Diamond ahukumiwa kwenda Jela miezi 6; alipa faini!

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Diamond%2B%2Bakionyesha%2B%2Bmbwembwe.JPG


Msanii Diamond na mcheza show wake wakiwa nje ya mahakama ya Mwanzo Iringa mjini



MSANII nyota wa muziki wa Kizazi kipya Diamond na wenzake wamekubali kosa la kumshambulia mwandishi Bw. Francis Godwin na kuhukumiwa kwenda jela MIEZI 6 Kila mmoja ama kulipa faini shilingi 50,000 kwa Kila mmoja ikiwa ni Pamoja na kulipa sh. 30,000 kwa Godwin.

Watuhumiwa wamelipa faini japo Francis Godwin hajapokea fedha hiyo na kukusudia kukata rufaa katika mahakama ya juu zaidi
 
Justice served vp akate rufaa au alitegemea kamshtaki jay z ktk mahakama ya usa apate mapene mengi!!!!
 
hii habari haina mantiki kwetu kama ameshalipa faini

Kuna kitu cha kujadili hapa. Wasanii ni watu muhimu katika fani yao kwa jamii. Wanachoshauri , kuhimiza, kutahadhalisha na mengineyo wanatakiwea kuwa mfano kwa matendo yao.

Vyombo vya habari vinafanya kazi kubwa pia kukuza na kutangaza kazi za wasanii, iweje waanza kuvishambulia wakati vyombo hivyo vikiwa kazini? Ni swa na polisi anapolinda usalama wako we unamsahambulia..

Cha ajabu hakuna taarifa ya kulipa gharama za uharibifu wa vyombo vya mwanahabari, wamepata adhabu ya kifungo cha mielzi 6 kama hawatalipa faili hiyo. Inatakiwa walipe gharama ya vifaa vya mwandishi walivyoviharivu, ndio maana anakusudia kukata rufaa mahakama ya juu zaidi.
 
Ujinga mtupu kwenye hii thread! Wewe Candidscope kama ndo francisgodwin tafuta namna nyingine ya kuutangaza mtandao wako
 
Taarifa zinazagaa mitandaoni kuwa yule dogo mwenye mikogo bingwa wa kujikoboa amefungwa jela miezi 6 leo!
 
MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond' na wenzake wamekubali kosa la kumshambulia mwandishi Francis Godwin na kuhukumiwa kwenda jela miezi sita kila mmoja ama kulipa faini ya shilingi elfu hamsini (50,000/=) kwa kila mmoja ikiwa ni pamoja na kulipa shilingi elfu thelathini (30,000/=) kwa Godwin.

Watuhumiwa wamelipa faini hiyo japo mwanahabari huyo hajapokea fedha hiyo na anakusudia kukata rufaa katika mahakama ya juu zaidi
 
afungwe bana tulikamu lile dubwana lake ....nagongana nalo kila siku kwenye chipsi pale kwa hamijei madukani...sasa dogo anakaba sana ....apigwe mvua watu tujipindue kama DEMBA BA....
 
Dimond na mwenzake leo iringa wamehukumiwa kwenda jela miaka 6 kila mmoja ama
kulipa fine Sh 50,000 kila mmoja nakumlipa fidia Francis.
Walituhumiwa kwa kumpiga na ku mwaribia vifaa vyake siku ya 31/12/2011 Iringa.
Source Francis godwin blog.
 
Watuhumiwa wamelipa faini hiyo japo mwanahabari huyo hajapokea fedha hiyo na anakusudia kukata rufaa katika mahakama ya juu zaidi
huyu muandishi wa habari matapishi kabisa....yeye ni mlalamikaji na jamuhuri ndo wenye kesi sasa anakata rufaaa kwa shangazi yake au ...
 
afungwe bana tulikamu lile dubwana lake ....nagongana nalo kila siku kwenye chipsi pale kwa hamijei madukani...sasa dogo anakaba sana ....apigwe mvua watu tujipindue kama DEMBA BA....

,hahahahahah
ukimtaja Demba Ba,kuna watu wanakosa normal blood circulation
 
Siwezi kuishangaa hukumu hiyo, kwani ndizo mahakama zetu na mahakimu tulionao. Kamera kwa malipo ya sh 30,000 ni haki kwa mahakama zetu. Mahakimu wanajidhalilisha wenyewe
 
Back
Top Bottom