Dida wa Mchops matatani kwa dawa za kulevya

Dida alikamatwa majuzi (Jumatatu) na wanausalama wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, akidaiwa kumeza dawa za kulevya, tayari kuzipeleka sokoni nchini China.

Akipiga stori na gazeti hili, Dida ambaye kwa sasa yupo nje kwa dhamana alisema kuwa, tukio la kukamatwa kwake ni njama za mwanamke aliyemtaja (jina tunalihifadhi) ambaye alikuwa na ugomvi naye siku nyingi zilizopita hadi kufikia hatua ya kufikishana polisi.

“Kila kitu nakijua. Hizo ni njama za kunimaliza, lakini naamini kwa uwezo wa Mungu nitashinda,” alisema Dida na kuongeza:

“Tuliwahi kugombana naye (jina tunalihifadhi) hadi kufikia hatua ya kunipeleka polisi na kunifanyia mambo ya kifedhuli sana, kisa alidai eti mimi namchukulia mume wake ambapo tulikuwa marafiki wa kushibana.”
Hata hivyo, Dida alisema kuwa, alishangaa kuona anashikwa mkono na mtu asiye mfahamu Uwanja wa Ndege na kuambiwa kuwa, yuko chini ya ulinzi kwa kufanyiwa upekuzi wa kina kwa tuhuma za kuwa na dawa za kulevya.

“Ni kweli nilikuwa chini ya ulinzi, najua ni mbinu za watu wasiyopenda maendeleo yangu wanabaki kila kukicha wananitafutia matatizo kinguvu ili yanikute, na ni juhudi zangu za maisha ndizo zinazonifanya niwe na maadui wengi,” alisema Dida.

Aliendelea kusema kuwa, siku hiyo ya tukio baada ya kuachiwa huru, alipata habari kuwa, kuna mtu alipiga simu kwenye kituo hicho cha
Ndege akitoa taarifa kuwa, Dida anasafiri siku hiyo na achunguzwe kwa makini kwani huwa anakwenda China kwa ajili ya kupeleka dawa za kulevya.

“Eti nichunguzwe kwa makini kwa sababu huwa nasafirisha dawa za kulevya kwa kumeza. Mtu huyo alijifanya ananijua vizuri mimi,”alisema Dida.

Kwa mujibu wa habari hizo, uchunguzi wa awali aliofanyiwa mrusha sauti huyo kwa kutumia haja kubwa ulionesha hakuwa na dalili za mihadarati tumboni.

Hata hivyo, Dida yuko nje kwa dhamana uchunguzi zaidi ukiendelea na huku akiwa amekatishwa safari yake ya nchini China.


the saga continues
 
Amah kumbe huwa wanasafirishaga pia toka huku. Basi mawazo yangu mimi mbwiga ni kuwa madawa ya kulevya huingizwa tu nchini yaani sisi Tanzania tu watumiaji au soko kumbe nasi tunauzaga?? Asa wanazitoa mkoa gani au ni bangi ndo zinazofungwa katika vikete?. Nisaidieni tafadhali
 
Amah kumbe huwa wanasafirishaga pia toka huku. Basi mawazo yangu mimi mbwiga ni kuwa madawa ya kulevya huingizwa tu nchini yaani sisi Tanzania tu watumiaji au soko kumbe nasi tunauzaga?? Asa wanazitoa mkoa gani au ni bangi ndo zinazofungwa katika vikete?. Nisaidieni tafadhali

...hahahaha acha maswali ya kimbwiga mkuu.
Umeona wapi jani likafungwa ktk kete?
hapa kwetu pamoja na kwamba ni warehouse ya sembe bali pia ni transit prot njema tu.
Hebu naomba ushahidi kama upo wa kuharibiwa kwa madawa yaliyowahi kukamatwa na kesi zake kutolewa maamuzi.... hapo ukishikwa unakuwa umewapa mtaji wadau wengine.
Dah kweli kweli
 
...hahahaha acha maswali ya kimbwiga mkuu.
Umeona wapi jani likafungwa ktk kete?
hapa kwetu pamoja na kwamba ni warehouse ya sembe bali pia ni transit prot njema tu.
Hebu naomba ushahidi kama upo wa kuharibiwa kwa madawa yaliyowahi kukamatwa na kesi zake kutolewa maamuzi.... hapo ukishikwa unakuwa umewapa mtaji wadau wengine.
Dah kweli kweli

Aksante ukweli nilikuwa mbwiga katika hilo. Sikuwa najua kuwa tunatranst hapa . Aksante mkuu kwa kunipatia mwanga.
 
wamemuoneaa kabisaa...na anatakiwa adai fidia na hao askari njaa pale uwanjanii wanasubiriaa kupewa tip za chuki na uongo watu wanaonea wivu mitaani huko labda ana kabiashara kake anasafiri kwenda china ......kuchukua vitu labda vya dukani au biashara....wanaona kama mwenzaoo ameshayatoaa hapana ni kupambana na umasikini tuu kila mtu ajitahidi kuchakarika tu...hata kama ni huyo bwana wake..labda ameachwa au amezidiwa na wenzake kitaaani anaanza kuleta wivu wa kipumbavu...lazima wamlipe..gharama ya kumchafulia jina kwenye jamii......pole sana dida....fundisho kwa askari njaaa pale uwanjani....
 
Nauliza kesi ya DIDA iliishia wapi? pia mwenye picha ya dida ( Hadija Shaibu) atuwekee hapa tumwone
 
Utakuta marafiki zake wa karibu ndio walio mchoma,marafiki siku zote ndio maadui zako,sababu wanajua kila kitu chako na sio wote wanayoyapenda maendeleo yako,wanataka mbaki sawa siku zote ili msipate hata wakuwasaidia!!
 
alikuwa na balaa huyu naye, china wakikukamata wanakunyonga. wanigeria wengi sana wananyogwa kila mwaka china believe me
 
Ok basi nakuletea mazingaombwe, click hizo sentensi zenye maandishi mekundu na blue utamuona.
dida.jpg

heee!!! kumbe ni mama mzeee kwa umri, pengine miaka 50+
 
Back
Top Bottom