepo, lakini hatukushirikishwa
Msituchukulie poa

Shere hiyo ifutwe, La siku hiyo state ya Tanganyika itambuliwe, na bendera yake , na wimbo wake wa Taifa.
Tanganyika = Tanzania? Dont fool anybody.

Hapo hapo,je bendera ya Tanganyika ndiyo hiyo inayotumika kama ya Tanzania?Wimbo wa Tanganyika ndiyo unaotumika kama wimbo wa Tanzania ya sasa?Katiba ya Tanganyika iliwahi kuwepo maana Zanzibar walianza na presidential decree,je katiba hiyo inafaa?

WANA JF nakumbuka wakati ninasoma UDSM niliwahi ongea na kujadiri kitu kuhusu Tanganyika lkn ndugu zangu wanafunzi wengi waliniita mimi msaliti na mkabila mpaka wakarefer kabila langu. Sasa LISSU msishangae anapoambiwa maneno kama hayo.

Kiufupi Tanganyika ilikufa na hakuna watu wa Tanganyika labda Watanzania Bara, je hii ni sahihi? IKUMBUKWE TULISHANGILIA SANA KUZALIWA SOUTHERN SUDAN, LINAPOKUJA KWETU BASI TUNAONA TABU, POLITICAL HYPOCRACY.

Haya tunayoyashuhudia leo ni matokeo ya udikteta wa Nyerere ambaye watu wameaminishwa kwamba ni baba wa taifa. Je ni taifa lipi? Kama ni taifa la Tanzania kwa nini Karume naye asiitwe hivyo? Muungano haukutokana na matakwa ya watu wa Tanganyika wala wa Zanzibar, hapakuwa na kura ya maoni bali ni makubaliano tu ya Nyerere na mwenzie Karume.
Kwa nyakati zile inawezekana kuwa wazo la muungano lilikuwa sahihi lakini kwa mwenye upeo hata wa wastani tu anajua kuwa leo muungano hauna tija. Ni ujinga wa kupindukia kwa wanasiasa wa hovyo wa Tanganyika kufanya jina hilo lionekane kama jinai kulitamka na badala yake watu wamezoezwa kusema Tanzania Bara wakati Zanzibar wanatumia jina lao lilelile.
Ni mawazo duni kuamini kuwa eti muungano ukivunjika hatutakuwa salama, nani ana ushahidi wa hilo? Wala hakuna haja ya serikali mbili wala moja wala tatu; Tanganyika turudi kuwa nchi yetu na Zanzibar waendelee na ya kwao, ubaki ushirikiano wa nchi jirani. Inashangaza ukienda Zanzibar unakuta wana mifumo na taasisi zao aidha tofauti na za kwetu au zinazolingana na za kwetu halafu watu wenye akili timamu bado wanazungumza kana kwamba hii ni nchi moja.
Lazima Watanganyika tudai jina letu, bendera yetu, wimbo wetu wa taifa na nembo ya jamhuri yetu. Muungano ni sinema tu ya mchana, hakuna kitu kama hicho ndiyo maana hata Vasco da Gama akienda kule visiwani ni kama kiongozi tu wa nchi jirani amepita kuwajulia hali, hana mamlaka yoyote.
Naamini itakuwa vyema zikipatikana bendera ndogo za Tanganyika tuzipepee siku ya uhuru.

Hapa wanasiasa wanatudanganya. Kuna haja hili nalo kuwaeka ktk katba mpya. Tanzania haijafikisha 50yrs.

Hapo sasa! kutokana a muundo wa muungano wetu haitakiwi kabisa tusherehekee sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika kwa sababu hakuna nchi Tanganyika kikatiba...Hivyo kwa kila siku tunayosherehekea inaonyesha CCM wanaitambua Tanganyika lakini hawataki kuipa Uhuru wake kama nchi.

Hawa jamaa bado hawajajua ni nin kinaendelea uku chin walipo wananchi.kama wanajua shingo zao ni ngumu lazima zitajavunjika tu.but nataka watu wajiulize maswal haya.KWA NINI WAZANZIBAR HAWATAKI MUUNGANO,NA KWA NIN VIONGOZ WA TANGANYIKA WANAUTAKA UONGOZ KWA NGUVU ZOTE.SOMETHING MUST BE WRONG SOME WHERE? Coz Also AMONG ZANZIBAR LEADERZ WANAUNG'ANG'ANIA MUUNGANO,SASA JE WAO HAWAJAONA YALE AMBAO WENZAO WAMEONA? NA KWA NINI WATU WASIKAE CHINI YAN WANANCH WOTE WAKATATUA MATATIZO YA MUUNGANO WAO WANATAKA UVUNJIKE? Ask urself usikurupuke

Kuna umhimu sana wa kukaa chin na kurekebisha,kwa hili wasitudanganye miaka 50 ya uhuru wa Tanzania hailet sense

Tulipozaliwa tuliitwa TANGANYIKA baadae tukabatizwa TANZANIA!

Siikubali hoja hii miaka 50 ya nini? niliwahi kuuliza hapa:
Tanganyika 1961-1964 (2.5yrs)
Tanzania 1964- to date(47.5 yrs)
HAMSINI siioni

Una hoja ya msingi, lakini simpo mathematics ukihesabu miaka hamsini kufikia Desemba 9, 2011 unajua ni nchi gani inazungumzwa. Tusichokoze Muungano.

Hapo kwenye bold, Kamura- Tusiwe watu wa kukubali kila kitu kinachosemwa kwa kuogopa kuchokoza kitu fulani. Unaweza ukaogopa kuzungumzia mapungufu ya Muungano wetu leo lakini kesho ukalia kwa matatizo yatakayosababishwa na Muungano huo ulioulinda 'usichokozwe".

Tulipokuwa tunahoji kwa kuandika na kuzungumza kuna watu wakatuona kama machizi. Kwa kuwa wamekataa kusikiliza na kuelewa ngoja waje waipate aibu kubwa.

Tanzania haikuwa kuwa koloni la nchi yoyote. Kama vile ilivyo Ethiopia. Hivyo haiwezekani kutangaza uhuru. Ikifanya hivyo sisi wenye akili tutawauliza, ni nani aliyewatala, aliyewakandamiza hata sasa mnataka kuwa huru?

With Tanganyika, yes! She was once the colony of German and then Britain. December 9, 1961 she declared Independence from British rule.

Napita tu. Nitakuja.

Back
Top Bottom