Diamond, Ali Kiba na mtu wa tatu

Naam hawa wapo vizuri sana, huyu Dimpoz kuna wakati alikuwa anamkaribia sana Diamond ila sijui kwa sasa amekosea wapi!
Anagombana na mamemanager wake mara kwa mara ndo maana ana drop nowadays
Ay
Mubenga
wamemtema dogo anajiona star eti na yeye anamsimami nedy music
 
Kwa sisi watu wa Hip hop tunaamini mtu wa kwanza ni Fid Q.....ila katika hawa wawili wanaovuma ni kwa sababu ya nguvu kubwa ya watu wazito na wenye pesa walio nyuma yao na team pia.
Fid q hamuwezi yule jamaa aliyeimba perfect comb
 
Samahani mkuu naomba kukuuliza,hivi hao madogo Baraka na Abdukiba unaosema "vijana wa " kiba una maanisha nini sijakuelewa .............???
Baraka yupo chini ya uongozi mmoja yeye na Kiba, Rock star......Abdul ni ndugu yake Kiba wa tumbo moja hivyo kuna ukaribu mkubwa.
 
Kwa sisi watu wa Hip hop tunaamini mtu wa kwanza ni Fid Q.....ila katika hawa wawili wanaovuma ni kwa sababu ya nguvu kubwa ya watu wazito na wenye pesa walio nyuma yao na team pia.
Fid ni local zaidi.
 
yaani umeongea kitu cha msingi sana, hao wengine hata wapige ngoma kali vipi watu wanawaanhalia hao tu namba 1 na 2


Kwangu Mimi namba 3 ni Vanessa au Navy Kenzo ( kimtazamo Wa kimataifa)
Ni kweli jamaa wanafanya vema kwa sasa.
 
Dimpoz ni kweli alikuwa na potential ya kuwa 'Top Player' kwa kipindi kile, ila tokea alipotoa Angela Graph yake ikaanza kushuka. Ben Pol ni msanii mkali ila hana potential ya kuwa Top Player kwenye muziki
Umenena vema mkuu.
 
Niliposoma swali kwenye title yako, nilifikiri unamaanisha mtu nyuma ya bifu yao, Mara nyingi issue kama hizi huwa zinatengenezwa kwa manufaa ya kibiashara zaidi, panaweza kuwa hakuna tatizo wala uhusiano mbaya kati ya watu hawa wawili, lakini panatengenezwa issue kuwa hawaelewani ili kuweka majina yao katika midomo ya watu na kutengeneza team za kiuhasama kwa lengo la kibiashara.

Mara nyingi washabiki na wana team wanakuwa hawajui lolote nyuma ya pazia, mtu anaweza mpenda mmoja wao sababu tu eti yule mwingine ana maringo, wengine utasikia mimi napenda tu mziki wa fulani bila kujali ubora wala umahiri katika kazi, Nilisikia mwingine akisema " Mimi nampenda fulani kwasababu tu ni mpiganaji na mbunifu katika maisha". Mwingine anampenda fulani kwa uvaaji wake tu, Mwingine kwa muonekano wa mwili wake tu.

Siku bahati mbaya ikatokea watu hawa wawili wakakutwa pamoja wakicheka na kufurahi pamoja au wakaamua kufanya kazi pamoja, huu ndo utakuwa mwisho wa kambi zao mbili na mwisho wao hao wawili utakuja haraka sana. Kazi ya mtu wa tatu( invisible person) ni kuhakikisha hali inabaki kama ilivyo kwa gharama yoyote, wana habari wamekuwa wakitumika bila kujua katika kufanikisha haya.
 
Back
Top Bottom