Diallo: Rais ajaye awe dikteta mzalendo

Kutokana na kuzoeleka kwa ufisadi Tz hasa katika serikali hii ya awamu ya 4 kiasi cha kufikia hata waandishi wa magazeti hawauzi magazeti yenye uso wa ufisadi kama zamani na hii ni kutokana na ufisadi Tz umekua sio kitu cha kustua kama ilivyokua kipindi cha mwalimu.

Na si kuzoeleka kwenye magazeti tu bali hata hao mafisadi wamezoea na hawaogopi kufisadi nchi hii, kuthibitisha hili tumesikia majibu ya watuhumiwa wakisema maneno kama hela ya 'madafu' ,'vijisenti' ,'ya mboga', na 'za ugoro', sitaki kuamini kwa sababu ya sheria mbovu tu bali BINAFSI naona iko haja ya kupata kiongozi mkali kidogo ambae ni dikteta nikisema dikteta baadhi ya watu wataogopa lakini dikteta ninaemtaka ni yule atakaekua mkali kwa fisadi yoyote yule bila kumwangalia usoni na pia hatacheka na wavivu, kuwatumia vyema wafungwa katika shughuli za uzalishaji mali na si kuotea vitambi jela huku magereza yakitegemea ruzuku kutoka serikalini badala ya magereza kuwa chanzo cha mapato ya serikali. Mara nyingi napenda kuita 'contemporary dictatorship' mwisho wa siku tuione Tanzania ikipaa kiuchumi kama China. Naamini inawezekana

Nini maoni yako mwanajf mzalendo wa nchi hii ya 'TANGAZANIA'.

Karibu
 
Panya Road tu mnawaogopa mnajifungia ndan na wake zenu, akija Rais Dikteta si mtakimbia nchi?
 
Umeongea vitu vya maana sana. Tupate rais ambaye atawaona vijana kama potential resource na si kuwaona mzigo usiobebeka kama inavyowaona serikali ya sasa
 
Rais wa Tanzania anachaguliwa na mafisadi kama walivyomchagua makinda

Na mtajikaanga mkimchagua rais toka ccm ndio mtajuta na kusaga meno maana hawezi kuwatema mafisadi
Itawezekana lowasa aje amfunge pacha wake chenge?au rizi one???
 
Hii si kiroja Bali in hoja nzuri sana,kuna watu wametumia uongozi kama kinga kwa maovu yao na kusema kweli kwa serikali iliyoko madarakani haina uwezo wa kukabiliana na hili kwani yenyewe pia ina mapungufu mengi ya kimaadili kama mawaziri kutanua na mabinti ughaibuni,it is a shame
 
ni kwel kabisa maana watu wanatuibia afu wanakuj n dharau eti na vijisenti mara za mboga na mkuu wa kaya eti za madafu.shit!!!
 
Rais ajae atoke kwenye kundi La Alshabab tuone vipi mafisadi ccm watakua hali gani
 
nakuunga mkono mkuu coz tunahitaji kiongozi dikteta kidogo aisee mwenye maamuzi kamili na siyeyumbayumba na kuteteleka mwenye misimamo ya kweli lakini zaidi ya yote mwenye uwezo wa kukamata majizi majizi yote yanayoifilisi Tanzania yetu kila kukicha....
 
Yeye alikuwa wapi miaka ile wakati akiwa mbunge wa mwanza vijijini??kabla ya kutenganishwa kuwa Nyamagana na Ilemela???
 
Mkuu hujui kuwa bungeni kuna majambazi na wezi wa magari hasa katika mikoa ya kanda ya kaskazini?
Upo obsessed sana na kaskazini .....utakufa na fikra za vichakani ukiwa mjini.Kaskazini ni moto mwingine.
 
Watanzania kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu, tunahitaji Rais atakayeweza kushughurikia wezi je kati ya walioomba kuchaguliwa yupo Rais wa namna hii? Ninegpenda UKAWA wapewe nchi lkn CCM hawawezi kuachia nchi tukomae saana na hawa CCM.
 
Natamani sana kumpata Rais atakaye kuwa na sifa za udikteta ili nchi hii inyooke.
1. Atukimbize mchaka mchaka mpaka tusahau kushinda nyuma ya keyboards kupika uongo na uzushi.
2. Awe na uwezo kutandika voboko watendaji wazembe wazembe.
3. Wazurulaji wote awapeleke JKT au Magereza wakalime mazao mengi nchi iwe na reserve ya kutosha ya chakula.
4. Awe na uwezo wa kunyonga kiongozi yeyote atakaye IFISADI nchi yetu.
5. Awe na uwezo wa kumtimua kazi waziri yeyote atakaye shindwa kuiendesha wizara yake.
6.........
7..........
8.........
n.k n.k
Mengine unaweza kuongezea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom