Diana chilolo aomba uenyekiti wa CWT

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Na
Nathaniel Limu, Singida


JUMLA ya wanachama wanne wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) mkoani Singida akiwamo Diana Chilolo, wameomba nafasi ya uenyekiti ngazi ya mkoa kupitia jumuiya hiyo.

Chilolo ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, anatetea nafasi yake ya mwenyekiti wa UWT.

Wengine wanaoomba nafasi hiyo ni Esta Masinga, Sundi Samike na Pendo Kone.

Akizungumza mjini hapa jana, Katibu wa UWT Mkoa wa Singida, Sija Lukwale, alisema nafasi ya uenyekiti kwa upande wa Manyoni imeombwa na Elizabeth Bajile, Neema Mwitizi na Mwanahawa Yusufu.

"Waliomba nafasi hiyo ya Mwenyekiti UWT Singida Vijijini ni Christina Jambi, Hadija Kissuda, Salma Kundya, Neema Ipande na Amina Ititi. Wilaya mpya ya Ikungi walioomba ni Theresia Nkuwi, Christina Hamisi na Helena Ayubu," alisema Sija.

Aliwataja Jenifa Miana, Hawa Athumani na Neema Imari kuwa wameomba nafasi ya uenyekiti wa UWT Wilaya ya Iramba wakati nafasi hiyo katika Wilaya mpya ya Mkalama, imeombwa na Elipendo Machafuko, Mariam Kahola na Magreth Kinota.

"Katika nafasi hii ya uenyekiti wa UWT wilaya na mkoa, wagombea watachujwa na vikao husika kwa ajili ya kubaki na wagombea watatu tu," alisema.

Alisema uchaguzi wa nafasi hizo utafanyika mara uchujaji wagombea utakapomalizika.

Aidha, alisema nafasi ya mjumbe wa Baraza Kuu Taifa CCM kutoka Singida, imeombwa na Theresia Nkuwi, Fatma Toufiq, Duda Mughenyi na Hadija Majii.

Alisema nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa imeombwa na Sarah Mkumbo, Mwajuma Shaha na Hadija Majii.


Chanzo: Mtanzania
 
Wengine wanaoomba nafasi hiyo ni Esta Masinga, Sundi Samike na Pendo Kone.

Hongera Mzee Parseko KONE
 
Diana Chilolo, una vitumbua vya kutupa wana-Iramba??....chaguzi ni CDM bwana, huku CCM ni mwendo wa vitumbua tu
 
Mgombea Uenyekiti wa UWT std VII?

Diana Chilolo kiboko, Mkoa hauna wakina mama wasomi mpaka std vii anarudia tena kugombea nafasi hiyo?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom