Diamond amchana baba’ke

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108

Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’.

Abdul Juma.
Erick Evarist na Gladness Mallya

SIKU chache baada ya kuibuka kwa baba aliyemlea Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ aitwaye Abdul Juma na kudai kuwa mwanaye huyo amemtelekeza na hamjali, mwanamuziki huyo amemchana mzazi wake huyo, Ijumaa lina kitu kamili.

Akizungumza redioni kupitia Clouds FM, Jumatatu wiki hii, Diamond alidai kushangazwa na mzazi wake huyo huku…



Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’.

Abdul Juma.
Erick Evarist na Gladness Mallya

SIKU chache baada ya kuibuka kwa baba aliyemlea Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ aitwaye Abdul Juma na kudai kuwa mwanaye huyo amemtelekeza na hamjali, mwanamuziki huyo amemchana mzazi wake huyo, Ijumaa lina kitu kamili.

Akizungumza redioni kupitia Clouds FM, Jumatatu wiki hii, Diamond alidai kushangazwa na mzazi wake huyo huku akimtaka kuacha kusema maneno hayo kwani siyo mazuri.

Huyu hapa Diamond ambaye kwa sasa yupo juu kuliko msanii yeyote Bongo kimuziki:
“Kiukweli ni vitu ambavyo mimi vimenishangaza sana kwa sababu sijui chochote na nisingependa nisikie suala la mzazi

wangu kusema mimi ni mtoto wake, sijui nini na nini kwamba mimi nafanya starehe sihusiki na yeye, siyo kauli nzuri kiukweli, ina maana ananijua kwamba mimi ni mwanaye baada ya kuwa Diamond?

“Siku zote kama alijua mimi ni mtoto wake, basi angenisomesha na kunipa elimu nzuri, lakini nilihangaika na mama yangu mzazi (Sanura Khassim ‘Sandra’) akanikuza na kunisomesha kwa shida na tabu zote mpaka leo nimekuwa hivi nilivyo,

nisingependa kumsikia mtu yeyote anaongea kwamba mimi ni mtoto wake au yeye ni nani kwa sababu siku zote hawakuonekana, wasitake kuonekana kipindi cha masilahi, mtu ndiyo anajifanya anahusika sana na mimi kama mtoto wake.

“Haya mambo nilianza kuyasema toka nilipotoa single (wimbo) ya Binadamu, sikujua hata kama leo ningekuja kuwa na Prado (gari alilonunua juzikati la zaidi ya Sh. milioni 60), makazi (anajenga nyumba Tegeta, Dar na tayari imetumika Sh. milioni 69)

au kuwa na haya mafanikio mengine, baba yangu ataendelea kuwa baba yangu tu ila siwezi kumpa kipaumbele kama ninachompa mama yangu kwa sababu kama angetaka hilo angenijali toka mapema.

“Mimi nilikuwa napenda kusoma na nilikuwa nafanya vizuri kwenye masomo yangu, lakini sikuwa na uwezo wa kifedha kuendelea kusoma, mzazi wangu alikuwa na fedha, ina maana angenijua mimi angenisomesha, leo ningekuja kuwa hata

mbunge au waziri kwa sababu mimi najua nina upeo mkubwa sana wa kielimu na vitu vingine, sasa nimesota na muziki halafu leo ndiyo wanajitokeza.
“Sitaki, naomba waniache na mama yangu mzazi,” alitiririka Diamond.

TURUDI KWA MZEE ABDUL TENA

Baada ya kutoa maneno hayo makali kwa mzazi wake huyo, Ijumaa lilizungumza na mzee Abdul ambapo alisema kwa kifupi bila kufafanua: “Basi sawa siyo mwanangu.”
AKUMBUSHWA YA KANUMBA

Kwa mujibu wa mashabiki wa staa huyo mkubwa wa Bongo Fleva waliozungumza na Ijumaa juu ya sakata lake na baba huyo walimtahadharisha kwa kumkumbusha hali ilivyokuwa kwa marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ na baba yake mzee Charles Kusekwa.

“Platnumz anatakiwa amalize suala hili kwa sababu nafikiri anakumbuka malumbano ya Kanumba na baba yake ambayo hayakuwa mazuri,” alisema Luda wa Kinondoni, shabiki namba moja wa Diamond.

TUJIKUMBUSHE

Wiki mbili zilizopita, mzee Abdul aliibuka na kuliambia gazeti ndugu la hili, Amani, kuwa Diamond ni mwanaye lakini hamjali na badala yake amekuwa akiponda starehe.

BADO UTATA

Hata hivyo, wiki moja baadaye ndugu wa Diamond waliibuka na kudai kuwa mzee Abdul siyo baba halisi wa msanii huyo bali baba halisi ni Idd Salum, ambaye alifariki mwaka 2004 ambapo Platnumz hakufafanua suala hilo. Global Publishers
 
Baba majukumu siyo baba jina, baba hajitambulishi bwana anatambulishwa na majukumu anayofanya
 
sasa huyu mzee keshapotezewa bado anamng'ang'ania Diamond inakuwaje? si apotezee tu mpaka anaanzwa kupondwa hadharani na mtoto mdogo yeye acheki ustaarabu wake
 
Huyu Platnum anakoelekea siko....is same way na ile ya The Great...ukiwa maarufu usimkane mzazi wako hata kidogo, tena in public...hata kama unasimamia ukweli lakini sio vizuri kabisa!! Recall it.
 
Angekuwa ni baba mzazi wala asingeenda kwenye vyombo vya habari bali Diamond angetutambulisha sasa hapa tunaona baba maslahi tu...diamong kasema ukweli aachwe kwani yeye hakuwa funguka na kulalamika kuwa baba hakumtuza bali dingi ndo kalianzisha..." ACHA NOMA NA IWE NOMA"
 
siyo busara kukana, hata kama cyo baba yake au hajamsomesha.ingekuwa vyema akae kimya kulinda heshima yake na huyo anayejiita baba yake.
 
We dayamondi, ni rahisi sana. Waambie hao mapararazi mambo yetu ya kifamilia tutayamaliza kifamilia. Nawasihi mtumie busara walau kidooogo.
 
We dayamondi, ni rahisi sana. Waambie hao mapararazi mambo yetu ya kifamilia tutayamaliza kifamilia. Nawasihi mtumie busara walau kidooogo.
 
Luck Dube alifanya hivi na Baadae akaanza kumlilia Baba yake...

Daddy popote ulipo Remember me...
you left for the city Many years ago and you promise to come back...

Asije pata Radhi kama yule Mzenji Kule Uturuki
 
na iwe fundisho kwa wanaume wote wanaotelekeza watoto....wakifanyikiwa mnawafuata midomo mbele....
 
Sawa sawa. Kama radhi zitampata yeye kwanza aliyeanza kukutelekeza. Mungu ni wa wote si wa baba tu.
 
Habari zilizotufikia ni kwamba msanii Diamond ni mgonjwa na yuko hospitali haijajulikana ni nini haswa kinamsumbua. Tutazidi kuwaletea habari kadri tutakavyo kuwa tunazipokea.


diamond is sick.jpg


1.jpg


2.jpg

kweli laana ya siku hizi ni kufumba na kufumbua mkuu.

Sawa sawa. Kama radhi zitampata yeye kwanza aliyeanza kukutelekeza. Mungu ni wa wote si wa baba tu.
 
Watu mnakazana na neno laana, kwa nini msiseme amelaaniwa baba yule amtelekezae mwanae!
Huu ni ufinyu wa mawazo kabisa, baba yangu alinitelekeza lakini hakuwahi nitamkia hadharani kuwa mimi si mwanae na hata kama aliwahi mtamkia mama sijawahi kuambiwa! waligombana na mama kwa sababu za kipuuzi nimehangaika na mama na kusoma hadi kupata mwanga. japo sina mapenzi ya baba, na msaada niutoao kwa mama si ule niutoao kwa baba lakini baba hajawahi niitia magazette.
Sisemi kwa kuwa baba yangu ni bora sana, ila naweza sema pamoja na umaskini wake anatumia hekima na busara kuishi na watotos japo wote wapo mbali.
Huyu anayejinasibu kuwa baba diamond alipaswa amalize hizi tofauti kifamilia na kuomba radhi kwa mwanae. magazette yanamdanganya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom