Tanganyika ilijifia wakati wa muungano 1964 na toka wakati huo hakuna nchi kama tanganyika in short ile sehemu ya nchini inayojulikana kama tanzania bara katika katika katiba ya sasa ilisurrender sovereignity yake na ndio maana hata kwenye katiba huwezi kukuta neno Tanganyika.
Mkuu,
Tukirudi kwenye kuungana, uhalisia tunajua kuwa Tanganyika na Zanzibar waliunaganisha baadhi ya mambo tu, siyo yote...Jee kulikuwa na umuhimu wa ku-surrender sovereignity yote? mbona Zanzibar waliendelea kushughulikia yale mambo yao ambayo amabyo hayakuwa ya muungano.
Nafikiri sababu ya Mambo ya Tanganyika kushughulikiwa na Bunge na serikali ya Muungano kwa sababu aliyoitoa Mwalimu ilikuwa ni kuepuka gharama ya kuwa na serikali tatu na hilo lilikuwa Rahisi kutendeka kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa Rais wa Tanganyika na pia alikuwa Rais wa Muungano... na aliendelea kuwa hivyo mpaka alipoona mambo magumu, nchi inatokomea kwenye umasikini na ufukara, akaamua "kung'atuka". Lakini kila aliyehoji kasoro za Muungano katika utawala wake alionekana kuwa ni mhaini.
Hivi ni sheria ipi ilifuta nchi ya Tanganyika na nani aliidhinisha kifo hicho?