Dida wa Mchops matatani kwa dawa za kulevya

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
975
47
Mtangazaji matatani kwa dawa za kulevya

na Happiness Katabazi

MTANGAZAJI wa Redio Times FM, inayomilikiwa na Kampuni ya Bussiness Times Ltd, Hadija Shaibu, maarufu kwa jina la ‘Dida wa Mchops’ anashikiliwa na askari wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya cha Jeshi la Polisi baada ya kumshuku kuwa anasafirisha dawa za kulevya.

Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zilizolifikia Tanzania Daima Jumatano, zilieleza kuwa Dida alianza kushikiliwa juzi baada ya askari wa kitengo hicho waliopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kumkamata wakati akijiandaa kupanda ndege kwenda China.

Habari zilieleza kuwa Dida alikuwa akijiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopian Air Line, lakini polisi walilazimika kumtia nguvuni baada ya kumpeleleza kwa muda mrefu na kuhisi kuwa huenda siku hiyo alikuwa amemeza dawa hizo ili azisafirishe nje ya nchi.

Zieleza zaidi kuwa baada ya Dida kukamatwa, alipelekwa kwenye choo maalumu kilichopo uwanjani hapo ambacho hutumiwa na askari wa kitengo hicho kuwahifadhi watuhumiwa wanaowakamata wakiwa wamemeza dawa za kulevya kwa muda ambapo endapo mtuhumiwa alikuwa amemeza dawa hizo atazitoa wakati akijisaidia.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa tangu alipoingizwa kwenye choo hicho juzi jioni hadi jana saa nne asubuhi, hakuweza kugundulika kuwa na dawa hizo tumboni ambapo alichukuliwa hadi makao Makuu ya Kitengo hicho, huko Barabara ya Kilwa kwa ajili ya kuhojiwa.

“Nakuhakikishia kuwa jana (juzi) tulimkamata Dida pale uwanja wa ndege, alikuwa akielekea China kwani tulikuwa tukimshuku kuwa amemeza dawa hizo lakini hadi hivi ninavyoongea na wewe yupo mikononi mwetu ila hatujamkuta na pipi hata mmoja.

“Tumemleta hapa ofisini kwetu Kilwa Road kwa ajili ya mahojiano zaidi na tayari mama yake ameishafika na tunaendelea kuchukua maelezo yake ila kwa sababu bado ni mchana ni mapema kukuhakikishia kuwa tutamalizana naye leo au la,” alisema mmoja wa maofisa wa kitengo hicho.

Taarifa nyingine zilizopatikana jana jioni zilieleza kuwa Dida alidhaminiwa jana majira ya saa kumi jioni.

Hata hivyo alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Godfrey Nzowa, ili aweze kuthibitisha taarifa hizo alishindwa kukubali au kukataa na badala yake akaishia kusema atafuatilia.

Hivi X-ray isingeonyesha kuwepo au kutokuwepo kwa hivyo vitu? Hivi kwa nini wamsubiri mpaka avitoe kwa njia ya kawaida? Kama havipo, watamsubiri mpaka lini? Hivi tutafika kweli kwa uchunguzi kama huu?
 
Mastar wengi wa hapa bongo wanauza na kusafirisha unga. hapa kwetu kinondoni unga unapatikana sana karibu kila pap unayoiona ni kituo cha unga. polisi wanakuja wanachukua chao wanaondoka.
 
...huwa wanasubiria avitoe kwa njia ya haja kubwa.... huwa wanaepuka sana kutumia exray sijui kwa nini? labda wanapenda kuona matokeo ya matumizi ya njia ya haja kubwa.... (kwi kwi kwi)
 
ma dear ones';haya ya huyu binti ni njaa ya usalama wa taifa,,tena cha kusikitisha aliemchoma alikuwa bwana wake yuko kitengo cha mbwa airport sasa sijui watamweleza nini kama wamekosa hizo dawa na wamemnywesha uji ambao hajui kama wameka nini;
nafikiri kunahitajika umakini zaidi na si kukamata ovyo kwa starehe
 
umh! kweli masuala ya upelelezi tupo nyuma ... aibu tupu.
 
