DIDEO : CCM Vipande vipande huko Dodoma

Wed

JF-Expert Member
Mar 7, 2011
315
266
Baada ya kushindwa uchaguzi Mkuu, CCM sasa yaamua Kutoana macho huko Dodoma. Hebu jiulize :

1/ Kama kweli CCM ilishinda uchaguzi Mkuu mbona sasa wananyoosheana vidole na kupigana huko Dodoma ?
2/ Kama kweli timu ya Makamba iliweza kushinda uchaguzi na kumrudisha Kikwete madarakani mbona Makamba anafukuzwa pamoja na kuvunjwa kwa Kamati Kuu na Secretarieti Kuu kwa kile wanachokiiata wenyewe Utovu wa "Nithamu na Maadil" wakati wengine wakiita kujivua "Magamba" /au/ Makamba ?? (ha ha ha)

2/ Kama kweli CCM ilishinda umea wa jiji la Arusha kwa kuwa na Quoram inayohitajika : mbona wameshindwa sasa kupitisha bajeti ya jiji la Arusha kwa kudai ati hawana quorum ya kutosha kwa sababu CDM wamesusia ushiriki ??
Je, quorum waliyokuwa nayo yakumchagua meya, sasa imekwenda wapi ???? Kama wanayo, siwapitishe bajeti ??

Hivi kweli CCM inathani watanzania ni wajinga kiasi hicho ??

Nimesikia huko Dar, CCM imekokotoa watoto na kuwajaza kwenye ukumbi ili wawazomee wachangiaji !!!! Kule Libya Gadafi naye amelipa mamluki wampiganie ili abaki madarakani. Haya sasa Nani anavunja amani Tanzania ?? Tusubiri tena kudanganywa kwamba ati CHADEMA ndo wanaovuja amani. Ha ha ha, hapa .... Mimi nasubiri

YouTube - Viongozi wa CCM wanajipanga upya yasababisha wengine kuachia ngazi
 
  • Thanks
Reactions: Zed
Huyu jamaa alijua udhaifu wake ndio maana akaendelea na ccm mbovu.angekuwa imara baada ya kunusa harufu ya mabadiliko angefanya kama Bingu wa Mutharika kule Malawi....kinachofanyika sasa kimekawia mno na hakitabadilisha harakati wala mioyo ya watanzania
 
hahaaa JK bana...haya tungoje nini kitaendelea baada ya hapa..lakini kwa sie wapenzi wa mpira ukisikia timu beki zinakatika basi ndo hapa sasa..yaani beki hazikabi kabisaaaaa
 
Maji sasa yamewafika Shingoni. Moto uliowashwa na CDM hautazimika mpaka tumeikomboa Tanzania kwenye makucha ya mafisadi. Lazima kuhakikisha kwamba Kila mtanzania, kila mtoto anayezaliwa, anaishi mahali pazuri na anaheshimika kama mtanzania. Sera za CCM zimekabithi rasilimali za watanzania mikononi mwa mafisadi wanaoendelea kupora mali zetu !! CDM go, we need a total liberation of our beloved country !
 
Unajua Mzee Makamba na timu yake hawakuwa watu wema kwa CCM, na JK, walimdanganya kwa kubeba watu kwenye malori na kumwambia eti Mzee hawa watu wooooooote wamekuja kukusikiliza wewe katika kampeni zako, kumbe maskini watu walikuwa wanaambiwa twendeni kunamsanii anaimba anaitwa Ma,.....,,...lo, na mwingine komedi, basi wananchi maskini ambao huwa wanawasikia tu redioni au kwenye tv mbao basi wanajichukulia usafiri, na JK anaona kweli watu wanamkubali kumbe kunauozo, JK cha maana asimame peke yake, afanye maamuzi yenye utashi wake,
 
hahaaa JK bana...haya tungoje nini kitaendelea baada ya hapa..lakini kwa sie wapenzi wa mpira ukisikia timu beki zinakatika basi ndo hapa sasa..yaani beki hazikabi kabisaaaaa

teh teh teh.....unamaanisha beki zinakatika kama zilivokatika ile jumatano pale darajani?
 
asante chadema kwa mchango wako mkuu,asiye ona wala kuskia ana tatizo la akili! Binafsi nilitaka hao vilaza wa ccm waendelee kuwepo ili tuizike haraka kabla ya 2015.......viva chadema
 
aaaaaaaaaaaaaah mods vipi yaani hata neno mkw.ere mnali-sensor? msifanye hivo bwana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom