Disco la nguvu la kesha siku mbili mfululizo MAKABURINI!!

Hiyo nayo ni moja ya sherehe kubwa saaaana ambazo kila mwanadamu lazima apitie. So, sometimes ni vyema kusherehekea badala ya kuomboleza!!

Ash to ash... Dust to dust...

Kama vile dar haiishiwi na vituko wiki iliyopita kulitokea msiba wa kijana mmoja anayetajwa kuwa ni mdogo wa mkurugenzi wa CLUb KAKALA pale Kigamoni! Kituko cha aina yake kilikuwa ni pale maandalizi ya kuchimba kaburi maeneo ya magogoni karibu na Mikadi Beach, ndipo mziki wa disco ambao hutumika pale club ulipopelekwa makaburini sambamba na generator la uhakika na vinywaji vya kufa mtu! Watu walikula na kunywa mpka siku mbili bila disco kuzimwa, kaburi lichimbwa likajengewa mbarumaru kwa ndani na bada siku mbili ndipo mwili wa kijana yule ukahifadhiwa pale! Binafsi nilishindwa kutafsiri aina hii mpya ya msiba!
Kibongobongo ukiona hivyo kuna mtu anaingiza pesa nzuri tu, kupitia kwa marehemu

people die''kama wakikupigia disco wao na laana zao we yako yaliisha cku ulipokata roho''hafu nini cha ajabu watu wanakufa kabla wewe hujazaliwa sasa cha ajabu kiko wapi?? we kufa tunafunga mziki makaburini na sie tunangoja ya kwetu'.

SAFI SANA!! Hiyo ndo hata mimi nataka nikifa!! Nitaacha funds kwa ajili hiyo tu, mambo ya kulia lia ya nini?

aliikufa kwa nini? Huenda kaugua kwa muda mrefu sana kiasi ambacho alikuwa kisha anza kuwafilisi... Hapo wakashangilia kwa disko la haja mrija wa kukimbiza utajiri na mali umekatika
alikuwa ana ngangania mali ,hivyo tuligonga moja moja ,mbili mbili na kisha tukahakikisha kafukiwa?

wamekoseaaaa
......... wangeleta mabinti wa pale manzese na buguruni.......WANAZIKA HUKU WANALAMBANA

Kama vile dar haiishiwi na vituko wiki iliyopita kulitokea msiba wa kijana mmoja anayetajwa kuwa ni mdogo wa mkurugenzi wa CLUb KAKALA pale Kigamoni!

Kituko cha aina yake kilikuwa ni pale maandalizi ya kuchimba kaburi maeneo ya magogoni karibu na Mikadi Beach, ndipo mziki wa disco ambao hutumika pale club ulipopelekwa makaburini sambamba na generator la uhakika na vinywaji vya kufa mtu!

Watu walikula na kunywa mpka siku mbili bila disco kuzimwa, kaburi lichimbwa likajengewa mbarumaru kwa ndani na bada siku mbili ndipo mwili wa kijana yule ukahifadhiwa pale!

Binafsi nilishindwa kutafsiri aina hii mpya ya msiba!

niliwaona pale Kigamboni nikiwa nakwenda Gezaulole kwa kijana wangu, nilidadisi nikaambiwa kijana aliefariki alikua ni kila kitu kwa wazazi wake, miaka ya mwanzoni mwa 2000 , alikimbilia South Africa. . . Akarudi anaumwa hapa Tz miaka 2 iliyopita, kisha miezi kadhaa nyuma alionekana kule Loliondo, Then baada ya hapo hakuwa na maisha marefu.
Baada ya kufariki wazazi wakaamua kutumia raslimali labda ndio zingekua urithi wake.. . . Kufanya boonge la party. . .

Kummbe ndio maana hata wachaga wa dar ssiku hizi wakifiwa wanaulizia wapi kuna mbege inaletwa pipa hata kama umefia masaki/osterbay

sio ajabu labda kwa mlio mjini sehemu kama ujaluoni ni kawaida sana watu wanaselebuka tuu kunywa mpaka kuchee,binafsi nilihswahi kuhudhuria kilio cha rafiki yangu mjaluo huko musoma nilishangaaa tuu ikabidi nitulie ilikua vigumu kukubaliana nao lakini ndo utamaduni wao ,kweli zunguka uone mengi,mlio mjini mmezoea ya kimjini mjini tuuu ,ila wakikupa sababu kwa nini wanafanya hivyo wako sawa wengine mnasindikiza kwa kuomboleza wengine wanasindikiza kwa furaha ni part ya maisha style utakayotumia haiwezi badili chochote kama imeshatokea

Back
Top Bottom