ma dear ones';haya ya huyu binti ni njaa ya usalama wa taifa,,tena cha kusikitisha aliemchoma alikuwa bwana wake yuko kitengo cha mbwa airport sasa sijui watamweleza nini kama wamekosa hizo dawa na wamemnywesha uji ambao hajui kama wameka nini;
nafikiri kunahitajika umakini zaidi na si kukamata ovyo kwa starehe

wow now i can understand the power of love.
ila kama hayo madawa yakikosekana ktk belly yake (hata ya kubambikiza maana mwela wa bongo ni experts kwa kubambikia) itabidi awe considered ktk kusafishwa. Unajua mbwembwe za kumkamata mtuhumiwa bongo hazina adabu wala utu kabisa.

Akikutwa nazo basi ndo tuseme atakuwa ameongeza CV yake ktk jamii.

..Najiuliza harakaharaka je huyu ni mmojawapo mwa wale waliokuwemo ktk orodha ya muungwana?? kwa hiyo ni miongoni mwa vigogo au naomba mnipe elimu kuhusu watuhumiwa vigogo....
 
MTANGAZAJI wa Redio Times FM, inayomilikiwa na Kampuni ya Bussiness Times Ltd, Hadija Shaibu, maarufu kwa jina la ‘Dida wa Mchops’ anashikiliwa na askari wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya cha Jeshi la Polisi baada ya kumshuku kuwa anasafirisha dawa za kulevya.

Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zilizolifikia Tanzania Daima Jumatano, zilieleza kuwa Dida alianza kushikiliwa juzi baada ya askari wa kitengo hicho waliopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kumkamata wakati akijiandaa kupanda ndege kwenda China.

Habari zilieleza kuwa Dida alikuwa akijiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopian Air Line, lakini polisi walilazimika kumtia nguvuni baada ya kumpeleleza kwa muda mrefu na kuhisi kuwa huenda siku hiyo alikuwa amemeza dawa hizo ili azisafirishe nje ya nchi.

Zieleza zaidi kuwa baada ya Dida kukamatwa, alipelekwa kwenye choo maalumu kilichopo uwanjani hapo ambacho hutumiwa na askari wa kitengo hicho kuwahifadhi watuhumiwa wanaowakamata wakiwa wamemeza dawa za kulevya kwa muda ambapo endapo mtuhumiwa alikuwa amemeza dawa hizo atazitoa wakati akijisaidia.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa tangu alipoingizwa kwenye choo hicho juzi jioni hadi jana saa nne asubuhi, hakuweza kugundulika kuwa na dawa hizo tumboni ambapo alichukuliwa hadi makao Makuu ya Kitengo hicho, huko Barabara ya Kilwa kwa ajili ya kuhojiwa.

“Nakuhakikishia kuwa jana (juzi) tulimkamata Dida pale uwanja wa ndege, alikuwa akielekea China kwani tulikuwa tukimshuku kuwa amemeza dawa hizo lakini hadi hivi ninavyoongea na wewe yupo mikononi mwetu ila hatujamkuta na pipi hata mmoja.

“Tumemleta hapa ofisini kwetu Kilwa Road kwa ajili ya mahojiano zaidi na tayari mama yake ameishafika na tunaendelea kuchukua maelezo yake ila kwa sababu bado ni mchana ni mapema kukuhakikishia kuwa tutamalizana naye leo au la,” alisema mmoja wa maofisa wa kitengo hicho.

Taarifa nyingine zilizopatikana jana jioni zilieleza kuwa Dida alidhaminiwa jana majira ya saa kumi jioni.

Hata hivyo alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Godfrey Nzowa, ili aweze kuthibitisha taarifa hizo alishindwa kukubali au kukataa na badala yake akaishia kusema atafuatilia

wanandugu haya mambo yataisha lini;mmemkamata hana mnavyotaka;
labda mkipata habari zaidi town ni kwamba huyu binti alikuwa naliwa na usalama mmoja alikuwa kitengo cha mbwa;baadae wakakorofishana kama binadamu wengine;sasa aijulikani jamaa aliamua kuwasha moto ama lah;ukweli halisi binti hana mzigo na jamaa wameanza kutafutana wenyewe hapo uwanjani kazi kwelikweli;'''''''''in short hawa usalama ndio wanaopitisha watu na mpaka wameingia kwenye ndege wanageuka na ndio wanaowapokea hawa watu wakitoka nje ndio maana ukiona ndege za EMIIRATES;QATAR NA KENYA AIRWAYS MARAMOJAMOJA WANAKUWA MBOGO KAMA WAMEMWAGIWA MAJI
pole binti;nafikiri sheria ifwate mkondo wake
 
