Mkoroshokigoli
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 14,594
- 5,568
Ukishakuja kwenye suala la utawala bora,kwakweli hata hao viongoz hawajui,wao wanasema utawala bora ni uwazi na utawala wa sheria,hawataji principles nyingine za utawala bora,na bahat mbaya miongoni mwa wananchi ndo hatujui kabisaa UTAWALA BORA,wananchi wanautamani 2015 kwa kuneemeka na fulana,pilau na pombe,Sisi watanzania tuna elimu ya viwango tofauti lakni kuwepo kwa elimu hiyo hatuna elimu ya utawala bora. Leo hii ukiwaambia wananchi wenye shida ya maji, umeme na miundo mbinu wamuulize kiongozi wao maswali, hakika wengi watatoa pongezi.
Mgombea akisimama jukwaani anajinadi nitawajengea barabara, maji nitawaletea na umeme mtapata. Hakuna wa kumuuliza utafanya hayo yote kwa pesa yako au ya wananchi? Hakuna wa kumuuliza kuwa atatumia mbinu gani kupunguza ukali wa maisha japo kidogo, tunatoa kodi kubwa je, inamalengo yapi kwa taifa?