Diamond akataa hela ya Wema stejini...

Mkare_wenu

JF-Expert Member
Mar 11, 2011
1,714
442
Check:



26.JPG

...Diamond aliendelea kuwajibika huku Wema akijaribu kumbembeleza

30.JPG

Pesa alizokataa kuzichukua zikiwa zimetupwa
 
Last edited by a moderator:
Jamaa yuko busy na kuimba pamoja na kucheza..
watu wanaweka fedha chini... ili kumuumbua tu dada wa
watu ikabidi waongeze chumvi eti kakataa. Wa Bongo bana..

Kuna mtu anauhakika Diamond alirudisha hiyo fedha kwa Wema?
 
Namuona kama anaangalia ya kuchukua ila ataachaje wakati wema kaweka nyingi sana
 
Kinyamwezi angepokea halafu kama mikausho baadae!hizi ni dalili za wivu diamond kaonyesha cuz kabla wema hajaenda dubai katika show ya PHD alimmwagia sana hela HEMED, mastory yakamfikia nasib!!!hela haisuswi na demu si wa kushindana nae!!mistake kubwa anafanya platinumz
 
aaaah ahhh wema alivyopotezewa akajikuta kama pedesheee akawa anamwaga pesa zake bt diamond kafnya vzuri snaaaaa ajaja ple kwa vijiset vyke
 
Kweli kazi.... watoto wa kiume ndio wanadengua kiasi hiki siku hizi? kweli usharobaro sio jambo zuri.... Au ndio ''Sizitaki Mbichi Hizi''
 

Attachments

  • Wema na Diamond.jpg
    Wema na Diamond.jpg
    12.3 KB · Views: 527
dogo mshamba kweri kweri....otherwise aseme alikuwa busy kucheza na hakuona haja ya kupoteza stepu na kuchukua hela....

shori kajikakamua kichizi kumtunza dogo...mshamba sana huyu dogo kudadadadeki..

 
Last edited by a moderator:
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Diamond Platinum akiwarusha mashabiki waliohudhuria katika tamasha lake la Diamond Are Forever lililofanyika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Diamond akionyesha umahili wake wa kuimba.
...Kumbe jini kisilani kaingia katika utamu wa penzi langu, alikuwa akiimba
...hapa alikuwa akimwaga mauno mbele ya mashabiki waliohudhuria.
Janeth Sostenes akifanya mahojiano na Godwin Gondwe.
...Aha! madansa wa Diamond wakiwajibika nae
Mashabiki wa kutosha wakifuatilia show.
...Diambond akiwajibika vilivyo
...Madansa wakiwajibika
...Safi sana
...Utata ulianzia hapa pale Dimond alishuka stejini na kwenda kwenye meza waliokuwa wamekaa akina Steve Nyerere na Mboni Masimba na ndipo alipopewa t-shirt ambayo kwa mujibu wa udadisi na uchunguzi wa udadavuzi wa mambo wa Kajuna Blog, ilisemekana kuwa t-shirt hiyo ilikuwa inapicha ya mwanadada ambaye alikuwa akitoa na Diamond kwa sasa. Na ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kumrusha roho Wema Sepetu.
...Mwanadada Mboni Masimba akimkabidhi Diamond t-shirt huku Steve Nyerere akimtunza, vile vile alichukua t-shirt aliyopewa na kuipeleka kwa mwanadada Jokate Mwegelo.
...Hapa akikabidhiwa t-shirt na kupewa maelekezo mahali pa kuipeleka.
...Baada ya hapo kumaliza lile movie la kwanza aliendelea na kupita katika meza mbali mbali huku akiwasalimia wageni waalikwa.
...Akiimba na bendi ya Odama ambayo alimpa ushirikia mkubwa.
...Mauno yamekolea
...Akiendelea kutoa shukrani kwa wageni waliofika kumsapoti.




Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Q-chief akimpa sapoti mdogo wake Diamond

...Ehe! utata mkubwa ambao ulizuka ni hapa ambapo mwanadada huyu alimtuza dola za Kimarekani, Diamond

...Diamond aliendelea kuimba huku mwanadada huyo akimtunza huku akitoa tabasamu na kicheko

Mwadada huyo hapa alikuwa amemaliza na kuondoka kwa mikogo..

Baada ya Diamond kurudi stejini ndipo mwanadada Wema Sepetu alienda kumtuza na pesa zake kukataliwa. Wema alikaa akimbembeleza kwa muda wa dakika 10 japo zoezi lake halikufanikiwa.

...Diamond aliendelea kuwajibika huku Wema akijaribu kumbembeleza

...Bembeleza, bembeleza na wewe jamaa ndiyo aliendelea kuwajibika

...Ndipo alipochukia na kuzitupia hizo hela stejini huku akiondoka huku akiwa amenuna

...Shamim Mwasha akilaumu kitendo alichokifanya Diamond cha kukataa hela alizoenda kutuzwa na Wema... 'Haiwezekani hii ni aibu sana'

Pesa alizokataa kuzichukua zikiwa zimetupwa

...Hapa alipiga kitu cha 'Nimpende Nani'

...Jokate na marafiki zake wakishangilia

...Baada ya tuio hilo kutokea Mange Kimambi alimuita mshereheshaji wa tamasha hilo, Taji Liundi na kumuomba amuite Diamond aje amuombe msamaha na ndipo Diamond akakataa.

...Diamond alishuka na kuelekea kwa mwanadada Jokate Mwegelo na kuanza kukata mauno.

...mwanadada Mboni Masimba akiwa amevaa t-shirt alizokuwa amevaa.

...Aha! nimependeza sana

Taji Liundi akimbembeleza Diamond ili aende nae kwa Wema ndipo Diamond akakataa.




...Mwanadada Mariam (Miss Popular) akimfuta jasho Diamond wakati Taji Liundi akimbembeleza ili aende kwa Wema.

...Diamond akiserebuka na warembo

Marafiki wa Wema Sepetu wakijaribu kumbembeleza wakati akimwaga chozi... huku watu wengine wakishangilia na kuimba aibu yetu au aibu yao???

...hapa mwanadada akijaribu kubembeleza bila matum



aini.
 

Baada ya Barnaba kuimba wimbo wa 'Napembelezwa' ndipo mwanadada Wema alienda kumtuza na kutoa machungu yake. Kwa mujibu wa uchunguzi na maoni ya watu mbali mbali walikiona kitendo cha Wema Sepetu kwenda mbele kumtuza Diamond ni sawa na kujidhalilisha na kuhusishwa na mambo ya kishirikina.
Pia Justmine Loyce Bobbie alisema: Kwanini Wema anamfatafata mtoto wa watu kila kona? amuache na maisha yake jamani.. mbona Diamond hamfatilii lol, YATAMSHINDA
 

Baada ya Barnaba kuimba wimbo wa 'Napembelezwa' ndipo mwanadada Wema alienda kumtuza na kutoa machungu yake. Kwa mujibu wa uchunguzi na maoni ya watu mbali mbali walikiona kitendo cha Wema Sepetu kwenda mbele kumtuza Diamond ni sawa na kujidhalilisha na kuhusishwa na mambo ya kishirikina.
Pia Justmine Loyce Bobbie alisema: Kwanini Wema anamfatafata mtoto wa watu kila kona? amuache na maisha yake jamani.. mbona Diamond hamfatilii lol, YATAMSHINDA

ukistaajabu ya yo yo autayajua ya wema na diamond
 
Back
Top Bottom