itabidi alipwe gharama zake kama polisi hawajabaini dawa kwa mshukiwa wao pia wamuombe radhi mbele ya uma wa watanzania kwani hadhi yake katika jamii imeshuka ukizingatia kazi na umaharufu aliokuwa nao noma sana pia chuki zawana
 
Ebwanaeh duh!

......
wanandugu haya mambo yataisha lini;mmemkamata hana mnavyotaka;
labda mkipata habari zaidi town ni kwamba huyu binti alikuwa naliwa na usalama mmoja alikuwa kitengo cha mbwa;baadae wakakorofishana kama binadamu wengine;sasa aijulikani jamaa aliamua kuwasha moto ama lah;ukweli halisi binti hana mzigo na jamaa wameanza kutafutana wenyewe hapo uwanjani kazi kwelikweli;'''''''''in short hawa usalama ndio wanaopitisha watu na mpaka wameingia kwenye ndege wanageuka na ndio wanaowapokea hawa watu wakitoka nje ndio maana ukiona ndege za EMIIRATES;QATAR NA KENYA AIRWAYS MARAMOJAMOJA WANAKUWA MBOGO KAMA WAMEMWAGIWA MAJI
pole binti;nafikiri sheria ifwate mkondo wake.....

Sweetbaby
umeongea kwa uchungu sana nimejitahidi kukuelewa ila kuna details naomba uzimwage hapa ili kuwekeza nyama ktk hoja yako.
nakushauri pangilia tena VINA na MIZANI kisha mwaga hoja hapa. Hakuna wa kumwogopa maana USALAMA wameishika nchi mpaka haipo salama tena.
 
Mastar wengi wa hapa bongo wanauza na kusafirisha unga. hapa kwetu kinondoni unga unapatikana sana karibu kila pap unayoiona ni kituo cha unga. polisi wanakuja wanachukua chao wanaondoka.

Karibu janvini naona weye ni mgeni hapa, labda nikufahamishe hapa ni a place where we dare to talk openly sasa tutajie majina ya hao mastaa iliuokoe maisha ya vijana wenzako wanaoharibika na matumizi ya madawa haya huko mtaani. Kusema tu mastaa ni generalisation ambayo inaweza kukuharibia reputation yako hapa JF. Na kila Pap ndio nini au Pub? na zenyewe zianike hapa halafu tuone kama wataziacha na hao polisi kama watakuwa wanachukua chao. Usipo wataja nakuachia wewe mwenyewe uamue upo upande gani wetu au wao..
 
Kama hawatamkuta na madawa namshauri adai fidia polisi bilion 5
 
..wakimkuta nazo wamdai fidia ya kiwango gani?? hasa kuwatibu wale vijana walioathirika na traficking-service yake.
 
Mkuu nyie hamjui kuisaidia polisi?Yule wamemshuku akinya hewa basi kapona.
 
..wakimkuta nazo wamdai fidia ya kiwango gani?? hasa kuwatibu wale vijana walioathirika na traficking-service yake.
List ya wauza madawa mheshimiwa rais KIKWETE alishasema anayo kwa nini asiwape hao polisi
 
Mnaosema mtuhumiwa asipoonekana na dawa za kulevya alipwe fidia..Sikatai alipwe fidia lakini si kwa fedha zetu walipa kodi. Inabidi hao askari wasofanya homework zao vizuri ndo wakatwe kwenye mishahara yao ndo wajue uchungu wa uzembe wao.
 
well said
na iwe fundisho kwa wazembe wengine wote ktk idara zote
 
Nchi yetu ina matatizo,hadi wanaona aibu maana dada wa watu wamemsumbua na kumharibia ratiba zake kwa taarifa za uongo.Sasa itabidi wamlipe garama zote!! Pole sana dada yetu!! Ni kweli umewaonyesha ulivyo msafi,hawatarudia tena!!
 
Back
Top Bottom